Almalik mokiwa
Senior Member
- Jun 5, 2020
- 147
- 157
Kwa mataifa mengi duniani, imekuwa kawaida watawala kutumia mifumo ya kiutawala inayokiuka misingi ya utawala bora. Katika kukuza na kudumisha utawala unao zingatia zaidi uhuru wa kujieleza, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa mahakama, uwazi, haki na umoja, ushirikishwaji wa wananchi na utawala wa sheria, dhana ya uwajibikaji siyo ya KUEPUKIKA. Na hii ndio huchora tafsiri halisi ya dhana ya utawala bora.
Tanzania ni moja ya nchi zenye viashiria vya kudhoofika kwa misingi ya utawala wa sheria, uhuru wa kujieleza, uhuru wa mahakama, kusheheni kwa matukio ya ufisadi na rushwa, kukosekana kwa uwazi, uwajibikaji MBOVU wa viongozi wa umma, ushirikishwaji hafifu wa wananchi katika kuamua, kudhoofika kwa uhuru wa vyombo vya habari na kuzorota kwa umoja na haki unaotokana na migongano ya tofauti za kiitikadi. Uchambuzi huu utaenda kugusa moja kwa moja ni kwa namna gani mifumo ya uendeshaji wa kiutawala umekuwa ukikiuka misingi ya utawala bora, na namna ya kuuendea utatuzi wake ili kuhuisha na kusimika nguzo ya utawala bora.
Licha ya Tanzania kutumia mfumo endeshi wa kidemokrasia kama nyenzo kuu ya kupitia ili kudumisha utawala ambao unaitanabaisha serikali kuwa serikali ya watu, inayoipa mamlaka makubwa wananchi katika kufanya maamuzi, lakini bado imeonekana kuwa ni demokrasia iliyochujwa kutokana na ubabaishaji katika kufatwa kwa kanuni zake.
Mambo machache, yanayo dhoofisha utawala bora ni kama ifuatavyo;
Kudhoofu kwa uhuru wa vyombo vya habari;
Tanzania imekuwa ikiingia katika ukakasi juu uhuru wa vyombo vya habari, ambapo umeonekana kuzorota kutokana na kujitokeza kwa matukio mbalimbali ambayo yamekuwa yakitishia usalama wa waandishi wa habari. Mwishoni mwa mwaka 2017, vichwa vya habari vya magazeti mbali mbali nchini, viliripoti taarifa ya kupotea katika mazingira ya kutatanisha kwa mwandishi machachari wa habari za uchunguzi aliyekuwa akihudumu katika gazeti la Mwananchi, ndugu Azory Gwanda. Matukio hayo yamekuwa yakiendelea kujitokeza ambapo waandishi wengine hasa wa habari za uchunguzi, kama Stan Katabalo, Daudi Mwangosi, Josephat Isango na Ben Sanaane kupotea na maisha yao kuwa katika mashaka. Waandishi hawa machachari wameonekana kuingia mashakani hasa baada ya kuonekana wakihoji juu ya utendaji na uwajibikaji wa viongozi wa umma. Kutungwa kwa sheria kandamizi za habari zinazowapa karaha waandishi wa habari na kufifisha utendaji na uwajibikaji wao katika kuuhabarisha umma. Mfano , sheria ya makosa ya kimtandao ya 2015 pamoja na kanuni za maudhui ya mtandaoni ya mwaka 2018.
Picha kutoka StockImages
Kuzorota kwa uwazi, uwajibikaji na ushirikishwaji wa wananchi
Kumekuwa na ushirikishwaji mdogo wa wananchi katika kushiriki kwenye shughuli za maendeleo ya nchi, kama vile ushiriki katika uundaji wa bajeti ya taifa, kama katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilivyo ainisha katika ibara ya 8, vile vile kudogodeshwa kwa ushiriki wa umma katika kufanya maamuzi juu ya ulinzi na utunzaji wa rasilimali zao kumekuwa kukionyesha ukinzani baina ya watawala na dhana ya utawala bora. Mfano azimio la Bandari, na kuidhinishwa kwa makubaliano ya ubinafsishaji wa bandari kwa DP world bila kusikilizwa na kuchambuliwa kwa kina kwa maoni ya wananchi, kumechora tafsiri halisi ya kupunjwa kwa ushirikishwaji wa wananchi katika kufanya maamuzi.
