Yese Kajange
New Member
- Oct 24, 2018
- 4
- 13
Bawasiri ni ugonjwa unaotokana na kuvimba kwa mishipa ya damu iliyopo ndani au katika eneo linalozunguka njia ya haja kubwa. Pia bawasiri unaweza kusababisha kujitokeza kwa kinyama kwenye njia ya haja kubwa au puru.
AINA ZA BAWASIRI.
Kuna aina mbili za bawasiri nazo ni
1. Bawasiri ya ndani
Ni kuota kinyama au uvimbe sehemu ya ndani ya haja kubwa. Mara nyingi huambatana na Maumivu makali pamoja na kutokwa na damu wakati wa kujisaidia haja kubwa.
2. Bawasiri ya nje
Ni kuota kinyama sehemu ya nje ya haja kubwa/puru hata Kama aujaenda kujisaidia.
DALILI ZA MTU MWENYE BAWASIRI.
1. Kupata muwasho mkali katika eneo la juu la puru/haja kubwa.
2. Kujitokeza kwa kinyama au uvimbe eneo la haja kubwa/puru.
3. Kupata kinyesi chenye damu.
4. Kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia.
5. Kupata maumivu ya tumbo na kiuno hasa pale bawasiri inapokua katika hali mbaya.
MAMBO AMBAYO YANAWEZA KUSABABISHA MTU KUPATA BAWASIRI.
1. UJAUZITO;
Wajawazito hupata bawasiri kutokana na sababu zifuatazo:
(i). Uzito kuzidi & mgandamizo
Mwanamke mjamzito huongezeka uzito na mgandamizo sehemu ya haja kubwa/puru kwasababu ya uzito wa mtoto, ukuaji wa mwili pamoja na kizazi ( uterus) hali hii hupelekea mgandamizo sehemu ya haja kubwa na kusababisha mishipa ya damu midogo midogo (veins) kuvimba na kupasuka hivyo kupelekea kuota kwa kinyama,kutoa damu, Maumivu makali na muwasho ambavyo ni viashiria vya bawasiri.
(ii). Kula udongo
Baadhi ya wajawazito hula sana udongo. Ulaji wa udongo hupelekea mjamzito kupata choo kigumu ambapo choo kigumu husababisha mgandamizo sehemu ya haja kubwa/puru.
2. UZITO KUPITA KIASI;
Ni moja ya sababu ya mtu kupata bawasiri kwasababu uzito mkubwa hupelekea kutokea mgandamizo katika mishipa ya damu (vein), sehemu ya haja kubwa/puru hivyo kusababisha kupasuka au kuvimba kwa mishipa ya damu kwenye njia ya haja kubwa. Hivyo kusababisha kujitokeza kwa kinyama au uvimbe ukiambatana na damu, maumivu na muwasho.
3. KUKAA KWA MUDA MREFU SEHEMU NGUMU;
Ni sababu ya mtu kupata bawasiri kwasababu kukaa sana sehemu ngumu hupelekea kutokea kwa mgandamizo mkubwa sehemu ya puru / haja kubwa. Hali hii husababisha mishipa ya damu ( vein) ambayo ipo eneo la haja kubwa kuvimba na kupasuka hivyo kupelekea mtu kupata bawasiri.
4. UNYWAJI WA POMBE;
Pombe husababisha bawasiri kwa namba kuu mbili.
(i). Pombe husababisha upungufu wa maji Mwilini.
Pombe ina kemikali ya lupolin ambayo huathiri mfumo wa homoni katika ubongo, huathiri homoni inayodhibiti upotevu wa maji mwilini (anti - diuretic hormone) hivyo kusababisha mwili kupoteza maji mengi. Hivyo kusababisha mtumiaji wa pombe kujisaidia choo kigumu na kupelekea mgandamizo sehemu ya haja kubwa/puru na kusababisha mishipa ya damu ya eneo Hilo kupasuka/ kuvimba hivyo mtu kupata bawasiri.
(ii). Pombe husababisha presha ya damu.
