Lole Gwakisa
JF-Expert Member
- Nov 5, 2008
- 4,735
- 2,265
TARURA inachukua nafasi ya Mhandisi wa Wilaya/Halmashsuri katika kushughulikia barabara.
Kama kuna sehemu Madiwani na Halmashauri zimelalamikiwa kwa miaka mingi, kuingilia michakato ya Ujenzi , kuonba rushwa, kupendelea watu/makampuni kutata tenda basi ilikuwa katika Ujenzi wa barabara nchi nzima.
Wahandisi wa Hamlashauri waligueka kuwa vibarua wa Madiwani na kila siku ni vitisho vya kufukuzwa kazi wasipotii matakwa yao.
Wakandarasi wanaojiamini walisusa kabisa kufanya kazi za Halmashauri.
Ukifanya kazi malipo sharti kwa rushwa, mara hela zote zimeenda kwenye mbio za mwenge, mara kampeni ya madawati, au kampeni ya ujenzi maabara shuleni.
Hivyo basi leo nimecheka sana kuona kichwa cha naneni:
Mameya, wenyeviti walalamikia TARURA
Majira pg 10 leo 9 Oct. 2017.
Nampa heko Rais Magufuli, Madiwani walizoea kugawana kwenye vikao fedha za ujenzi wa barabara.