Mawazo na ushauri wako vitanisaidia.

slow_learner

Senior Member
Nov 24, 2016
139
110
Habari zenu wana jamvi!

Leo niko hapa ndugu zangu kwa ajili ya kuomba wenu ushauri ya kipi nifanye ili kuweza kukaa vyema kiuchumi.

Kisa changu kinaanzia hapa;
Tangu nilipoacha masomo yangu ya elimu ya chuo kikuu mambo yalikuwa ni magumu kwa upande wangu.
Sikuweza kujua nianzie wapi ili kujikimu kimaisha kwa kuwa sikuweza kuwa na usaidizi wa aina yoyote ile kutoka kwa mtu mwingine.

Kutokana na hali ile ilipelekea kuuza simu yangu ili nipate mtaji wa biashara. Nilipata shs20000 kisha nikatumia nusu ya pesa kununua jiko na wavu na nusu iliyobaki nilinunua mahindi na mkaa.
Kilichonishangaza katika biashara hiyo ni mara baada ya kurudisha pesa ya mtaji bidhaa ilikuwa haitoki; hali hii ilijitokeza kwa siku kadhaa hadi pale nilipochukua uamuzi wa kuachana nayo.

Baadaye niliamua kujihusisha na kazi za migodini kwa kipindi cha mwaka mmoja lakini sikuambulia kitu maana pesa nilidhulumiwa hivyo sikuweza kuendelea kwa lolote lile.

Mwaka 2020 kwa msaada wa rafiki yangu, aliniazimisha shs20000 ambayo niliamua kuitumia kama mtaji na nikaanzisha genge la kuuza matunda.
Nashukuru mambo yaliweza kwenda vizuri kwa kuwa ndani ya mwezi mmoja niliweza kupata pesa ya kulipia eneo la biashara na sehemu ya kulala.

Baada ya mwaka mmoja niliweza kununua kiwanja cha cha thamani ya 700k na pia kukarabati genge langu.
Mambo yalikuwa ni mazuri sana japo changamoto za kibiashara hazijawahi isha ila niliweza kufanya vizuri tu.

Mwaka 2021 nilianza ujenzi na mambo yalikuwa sawia tu japo ni ujenzi wa kuunga unga ila nashukuru maana niliweza kufika kwenye usawa wa linta na niliishia hapo kwanza.

Mwaka 2022 kuna mtu alikuja kuchukua pesa kwangu kiasi cha 800k na kunikabidhi moja ya eneo lake kwa maandishi. Kwa kweli mambo yalikuwa ni mazuri tu. Pia kutokana na mwingiliano mzuri na watu vile vile niliweza kujiunga na kikundi cha kuwezeshana; ambapo kilichangia kwa kiasi kikubwa mimi kuboresha biashara yangu na kumjengea nyumba ya wastani mzazi wangu kabla ya kumalizia ya kwangu. Hii ni kutokana na nyumba ya mzazi wangu kuanguka kipindi cha mvua.

Mwaka 2023 miezi ya mwanzo mambo yalikuwa ni mazuri tu hadi ilipofika mwezi wa sita tarehe za mwanzoni ambapo nilipigwa na tukio zito. Katika kikundi cha kuwezeshana mimi nilikuwa ni mhasibu na kwa hiyo pesa zote nilikuwa nikitunza mimi kabla ya kupelekwa Benki.

Nilipokuwa nakaa na muda wa kukusanya pesa ili kuzipeleka benki havikuwa rafiki hivyo ilikuwa ni lazima nilale nazo na siku inayofuata asubuhi sana pesa ilikuwa ikipelekwa benki. Ila wiki ya kwanza ya mwezi Juni haikuwa nzuri kwa kuwa nikiwa nimelala niliamka mlango umeharibiwa kitasa na baadhi sebuleni hakukuwa na Tv yangu. Nilitahayari sana na ndipo nilipoangalia sehemu ya kutunzia pesa sikufanikiwa kukuta Chochote kile. Dah! Nilipiga ukunga maana nilichanganyikiwa ni kwa namna ipi nitawaaminisha wenzangu lakini haikusaidia Chochote kile.

Nilitoa taarifa kuhusu tukio ila hakuna aliyeweza kunielewa. Kila mmoja alisema zile ni njama za kutaka kuwadhulumu. Sikuweza kuwa na namna yoyote ile zaidi ya kunishinikiza nilipe pesa yao. Kiukweli nisingeweza kulipa maana pesa ilikuwa ni nyingi na mimi kwenye akiba yangu nilikuwa na pesa kidogo tu.

