Uchambuzi wa kitabu The Fountainhead (Jinsi ya Kuishi Maisha ya Ndoto Yako Licha ya Kupingwa na Jamii)

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,811
3,102
Kila mtu huwa anakuwa na ndoto kubwa ya maisha yake katika hatua fulani ya maisha.

Wengi hupata ndoto hizi kati ya miaka 7 mpaka kumi.

Muulize mtoto yeyote kwenye umri huo na atakuambia wazi anataka kuwa nani akiwa mkubwa.

Lakini mfuate mtoto huyo huyo miaka 10 baadaye na muulize anataka kuwa nani, utaona utofauti mkubwa. Kwanza hatakuwa anajiamini kama mwanzo na pili atakuwa amebadili anataka kuwa nani.

Hapo unajua jamii imefanya kazi yake na imefaulu.

Jamii huwa ina kazi moja kubwa, kuhakikisha inaua ndoto kubwa za watu na kisha kuwataka wawe kawaida, wawe kama watu wengine.

Lakini kwenye kila jamii kuna watu huwa wanakataa nguvu hiyo ya jamii kuua ndoto zao. Hawa ni wachache ambao wanaendelea na ndoto zao lisha ya kupingwa na jamii nzima.

Watu hawa hupitia kipindi kigumu sana, huku wenzao waliokubaliana na jamii wakionekana kuwa na maisha mazuri. Wengi wanaojaribu njia hiyo hukata tamaa na kurudi kuungana na jamii.

Lakini wachache sana huendelea na safari hiyo, licha ya magumu wanayopitia na hawa ndiyo wanaoleta mabadiliko makubwa kwenye jamii na hata kufanikiwa sana.

Hiki ndiyo tunajifunza kwenye riwaya inayoitwa The Fountainhead iliyoandikwa na mwandishi Ayn Rand.

Fountainhead.jpg

Riwaya hii inaonesha maisha ya vijana wawili ambao wanaanzia sehemu moja, wote wanasomea taaluma moja, mmoja anachagua kuifuata jamii inataka nini na mwingine anachagua kusimamia ndoto yake.

Howard Roark ni kijana ambaye ameamua kusimamia ndoto yake, anafukuzwa chuoni kwa kuwa na msimamo wa kile anachotaka na kukataa kufuata kile jamii inataka. Walimu wake wanamuona ni mtukutu na asiyerekebishika.

Peter Keating ni kijana ambaye anataka sana mafanikio na umaarufu na anachagua kufuata kile jamii inataka ili kupata mafanikio hayo. Anahitimu Chuo akiwa na ufaulu mkubwa, lakini ufaulu huo hajaupata kwa juhudi zake, bali kwa kufanyiwa kazi na wenzake.

Vijana hao wawili wanaingia kwenye ulimwengu wa kazi ya usanifu majengo (Architecture). Kwa kuwa Peter ana ufaulu mzuri, anapata kazi kwenye kampuni kubwa ya usanifu. Na kwa kuwa Howard hakuhitimu masomo, anaamua kwenda kuomba kazi kwa msanifu majengo ambaye kwa viwango vya kijamii anaonekana kushindwa.

Kwenye ulimwengu wa kazi, Peter anafanikiwa mapema, anajifunza njia ya kufanikiwa mapema ni kuipa dunia kile inachotaka, kuwahadaa watu na kuwatumia wengine kupanda ngazi. Mfano alipotaka kupanda cheo kazini, alihakikisha aliyepo kwenye cheo hicho ameondoka kwenye kazi hiyo ili achukue yeye. Pamoja na kutokuwa na uwezo mkubwa wa kusanifu, alitumia kazi za wengine kujipatia sifa. Njia hizo zinampa mafanikio makubwa mapema, lakini hawezi kuyafurahia mafanikio aliyoyapata.