Picha kutoka PA times
Kukiukwa kwa misingi ya utawala wa Sheria na kuongezeka kwa vitendo vya ufisadi na Rushwa
Yapo matukio tofauti tofauti yanayo dhihirisha ukiukwaji wa utawala wa sheria, ambapo viongozi wameonekana kujiingiza katika matendo yasio randana na sheria za nchi yetu, tunaweza kujikumbusha kupitia zuio la mikutano ya vyama vya siasa lililowekwa kinyume na sheria za vyama vya siasa. Kutofatwa kwa misingi ya utawala wa sheria kumesababisha kuongezeka kwa vitendo vya ufisadi, kwani wanao husishwa na vitendo hivyo wamekuwa wakitoa RUSHWA ili wasiwajibishwe na sheria kutochukua mkondo wake.
Picha kutoka AdobeStock
NAMNA YA KUUENDEA UTATUZI WAKE ILI KUKUZA DHANA YA UTAWALA BORA KWA MANUFAA YA JAMII.
Uchambuzi wa makala hii umelenga kuleta utatuzi juu ya masuala yanayo zorotesha dhana ya utawala bora na kusimamisha nguzo ya utawala wenye tija katika jamii, ili jamii ipate kunufaika.
Kuundwa kwa mifumo ya uwajibishwaji wa viongozi
Mifumo hiyo inaweza kuwa, utunzi wa sheria ya kuwachukulia hatua viongozi wote wa umma wanaohusishwa na ufisadi kutoka katika ripoti ya mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG) kama vile, kifungo cha maisha na kutaifishwa kwa mali za mshitakiwa wa makosa ya ufisadi. Mwaka 2021 ripoti ya CAG ilimtuhumu mkurugenzi mtendaji wa bandari kwa kumhusisha na ufisadi wa fedha za umma bilioni 3.7 na kuishiwa kusimamishwa kazi tu.
Picha kutoka Daily News
Mabadiliko katika mitaala ya elimu, yenye kulenga kuwajenga vijana kuwa WAZALENDO
Vijana ndio nguzo na muelekeo wa leo na kesho ya taifa lolote duniani, taasisi za kielimu zinapaswa kuwalea vijana katika makuzi ya kizalendo, kuwafanya vijana kuwa viziwi wa kutosikia sauti zenye maudhui ya kupewa RUSHWA, vipofu wasioona ubora katika kujibinafsisha na kujilimbikizia mali za umma, viwete wasio weza kuuendea ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma, mbadala wake, wawe wakali pale rasilimali zao zinapoguswa na walowezi. Vilevile, taasisi za elimu ziweke somo la sheria kuwa la lazima, kwa lengo la kuwaandaa vijana kuwa weledi katika kuzielewa vyema sheria za nchi yao, hii itasaidia katika kudumisha ulinzi wa rasilimali na kuhuisha utawala wa sheria.
Picha kutoka UNICEF
Matumizi ya sanaa katika kuchochea utawala bora
Mtawala mwenye maono ya kulifikisha taifa au taasisi katika nchi ya ahadi, iliyo na miti ya mitende, mito ya maziwa na harufu ya Haluwa, anapaswa kufanya uwekezaji mkubwa katika sanaa, kuwaondolea vikwazo vyote kwa wasanii wenye roho ya ujasiri wa kudadavua athari za uwajibikaji mbovu wa viongozi wa umma na kukosoa vikali vitendo vya RUSHWA na UFISADI kupitia kutanua na kuupigia chepeo UHURU WA KUJIELEZA. Hii itachangia katika kukuza utawala bora.
Picha kutoka East Side Online
Kuundwa kwa mfumo wa kielektroniki unaoupa umma fursa ya kuweka maoni juu ya viwango vya utendaji na uwajibikaji wa viongozi wa umma
Mfumo huu utaweza kuonyesha utendaji wa viongozi kupitia viwango vilivyopendekezwa na umma, kiongozi ambae anaonekana kuwa na viwango vya chini zaidi anapaswa kuondolewa na kubadilisha kuweka mwingine ambae ataendana na kasi ya mahitaji ya wanajamii. Hii itachochea uwajibikaji wa viongozi wa umma.
Picha kutoka Adobe Stock
Mwisho; Ili kudumisha utawala bora mahakama zinapaswa kuwa huru kupitia kupunguza mamlaka ya rais kuteua majaji, mbadala wake iundwe tume ya majaji kwaajili ya kuteua majaji.