Kiukweli baada ya kuniandama sana sikuwa na chaguo zaidi ya kuamua kuondoka bila taarifa na kuacha kila kitu changu mpaka pale nitakapoweza angalau kupata hata nusu ya pesa ili niwapelekee na nirudi katika hali yangu ya kibiashara. Huku nilipo maisha nayaona ni magumu sana.

Nimejaribu kufanya shughuli katika mji Tunduma lakini hali imekuwa ni mbaya sana. Kwa sasa niko mji Dar Es Salaam na nina kiasi cha Shs100000 tu.

Kama mwana jamvi mwenzangu unaweza nishauri nifanye kitu gani ambacho kitanisaidia kuweza kuikuza pesa hii ili angalau nikuze mtaji na niweze kwenda kulipa pesa ya wanakikundi wenzangu? Nadaiwa shilingi milioni kumi na mbili(12,000,000).

Tafadhali; nimetoa historia kwa ufupi nilipotoka na nilipofikia na jinsi nilivyokwama kwa lengo la kuomba ushauri.
Sina amani ya moyo kabisa mpaka nitakapolipa pesa ya wenzangu maana hata nikisema kuuza mali zangu pesa hiyo haiwezi kufika kwa kuwa mimi mwenyewe nilikuwa najitafuta tu.

Uaminifu ni mtaji japo siaminiki tena ila sitodhulumu mtu.
Nisaidie kwa mawazo ya kunivusha.
Asanteni sana kwa muda wenu.🙏🙏
 
Nenda buguruni sokoni nunua machungwa kwa bei ya jumla tafuta eneo lolote lililochangamka jibanze sehemu ita wateja.
Kama ulinunua 60 tsh au 50 tsh uza 100tsh
 
Ulivyokimbia ndo umeharibu kabisa, deni halifungi mkuu Bora mngeenda kisheria mjue utalipa vipi deni la watu, au uliogopa watakuua

Ila story yako Ina ukakasi sana, kama hutojali naomba unijibu, kwa utandawazi huu inakuaje unalala na milioni 12 ndani tena pesa ya watu, wakala wa bank wamejaa Kila Kona, alafu hiko kikundi chenu mlichanga milioni 12 kwa siku Moja wakakupa wewe au ni pesa ulizokua unapewa kidogo kidogo? Kama ni pesa ulikua unapewa kwa awamu kwanini uweke ndani? Kama mlichanga kwa siku Moja basi mtakua wapumbavu maana kikundi Cha kuchanga milion 12 kwa siku mnakosa akaunti ambayo Ina signatories hata watatu mnapeana hela kishkaji tu?

Kuna kitu unaficha kiufupi nashindwa kuunganisha dots kabisa?? Nahisi utakua uliwapiga tu wenzako tukio samahani lakini
 
Rafiki kabla ya kuchukua maamuzi ya wewe kuondoka eneo hilo haukuweza kuongea nao ili uweze hata kuwalipa pesa zao kidogo kidogo?? Naamini ingekua ni njia nzuri ungeweza endelea na biashara yako hapo hapo
 
Asanteni sana kwa muda wenu.
Duh pole sana kwa changamoto
 
Kwanza nimetoa historia kwa ufupi sana.
Pili watu wana pesa tofauti na wengine tunavyofikiria.
Tatu ni pesa ambayo huwa tunapeleka benki kwa hiyo sikuwa na wasi wasi wowote ule. Kwa maana katika kikundi hiyo ilikuwa ni pesa ndogo tu. Ila kwangu mimi ni kubwa sana.

Halafu kama ni kuwapiga wenzangu ningewapiga pesa ndefu zaidi ya hiyo kwa maana wengi nilikuwa ninawatunzia na unapofika muda wa kuwasilisha nawapatia wanawasilisha.

Mimi siyo mtu wa maneno mengi sana ila kauli na vitisho vyao kiukweli havikuniacha na usalama wa nafsi. Hivyo niliamua kutoka na kuacha kila kitu changu.
 
Rafiki kabla ya kuchukua maamuzi ya wewe kuondoka eneo hilo haukuweza kuongea nao ili uweze hata kuwalipa pesa zao kidogo kidogo?? Naamini ingekua ni njia nzuri ungeweza endelea na biashara yako hapo hapo
Mpaka sasa natamani kurudi na kuendelea na biashara yangu ila vitisho vyao kiukweli havikuniacha salama licha ya kuwasihi nitawalipa kidogo kidogo na kama sitofanikiwa kumaliza kwa wakati watakata kiwango kilichosalia katika akiba yangu kwenye kikundi ila maelewano hayakuwa SAWA.
 