Pombe husababisha mwili kuzalisha homoni iitwayo endothilin ambayo huingia kwenye damu na kusababisha kusinyaa kwa mishipa ya damu ( vasoconstriction of blood vessels). Kusinyaa kwa mishipa ya damu hupelekea presha ya kupanda na baadae husababisha mishipa ya damu ambayo ipo sehemu ya haja kubwa kupata stress/straining na kupelekea kuvimba/kupasuka; Kwasababu ipo eneo la haja kubwa ambalo huwa na mgandamizo wakati mtu anakaa au kujisaidia.
Hivyo ndivyo pombe husababisha bawasiri kwa hiyo Kama una bawasiri halafu unakunywa pombe kupona ni ngumu sana unaweza kutumia dawa za kila aina bila mafanikio.
5. KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE;
Kuingiliwa sehemu ya haja kubwa ni sababu ni sababu ya mtu kupata bawasiri kwasababu sehemu ya haja kubwa ni sehemu maalumu kwaajili ya kutolea haja kubwa hivyo kuingiliwa sehemu sehemu hiyo hupelekea mgandamizo na kupasuka kwa mishipa ya damu kwasababu ya ufinyu wa eneo Hilo la haja kubwa/puru. Hivyo hupelekea mtu kupata bawasiri.
Huu ni mchezo mfachu Sana na wengi ambao huufanya mchezo huu kufikia hatua ya kupata kansa ya utumbo ( colorectal - cancer ) hivyo watu wajiepushe.
6. KUJISAIDIA CHOO KIGUMU;
Ni moja ya sababu za watu kupata bawasiri kwasababu mtu hutumia nguvu nyingi wakati wa kujisaidia hivyo hupelekea mgandamizo wa mishipa ya damu sehemu ya haja kubwa/ puru hali hii hupelekea kupasuka/ kuvimba kwa mishipa ya damu na kusababisha bawasiri.
Miongoni mwa sababu za mtu kujisaidia choo kigumu ni pamoja na hizi zifuatazo:
(i). Ulaji duni - kutohusisha vyakula vyenye nyuzinyuzi ( fibres) katika mlo Kama vile mbogamboga na matunda, kutokunywa maji ya kutosha, kula vyakula vilivyokobolewa kama sembe na wali bila kuhusisha vyakula vya kusaidia mmeng'enyo wa chakula ili uweze kupata choo vizuri.
(ii). Vidonda vya tumbo - husababisha mtu kujisaidia choo kigumu kwasababu vidonda vya tumbo huathiri mmeng'enyo wa chakula na kupelekea kapata choo kigumu.
(iii). Ngiri/hernia - husababisha mtu kujisaidia choo kigumu kwasababu ngiri huathiri mmeng'enyo wa chakula na kupelekea kupata choo kigumu hivyo kusababisha bawasiri.
ATHARI ZA BAWASIRI.
1. Upungufu wa damu mwilini.
2. Kutokwa na kinyesi bila kujitambua.
3. Kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa.
4. Kupungukiwa na nguvu za kiume
5. Kupungukiwa na uwezo wa kufanya kazi kutokana na Maumivu.
6. Kupata tatizo la kisaikolojia.
7. Kutopata ujauzito.
8. Kupata kansa ya utumbo.
9. Mimba kuharibika.
10. Mwili kudhoofika.
MUHIMU.
- Usipojua chanzo Cha bawasiri yako au kutatua chanzo hicho basi unaweza kuhangahika na bawasiri hata kwa zaidi ya miaka kumi.
- Bawasiri ni athari ambayo unaashiria Kuna tatizo hivyo tibu au jiepushe na chanzo.
USHAURI.
Kama kazi unazofanya hupelekea kukaa kwa muda mrefu basi jitahidi kusimama kwa muda wa dakika 10 mpaka 15 kila baada ya masaa mawili, hii itakusaidia kupunguza mgandamizo sehemu ya haja kubwa/puru na kujiepusha kupata bawasiri.