Jinsi Ya Kuishi Maisha Ya Kitajiri Kwa Kuanzia Hapo Ulipo Sasa

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,812
3,105
Rafiki yangu mpendwa,

Kwenye harakati za kujenga utajiri na uhuru wa kifedha, huwa ni rahisi sana kujisahau kuyaishi maisha.

Ni mpaka pale mtu anapofikia lengo alilokuwa nalo ndiyo anagundua hapati furaha aliyotegemea angeipata.

Tatizo siyo kwamba utajiri na uhuru a kifedha hauleti furaha, bali tatizo ni watu kusahau kuyaishi maisha yao.

ISHI-MAISHA-1024x576.jpg

Mwandishi Ramit Sethi kwenye kitabu chake kinachoitwa I WILL TEACH YOU TO BE RICH ametufundisha jinsi tunavyoweza kuyaishi maisha ya kitajiri kwa kuanzia pale tulipo sasa, ili tunapojenga utajiri na uhuru wa kifedha, tuwe na maisha bora pia.

Karibu tujifunze kutoka kwenye sura mbili za mwisho za kitabu hicho na kuweza kuyaishi maisha ya kitajiri huku tukijenga na kutunza utajiri ambao unatupa uhuru kwenye maisha yetu.

SURA YA 8; BORESHA NA KUZA MFUMO WAKO.

Baada ya kufanya kazi kubwa ya kujenga mfumo wako wa kifedha, kinachofuata ni kuboresha na kukuza mfumo wako.

Kwa mfumo wa suluhisho la asilimia 85 ambao ndiyo mwandishi anatumia, kama umefanyia kazi yote ambayo umeshajifunza mpaka sasa, kuna maeneo manne ambayo tayari umeshachukua hatua;

I. Umeshaweka vizuri mpango wa kutoka kwenye madeni kama unayo.

II. Umeshaweka vizuri akaunti zako za benki kwa kuwa na zile unazohitaji na kupunguza gharama.

III. Umeshaweka mpango wako sahihi wa matumizi ili usiwe na hatia wala majuto.

IV. Umeshafungua akaunti zako za uwekezaji na kuanza kuwekeza.

Hayo ndiyo maeneo ya msingi kabisa ambayo kitabu hiki kinapaswa kuwa kimekusaidia kuyajengea mfumo wa kuweza kuyafanya moja kwa moja bila ya hisia na tabia zako kuingilia.

Kinachofuata ni kufanya hayo kwa ukubwa zaidi ili kuweza kupata matokeo makubwa zaidi.

Na kinachohitajika ili kupata zaidi ni wewe kulisha zaidi huo mfumo wako. Unalisha mfumo wako kwa kuwekeza kwa ukubwa na kurudisha vizuri uwiano wa mfumo wako.

Kutathmini na kuboresha mfumo wako.

Kadiri muda unavyokwenda, vitu huwa vinabadilika. Hivyo kila baada ya kipindi fulani unapaswa kujifanyia tathmini kwenye mfumo wako na kuboresha maeneo ambayo yamevurugika.

Maeneo ya kuzingatia wakati wa tathmini na kuboresha ni kama ifuatavyo;

1. Mpango sahihi wa matumizi.

Hapa hakikisha uwiano unaendelea kuwa sawa kama ulivyopanga. Kumbuka;

i. Matumizi ya msingi – 50 – 60%

ii. Akiba – 5 – 10%

iii. Uwekezaji – 10%

iv. Matumizi ya raha 20 – 35%

Hakikisha unaendelea kubaki kwenye uwiano huo ili maisha yako yaweze kuwa bora wakati unajenga utajiri.

2. Punguza gharama kwenye matumizi, mikopo na benki.

3. Fanya uwekezaji kwenye mfuko wa mafao, mifuko binafsi na maeneo yenye unafuu wa kodi.

4. Ondoka kwenye madeni kwa kuwa na mpango na kuomba punguzo.

5. Ongeza kipato kwa kuomba ongezeko la mshahara na kuanza biashara ya pembeni kwa walioajiriwa na kukuza mauzo kwa wafanyabiashara.

6. Zingatia mambo mengine muhimu kama kuwa na bima na kuandika wosia pale unapokuwa na wategemezi.

Ili kuepuka makato ya kodi ambayo yanapunguza ukuaji wa uwekezaji, epuka sana kuwekeza na kuuza uwekezaji mara kwa mara. Wekeza kwa muda mrefu bila kutoa ili utajiri uweze kukua.

SOMA; Jinsi Ya Kutajirika Ukiwa Umelala.

SURA YA 9; MAISHA YA KITAJIRI.

Maisha ya kitajiri siyo tu kwa upande wa fedha, bali kuna pande nyingi za maisha ambazo mtu unapaswa kuzizingatia, hasa pale unapokuwa umeanza kujenga utajiri kwenye maisha yako.

Baadhi ya mambo ya kuzingatia kwenye maisha wakati unajenga utajiri ni kama ifuatavyo;

1. Maisha ya kitajiri ni wewe kuziishi ndoto ambazo umekuwa nazo kwa muda mrefu na siyo kuiga matumizi ya wengine. Ukiishi ndoto zako, utajiri utakutosheleza, ukiiga wengine, utajiri hauwezi kukutosheleza.