Kwanza nimetoa historia kwa ufupi sana.
Pili watu wana pesa tofauti na wengine tunavyofikiria.
Tatu ni pesa ambayo huwa tunapeleka benki kwa hiyo sikuwa na wasi wasi wowote ule. Kwa maana katika kikundi hiyo ilikuwa ni pesa ndogo tu. Ila kwangu mimi ni kubwa sana.

Halafu kama ni kuwapiga wenzangu ningewapiga pesa ndefu zaidi ya hiyo kwa maana wengi nilikuwa ninawatunzia na unapofika muda wa kuwasilisha nawapatia wanawasilisha.

Mimi siyo mtu wa maneno mengi sana ila kauli na vitisho vyao kiukweli havikuniacha na usalama wa nafsi. Hivyo niliamua kutoka na kuacha kila kitu changu.
Haikua busara kulala na pesa za watu ambazo ni "nyingi' kwako kama unavyosema!! Hata matajiri siku izi unakuta nyumbani ana kama laki 3 tu... Anyway Liwe funzo kwako na pole kwa masaibu
 
Hakika sitokuja rudia kosa kama hilo japo kuna muda mtu huwezi kuepuka kuwa na kitu kulingana na muda na mahali
Asante kwa pole
 
Mdaiwa hafungwii ungekomaa tu wangekusumbua mwishowe wangepoa kosa ulilofanya ni kukimbia tatizo baada ya kutatua,na kuendelea na biashara yako hakuna kazi ngumu Kama kuanza biashara mpya.ushauri wangu biashara ulivyokua unaifanya kule iendeleze huku.
 
Mpaka sasa natamani kurudi na kuendelea na biashara yangu ila vitisho vyao kiukweli havikuniacha salama licha ya kuwasihi nitawalipa kidogo kidogo na kama sitofanikiwa kumaliza kwa wakati watakata kiwango kilichosalia katika akiba yangu kwenye kikundi ila maelewano hayakuwa SAWA.
Pole sana ila naona kama anguko lako umelisababisha wewe mwenyewe. Kama umeliweza kunyanyuka kutoka chini mpaka ukanunua kiwanja na kumjengea mzee wako kibanda sioni ni kwa nini una-panick. Anza tena kutoka chini na utanyanyuka.
 
Ni kweli kabisa kuna muda nafikiria hivyo ila kiukweli sijawah ingia matatani kiasi hicho na ndiyo maana nina wasiwasi sana.
 
Ulivyokimbia ndo umeharibu kabisa, deni halifungi mkuu Bora mngeenda kisheria mjue utalipa vipi deni la watu, au uliogopa watakuua

Ila story yako Ina ukakasi sana, kama hutojali naomba unijibu, kwa utandawazi huu inakuaje unalala na milioni 12 ndani tena pesa ya watu, wakala wa bank wamejaa Kila Kona, alafu hiko kikundi chenu mlichanga milioni 12 kwa siku Moja wakakupa wewe au ni pesa ulizokua unapewa kidogo kidogo? Kama ni pesa ulikua unapewa kwa awamu kwanini uweke ndani? Kama mlichanga kwa siku Moja basi mtakua wapumbavu maana kikundi Cha kuchanga milion 12 kwa siku mnakosa akaunti ambayo Ina signatories hata watatu mnapeana hela kishkaji tu?

Kuna kitu unaficha kiufupi nashindwa kuunganisha dots kabisa?? Nahisi utakua uliwapiga tu wenzako tukio samahani lakini
Hata mimi naona kama kuna kitu anaficha japo sina uhakika. Huenda kuna mtu alimwambia kuna deal la kuingiza fedha chap chap, akatumia hizo fedha za chama ili afanye deal, achukuwe faida na fedha za chama zibaki, lakini mambo yakaenda sivyo. Watu wengi wanaotunza fedha za vyama huwa wanaangukia kwenye mtego kama huu. Yaani alilala na fedha nyingi namna hiyo na wezi wakaingia na kuchukuwa fedha tu bila yeye kusikia? Anyways, ni hisia zangu tu na anaweza kuwa anasema ukweli.
 
Pole mkuu bahati nzuri unajituma Mungu atakubairiki.
Ulichokosea ni kukubali ukae na 12M ndani kirahisi sana wakati ulijua likitokea lolote hutaweza kuzilipa, hivyo ulivyoondoka wenye pesa zao ndo wanaamini kabisa umewaibia japo hata ungebaki wangeendelea kuamini ni mchongo.
 
Back
Top Bottom