SoC02 Ujinga wako ni fursa kwa mwingine na Silaha za kukuwa kiuchumi

Stories of Change - 2022 Competition

GueNard

New Member
Aug 25, 2022
1
2
Utofauti wa mawazo kati ya binadamu na binadamu, utofauti kati ya mawazo ya mtu mmoja mpaka mwingine na utofauti wa shida kati ya huyu na na yule, hii ni siraha bora ya kukuwa kiuchumi, licha ya kuwa mambo mengi upelekea watu kuanguka na kushindwa kufanikiwa kiuchumi , je ni vipi Ujinga wako ni fursa kwa mwingine?....

Emu fikiria sigara yenye nembo inayosema ni hatari kwa afya yako hii ndio bidhaa inayoongoza kwa kuuza au kuingiza mapato mengi kwa sekunde, dakika, siku mpaka mwaka, Emu fikiria kuhusu madada poa (malaya) wanaojiuza barabarani, ushawahi kufikiria kuhusu magonjwa ya zinaa yatikanayo na ngono, je ushawahi jiuliza wanaowatumia hao wadada huwa wanajua afya zao? Jibu jepesi ni hapana...kunakipindi unatakiwa ujiulize je wavutaji wa sigara kwa nini wamekuwa mtaji kwa wengine, je umewahi kujiuliza ni kiasi gani wanawatengenezea wamiriki wa makampuni hayo... sitaki kukulazimisha wewe uamini ni kweli kwamba sigari ni hatari kwa afya yako pia sitaki kukufanya uamini kwamba madada poa (malaya) ni chanzo cha magonjwa, kabla ya kuanza kunismini au kabla ya kuanza kujua nilichoandika kina ukweli gani, em anza kufikiria na kuchunguza je ni maisha gani wanaishi makahaba mjini, jaribu kuangalia wamiriki wa makampuni ya sigara wanaishi vipi mjini utakuja kunambia ni kweli UJINGA WA MTU MMOJA NI FAIDA KWA WATU WENGINE.....

“Bia tamu” huu ndo msemo wa taifa na ndio nyimbo bora ya walevi Afrika mashariki kwa sasa, sikatai maneno yao sababu sijui radha ya bia, wimbo huu inaonekana umeongeza mapato kwa makampuni tofauti tofauti ya pombe au bia, wimbo huu unapopigwa kwenye mabaa unafanya matumizi yaongezeke kwa kila mlevi, wimbo huu unapelekea mtu kuinywa bia kwa hisia kali na kupandisha mzuka wakuongeza nyingine, kipindi tunakuwa kulikuwa kuna msemo unasema “TIKISA KAMA IMEKWISHA” utakumbuka pia watu walivyokuwa wakitikisa na wahudumu kuongeza bia nyingie, Kulikuwa na kauli hapo zamani ya “KATA MTI PANDA MTI” sitaki kuzungumzia sana kauli ya nani kamwaga pombe yangu japokuwa pia ni moja ya mjengo wa hamasa ya unywaji. Unywaji wa pombe ni gharama sana na wauzaji walipogundua pesa ni ngumu waliamua kuanza kuuza pombe kwakupima hususani ni vinywaji vikari ukiwa na shilingi mia tano (Tsh 500) utakunywa ukiwa na buku utakunywa yaani unapimiwa kwa kiwango cha pesa yako, je unajua vijana wengi kuanzia asubuhi wanapima ya shilingi ngapi mpaka unapofika muda wao wa kulala kwa uzoefu mdogo tu ni kwamba asilimia kubwa ufanya kazi ili walewe unaweza sema kwa lugha nyepesi wanaifanyia kazi pombe, Sijakwambia usinywe pombe ila tu ni kwamba Ujinga wako ndio fursa kwa Wengine.....

Ni ngumu kunielewa nimelenga kuzungumzia nini kwa sasa lakini hivi, umeshawahi kwenda kwenye vituo vya mabasi kote nchini Tanzania angalia idadi ya wapiga debe utaanza kuelewa kauli ya kwamba Ujinga wako ndio fursa kwa wengine, kuna kipindi ukiwa na safari hasa sehemu ngeni kwako ukifika vituo vya mabasi utapokelewa na watu wenye kauli nzuri na wachangamfu sana kila mmoja akikwambia “twende huku gari flani ndo bora” watoto wa mjini wanakwambia akiri kumkichwa, je ushawahi kujua kila stendi ya mabasi imeajiri wapiga debe wangapi, mi sijui najua na wewe hujui ila jibu letu sote ni wengi, je unajua wewe kutokupanga safari na kujua utapanda gari lipi ndo ajira kwa vijana na wazee walio kwenye mastendi hayo? Je unajua watu wale kwa siku wanaingiza pesa ngapi kupitia ujinga wa abiria, ni pesa nyingi inatengenezwa na watu hao, wapo wenye vipato vyao vizuri kwa siku, wamejenga japo ni vibanda vinavyowafaha wao na familia zao, wanasomesha na wanaacha pesa kwa familia zao, wapo wenye usafiri binafsi kama baiskeri,piki piki mpaka bajaji kwenye upande wa gari sina hakika, wapo wanaomiriki viwanja na biashara ndogo ndogo....lengo langu si kukusanua ili uwe mjanja, kwani ukiwa mjanja unaweza wakosesha riziki ya kila siku wavuja jasho wale.....