Howard njia yake inakuwa ngumu mno. Amegoma kuwapa watu kile wanachotaka, badala yake anasimamia kile ambacho anajua ni sahihi. Anapingwa na jamii ya wasanifu majengo kwa kuchagua kufanya majengo ya kisasa (modern) badala ya majengo ya kizamani (classical). Anakosa kazi kwa kuwa hakubali kupangiwa na wateja kile ambacho anajua siyo sahihi. Na hili linampelekea kuwa na maisha magumu, wakati mwingine kulazimika kufanya kazi za nguvu ili apate fedha ya kuendesha maisha yake.

Mwisho wa siku, mafanikio aliyoyapata Peter yanaondoka kama yalivyokuja, kwa kuwa mafanikio yake yalitegemea zaidi watu, watu hao waliweza kumnyang’anya mafanikio waliyompa.

Howard anafikia mafanikio makubwa na ya kudumu, kwa sababu mafanikio yake yanategemea uwezo mkubwa ulio ndani yake, hakuna anayeweza kumnyang’anya mafanikio hayo.

Kuna mambo mengi sana ya kujifunza kwenye kitabu ambayo yatakusaidia sana kwenye safari yako ya mafanikio.

Utajifunza jinsi jamii inavyofanya kila njia kuhakikisha huwi tofauti na ukafanikiwa.

Utajifunza jinsi mafanikio yako yanaweza kuwa hatari kwa wengine na hivyo wakahakikisha hufanikiwi.

Utajifunza jinsi mafanikio ya haraka ya wengine, ambayo hayatumii misingi sahihi yanakuja kuwatesa.

Utajifunza mchango au mkwamo unaoweza kuletwa na watu wa karibu yako.

Na muhimu zaidi utajifunza kwamba uvumilivu na ung’ang’anizi, siku zote huwa unalipa, japo mambo hayawi rahisi, ila yanawezekana.

Kitabu hiki ni muhimu sana kwa wale wote ambao wamechagua kuishi maisha ya ndoto zao, wale waliokataa kuwa kawaida, waliokataa kufuata mkumbo na wamechagua kuwa wao.

Kitabu hiki ni mwongozo sahihi kwa wale waliokataa ajira au walioamua kuondoka kwenye ajira ili kwenda kujiajiri.

Kitabu hiki kinatoa mwanga kwa wale ambao wana ndoto kubwa, ila kila anayewazunguka wanamwambia hawezi au haiwezekani na aache kujidanganya na awe na maisha ya kawaida.

Usikubali hata kidogo kuzika ndoto yako, usikubali kuendelea na kazi au biashara unayoifanya na usikubaliane na wale wanaokuambia huwezi au haiwezekani.

Unapoamua kweli, hakuna kinachoshindikana, na hili ndiyo tunajifunza kwa kina kwenye kitabu cha The Fountainhead.

Nimekichambua kitabu hiki kwa kina kabisa, kikiwa na mafunzo mengi ya safari ya mafanikio na katika sehemu nne za safari hii ya mafanikio. Kazi ni kwako kupata uchambuzi huu wa kitabu, kuusoma na kufanyia kazi ili uweze kuishi maisha ya ndoto yako.

Karibu kwenye channel ya SOMA VITABU TANZANIA, upate uchambuzi wa kitabu The Fountainhead na vitabu vingine zaidi ya 100.

Chagua kuishi maisha ya ndoto yako, pata kitu cha kusimamia ili jamii isiweze kukuhadaa na kukuangusha. Soma uchambuzi wa kitabu The Fountainhead na utumie kuwa mwongozo kwenye safari yako ya mafanikio.
 
Nimejifunza kitu kipya hapa.
Pia machapisho yako yamekuwa msaada sana kwangu (bilashaka na kwa wengine)
Endelea kutuelimisha Mkuu,poor members response isikuvunje moyo.
Usiku Mwema.
 
Asante sana Mkuu.
Karibu tuendelee kuwa pamoja katika kujifunza na kupiga hatua zaidi.
 
Back
Top Bottom