KERO Ubovu wa miundombinu ya vyoo Chuo Kikuu cha Dodoma Ndaki ya Sayansi ya Kompyuta na Elimu Angavu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mwanafunzi wa UDOM college of informatics and virtual education(CIVE).

Hali ya miundombinu ya college hii ni mibovu sana na hatarishi kwa afya hususani vyoo.

College ya CIVE ina jumla ya blocks 6, tatu katika hizo sita ni mbovu kupindukia. Block moja zima unaweza kukuta vyoo(matundu) viwili pekee ndio vinafanya kazi, hivyo vingine vimeziba na havifanyiwi matengenezo, na hata yakifanyika basi wanachokonoa kidogo tu lakini sio kurekebisha mfumo mzima wa maji taka.

Nimeambatanisha sehemu ya picha na video zinazoonesha vyoo vinavyotumika.

Tunawaomba mtupazie sauti kwa mamlaka husika ili kuwepo na uwajibikaji, na pia tuweze kuishi katika mazingira safi na salama.

Screenshot_20240426-091248_1.jpg


Screenshot_20240426-091256_1.jpg

Screenshot_20240426-091307_2.jpg
 
Ni fezea sana chuo kikubwa kama hiki vyoo kujaa makimba, wahusika walifanyie kazi mapema aisee. Kwa mtindo huu wataanza jisaidia vichakani.
 
Siku nimeenda kufanya interview moja katika hiki chuo ndio niligundua kwamba chuo hiki ni cha kata kama kilivyozoeleka midomoni kwa wengi. Imagine kuna mtu anajinadi kuwa hiki ni chup cha kimataifa ila kina vyoo vichafu kuliko vyoo vya baa ya uswahilini.
 
Yaani sehemu ambapo watu wanauelewa mkubwa kuhusu afya lakini ndipo panakuwa na mazingira hatarishi Kwa afya!lakini hii siyo UDOM tu hata udsm.Nakumbuka Kuna miaka ya nyuma palikuwa na vyoo vichafu sana
 
Yaani sehemu ambapo watu wanauelewa mkubwa kuhusu afya lakini ndipo panakuwa na mazingira hatarishi Kwa afya!lakini hii siyo UDOM tu hata udsm.Nakumbuka Kuna miaka ya nyuma palikuwa na vyoo vichafu sana
Acha uongo wee, huwezi kuta Udsm uchafu.
 
si mna umoja wa wanafunzi UDOM

makatibu wa hostel hamna? Matron hamna wapelekeeni haya malalamikp yenu.

Maana ndio viongozi waliokaribu yenu
 
Back
Top Bottom