Sitaki kuwazungumzia sana madalali wa vyumba, nyumba, magari na vitu mbali mbali, emu fikiria unataka kupanga hususani ni katika mikoa mikubwa, hivi unajua Dar es saalam dalali ana sauti katika upangishaji wa hawali kuliko mmiliki halali wa nyumba? .. je unajua dalali akikupa chumba cha laki mbili na yeye unamkabidhi laki mbili mkononi, watu wengi hawajui kama dalali mwenye dili nyingi zakutosha ni zaidi ya mtu anayelipwa laki tatu kwa mwezi? Sitaki kusema kwamba madalali ni wezi no..! hilo sio lengo langu, dalali ni kiunganishi kati ya mteja na muuzaji na udalali ni kazi halali kabisa na sio kuvunja sheria... nakumbuka kuna siko nipo darasani katika somo la Sheria ya ardhi (land law) mwalimuwa wangu Dr Tenga alisema darasani “madalali wengi wanafanya fanya tu leo mimi nakufundisha wewe ukafanye kazi hii kisomi zaidi” Siku hiyo ndio nilijua uhalali wa watu hao katika kazi zao, Je unajua ukinunua kitu cha laki 5 kwa dalali ujue mwenye kitu alikuwa anataka laki 4 mpaka laki 4 na 70, je unajua kwamba dalali akipiga kipato kidogo kwako upata tena kipato kidogo kwa mmiliki wa mali hiyo... sijasema usinunue kitu kwa dalali usininukuu vibaya....

Bado naendelea kusema Ujinga wako ndio fursa kwa mwingine.......


Je ushawahi kumuona Teja katika maisha yako? Je ushawahi kujiuliza Teja utumia pesa ngapi ili kutuliza alosto (hamu) aliyonayo?.... Je unajua kete moja ya unga inauzwa shilingi ngapi?....Swala sio bei ya unga wala sitaki wewe ujue bei ya kete ya unga, swali la msingi ni pesa ngapi teja ulipa kwa siku ili tu abembee (akate kiu yake) kwa siku tu pesa ndogo kabisa teja hutumia si chini ya shilingi elfu 50, je wamiliki wa biashara hizo unajua wanaingiza pesa ngapi?...Je ushawahi kuona madhara yatokanayo na unga?... Mimi leo nipo hapa kuongelea swala la Ujinga wa mtu unavyokuwa fursa kwa mwingine.

Mitandao ya kijamii (Facebook, WhatsApp, Twitter, YouTube na instagram) unajua kama ni chanzo kikubwa cha mapato kwa wamiliki wa mitandao hiyo, wamiriki hao uitwa mabilionea, tena si mabilionea wa pesa za kitanzania ni wamiliki wa pesa inayoitwa dola bilioni kadhaa.... ili wao waingize pesa ni lazima wewe uweke pesa uibadili kuwa mbs (data) na ushinde ukitumia mitandao hiyo iwe kwa umbeya, hanasa au hata kutangaza biashara, mitandaoni hii haiwezi kutembea bila pesa je unajua kipindi Tanzania kuna Facebook ya bure iliyokuwa ikitolewa na mtandao fulani unajua ilipunguza mapato kiasi gani? Je unajua Facebook ya bure ilipofutwa na mtandao huo fulani ulikuza vipi pato la mmiliki wa Facebook? Sasa jiulize tu Facebook inaunganisha watu wangapi duniani?... je jiulize mtandao huo unapotezea pesa ngapi vijana tusio na pesa hususani katika nchi zetu za kimasikini... kuna kipindi nilikuwa nawaambia washikaji simu ya kupangusa (Smart phone)isiyokuwa na kifurushi (data) ni sawa na kopo au bora uiweke ndani tu, hapa nachotaka kusema bado chanzo cha mapato cha wamiliki wa mitandao hiyo ni ujinga wetu wa kutaka kuchapisha (post) picha na jumbe za vijembe katika akaunti zetu za mitandao hiyo, ni kutaka kuweka memes katika nambari zetu za whatsApp hii si kitu kibaya ila kizazi hiki cha likes na comment kitumia zaidi ya elfu mbili (2000) kwa siku kuweka bando tu kwenye simu ili wakumbane na likes na comment na si kukuza kipato, katika status 20 kwenye simu utakuta 15 ni majisifu, vijembe na bata 5 tu ndo utakuta matangazo ya biashara ndogo ndogo za kukuza uchumi wa mtu, swala bado ni lile lile UJINGA WAKO NDIO FURSA KWA MWINGINE....