2. Unapoanza kuwa na utajiri, utashauriwa na watu wengi sana kuhusu nini ufanye na fedha zako. Cha kushangaza, wengi watakaokuwa wanakushauri hawajaweza kuwa na fedha kama ulizonazo wewe, lakini watasisitiza unapaswa kuwasikiliza. Usiwe na kiburi au dharau kwao, lakini baki kwenye mpango wako badala ya kuhangaika na mipango ya wengine.

3. Unapojenga utajiri, mahusiano yako na watu wako wa karibu yatabadilika sana. Kuna ambao wataingiwa na hali za wivu na chuki kwa namna ulivyopiga hatua kuliko wao. Kuna ambao wataona wanastahili sana kunufaika na utajiri wako. Usiumizwe na hayo yote, wahurumie hao wote kwa sababu hawajui yale unayojua wewe, lakini usikubali kuyumbishwa nao.

4. Unapowasaidia watu wako wa karibu kwenye eneo la fedha, usiishie tu kuwapa fedha, wasaidie pia kujenga mfumo wao wa kifedha. Kama ambavyo wewe umeweza kujenga mfumo wa kifedha kwa mafunzo ya kitabu hiki, wasaidie na wao pia. Wasaidie waondoke kwenye madeni, wadhibiti matumizi na wawekeze. Kama unawapa tu watu fedha bila kuwasaidia kwenye hiyo misingi, wataishia kuwa tegemezi kwako milele, kitu ambacho kitaathiri ukuaji wa utajiri wako.

5. Kuwa makini kuhusu kuwaambia watu kuhusu kipato chako na thamani ya utajiri wako. Wengi wanaweza kuona kwa nje una utajiri, ila wanapojua namba halisi, ambayo labda ni kubwa kuliko wanavyodhani, inaweza kujenga hali ya wivu na kuonekana una kiburi.

6. Ndani ya familia, wewe na mwenza wako mnapaswa kuwa na malengo ya kifedha kwa familia. Lazima wote muwe na maono yanayofanana na mnakwenda sawa. Kama mmoja atakuwa na nidhamu ya fedha na mwingine hana, familia haiwezi kuwa imara.

7. Kwa manunuzi yote makubwa unayofanya, kama ya gari na nyumba, hakikisha unafanya utafiti wa kutosha ili upate kilicho bora na kwa gharama nafuu. Ukifanya manunuzi hayo kwa gharama kubwa, inaathiri sana utajiri wako. Pia unapofanya manunuzi hayo, hakikisha unakaa nayo kwa miaka mingi, angalau miaka 10. Ukiwa mtu wa kununua na kuuza ndani ya muda mfupi, unaingia hasara kubwa.

8. Nyumba ya kuishi siyo uwekezaji, bali ni matumizi. Hiki ni kitu ambacho watu wengi huwa hawapendi kusikia na huwa ni mada inayoleta ubishani mkali sana. Lakini unapoangalia kwa misingi ya uwekezaji, hakuna riba au gawio unalopata kutoka kwenye nyumba ya kuishi, zaidi ya gharama unazoingia kwenye kuitunza. Wapo wanaosema kodi ambayo ungelipa ndiyo faida unayopata kwenye nyumba, lakini ukweli ni matumizi unayokuwa nayo kwenye nyumba yako binafsi ni makubwa kuliko ungekuwa umepanga. Hili halimaanishi usiwe na nyumba, unapaswa kuwa nayo, lakini usiihesabie kama uwekezaji. Badala yake hakikisha unakuwa na uwekezaji mwingine mkubwa nje ya nyumba ya kuishi.

9. Utajiri siyo kwa ajili yako binafsi, bali unapaswa kurudisha utajiri wako kwenye jamii kupitia utoaji. Na utoaji siyo mpaka uwe na fedha nyingi, chochote kidogo unachoweza kutoa na kikawasaidia wengine ni vizuri kufanya hivyo. Na hata kama huna fedha za kutoa, toa ujuzi wako, muda wako na mengine katika kuwasaidia wale wenye uhitaji.

10. Kila mtu anaweza kuwa na utajiri kwenye maisha yake, muhimu ni kujua utajiri una maana gani kwako kisha kujenga mfumo wa utajiri utakaokuwezesha kuwa na fedha ya kuishi maisha ya kitajiri kwako. Mahangaiko ambayo wengi wanakuwa nayo kwenye utajiri ni kuiga maisha ya wengine badala ya kuishi maisha halisi kwao.

Zingatia haya uliyojifunza hapa ili uweze kuishi maisha ya kitajiri, kwa kuanzia hapo ulipo sasa na kuhakikisha maisha yako yanakuwa bora.

Masomo yote ya kujenga utajiri kutoka kitabu kinachoitwa I WILL TEACH YOU TO BE RICH kilichoandikwa na Ramit Seth yanapatikana kwa kubonyeza MAANDISHI HAYA.

Hapo chini ni kipindi cha ONGEA NA KOCHA ambapo tumekuwa na mjadala mzuri kuhusu somo hili. Fungua ujifunze kwa kina na kupata shuhuda za wengine.

View: https://youtu.be/QBQbzy-i2N0

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.
 
asante sana life coach kwa madini muhimu
 
Back
Top Bottom