Najua umepata tabu sana kuelewa nilikuwa nataka kusema kuhusu nini lakini tumkumbuke Mwl Nyerere katika kauli yake alipowatambulisha maadui watatu wa taifa ili ni Ujinga, maradhi na umasini...pumzika kwa amani Mwalimu...

Maradhi ni zao litokanalo na UJINGA, najua utataka kujua ni kivipi ingawa sio mada yangu kuu ila nitakupa mifano midogo tu utanielewa kiwepesi, mbu ni wadudu waenezao malaria pamoja mtu anaweza kumiliki chandarua ataacha kutumia kwa misingizio cha joto ni ujinga ambao utazaa maradhi, watu wanaonunua madada poa (malaya) wengi upenda kavu kavu na wanajua kabisaa watu wale utumiwa na watu wengi lakini pia awana uwakika na afya zao watawatumia bila kinga sababu tu wanakwambia “utamu wa pipi kula bila maganda” hivyo kauli hizi za kijinga ndio upelekea kwa kuazlisha maradhi kupitia Ujinga wetu huo.

Umaskini ni zao litakanalo na Ujinga wazo ili ndilo linaweza kuja kubeba mada kuu ya andiko ili...Je ni vipi ujinga upelekea umaskini kwa wajinga, matumizi yasiyo na staha ufanya watu kukosa hata akiba kwaajili ya kesho hivyo watu wengi tunashindwa kukuwa kiuchumi na kupata maendele ya kiuchumi na wengi wetu utokana na zao la Ujinga, hivyo upelekeakupata anguko la kiuchumi linalopelekea kushindwa hata kupata mahitaji muhimu ya kibinadamu, yale yatufahayo kila siku, kushindwa kuendeleza tulichonacho sababu ya ujinga pia uleta anguko na anguko ilo ndilo tunaliita Umaskini, kuna baadhi ya watu ambao uwezi wahita wajinga sababu ya maamuzi yao ila vitendo vyao uibua ujinga wao, watu hao ni wale walio katika kundi la uchumi uliopumzika, je mtu aliye katika uchumi uliopumzika ni yupi? Ngoja nikwambie Uchumi uliopumzika ni uchumi ule usiokuwa wala kupungua ukikua hauwezi kuwa na mabadiriko na hata ukiporomoka unakuwa hauna madhara kwa muhusika... mfano mfanyakazi aliyeajiriwa na asitumie mshahara wake kukuza kipato chake kwa kazi nyingine kama, mtu huyo kama kwa mwezi ulipwa laki 5 uitumia pesa hiyo hiyo mpaka mwezi mwingine atakapopata nyingine hataki kuikuza kabisa, kuongezeka kwake utegemea zaidi ongezeko la mshahara wake na marupu rupu ya kazi yake, mtu huyu ndio naweza kumuita mtu mwenye uchumi uliopumzika......

Ujinga pia ulitambulika kama adui mkuu wa taifa la Tanzania, kwani ujinga hasa hufanya au upelekea kuwa na matokeo hasi zaidi kwa mtu mjinga au mjanja yeyote mwenye ujinga ndani yake uweza kupata madhara katika maisha yake. Ujinga mdogo ndio fimbo inayotumika na vyombo vya dola kupoka haki ya mtu na mtu huyo kwa kuwa tu ni mjinga kwa kushindwa kujua haki zake ni zipi na vipi anaweza kulinda haki zake hizo ndipo mtu huyo hukutana na madhira ya kushindwa kulinda na kutetea haki zake hizo, mara kadha wa kadha mtu haki zake uchukuliwa tu bila utaratibu sahihi, tumebaki na maneno yanayoendelea kudhihirisha ujinga wetu mfano; “Namuachia Mungu, waache tu kwani kitawafikisha wapi, vitu vinatafutwa, na kauli kama waache wao si ndio wenye nguvu bana”.

Andiko hili ingawaje halipo zaidi katika kuzungumzia zaidi maswala ya haki, tuendelee zaidi kuongelea uchumi na jinsi ya kukuza uchumi ambao unaweza poromoshwa na ujinga wa mtu, ujinga uweza kuporomosha uchumi wa mtu kupitia matendo mbali mbali yanayosababishwa na ujinga wake huo. Mtu yeyote asiyekuwa na uelewa ni jinsi gani ujinga wake ndio silaha itakayo muangamiza au ujinga huo ni sumu inayomuua taratibu katika uchumi wake ni vigunu kujenga afya ya uchumi wake katika maisha yake ya kila siku. Achana na matumizi yasiyo na tija hasa katika mapambano ya kukuza pato lako wewe kama kijana, jaribu kufikiria bei ya maji ya dukani lita 1 yenye thamani ya Tsh 500, je kila siku ukiwa kwenye harakati unatumia ya pesa ngapi? Muhimu ni kumiriki chuma yako inayotunza maji yanayokutosha Kwa siku husika hii itakusaidia kuongeza pato binafsi, ukiona umeanza kuachana na matumizi ya pesa yasiyo na msingi hata senti moja jua ndio upo katika hatua ya kukua kiuchumi na ndio nafasi yako ya kuachana na ujinga wako ambao utengenezea Pato watu wengine.

Kuna silaha tofauti tofauti zitakazo tumika kumfanya mtu yeyote kuweza kukuza na kusimamisha uchumi wake na wa jamii inayomzunguka kwa kutumia silaha hizi kwa maarifa na utulivu mkubwa katika mbio zake za ukuzaji wa uchumi wake. Tambua hatua hizo ili uweze kuongeza na kukuza uchumi binafsi silaha hizo ni hizi zifuatazo-:

Lengo hii ndio hatua ya awali ambayo umfanya mtu yeyote kukuza Pato lake yeye mwenyewe, nini umuhimu wa lengo? Lengo ndio mwanzo wa njia ya mafanikio kwani huu ndo mwanzo wa mchoro wa mafanikio wa mtu yeyote aliyeamua kubadirika katika jambo lolote lile. Lengo ndio picha inayobeba matumaini, moyo, nia na uthubutu wa kile unachofikiria kufanya, kama ukiweka lengo hakikisha kuna ukomo w muda wa kusimamia lengo ilo itakufanya uweze kufanya kazi Kwa bidii na kwa umakini mkubwa zaidi. Hivyo kabla ujafikiria kufanikiwa lazima ujiandae kuweka lengo linakobeba mafanikio yako.

Uthubutu, kila anayetaka kufanikiwa basi sharti la kwanza ni lazima ufanye uthubutu katika kupigania malengo uliyojiwekea, lengo lako alitakiwi kubaki kichwani tu wala alipaswi kuwa kama ndoto bali unapaswa kubadirisha lengo ilo kuwa picha halisi itakayobebwa na uthubutu, katika kuthubutu kuna kukatishwa tamaa, kuvunjwa moyo na kurudishwa nyuma ili mafanikio yaonekane basi huna budi kutoteteleka katika kile ulichokianza hii ni moja ya silaha itakayokubeba vyema na kukuweka sehemu bora zaidi na uthubutu wako ndio utakaokuweka katika nafasi ya mafanikio au mdondoko wako.

Msimamo, kuamini na kupenda unachofanya msimamo wako katika kile unachopenda na kukiamini ndio moja ya njia bora zaidi kwani ya kuongeza juhudi na morali katika harakati ,unazofanya hivyo upelekea kujali kile unafanya pia kukipa muda na maboresho ya kila siku katika kazi au juhudi zako za kukuza Pato lako hususani ni kijana wa leo.

Pokea ushauri na kubali kubadilika, ushauri wowote ule upelekea kuboresha kile unafanya, ushauri mbaya ukiutumia vizuri ndio chanzo cha kukuza na kukomaza akili yako na kukuwa zaidi kwani ukifanikiwa kuchukuwa ushauri mbaya na ukapambana nao ukafanikiwa kuushinda jua sasa utaweza kuzalisha kilicho bora zaidi kuliko kile ulichonacho, mabadiliko ni kitu cha kawaida katika dunia yetu hii ya sasa kwani mambo hubadilika kila uchwao, ukifanikiwa kwenda na mabadiliko chanya itafanya uweze kuleta faida maradufu kuliko mwanzoni mabadiliko hayo yataleta ubora zaidi katika Moengo na uthubutu wa kile unachotaka na unavyotaka katika kukua na kukuza uchumi.

Chanzo kipya cha mapato, siku zote pato huwa alitoshi na mpambanaji hususa ni vijana hakikisha unaanzisha sehemu mpya itakayo kuongezea pato kwani hii ukupelekea kuweza kuwa na uwezo wa kuinua na kuongeza pato kwani chanzo kimoja kikifeli inawezekana chanzo mbadala cha mapato hivyo inaweza kukubeba pale chanzo kikuu kinaposhindwa kusimama kama awali, hivyo chanzo kipa ni muhimu zaidi.

akiba, Akiba AKiba AKIba AKIBa AKIBA hii ndio silaha ya mwisho ya mafanikio, tunza AKIBA, weka AKIBA, hifadhi AKIBA, kuwa na AKIBA, heshimu AKIBA
 
Back
Top Bottom