Ubalozi wa Marekani kufanya mnada wa kuuza vitu nchini

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
4,006
14,070
Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam unapenda kutangaza kuwa itauza mali mbalimbali katika mnada utakaofanyika tarehe 10 Februari 2024, kuanzia saa 3 asubuhi. Mnada huu utaendeshwa na kufanyika UNIVERSAL AUCTION CENTRE, iliyoko karibu na Golden Resort, Lion Street, Sinza, Dar es Salaam (Angalia ramani).

Vitu vyote vitauzwa "kama vilivyo" bila garantii, huku kodi zote na ushuru ukiwa jukumu la mnunuzi. Maegesho ya magari ni machache. Ni watu 200 tu wa mwanzo ndio watakaoruhusiwa kuingia katika mnada, hivyo tunapendekeza ufike mapema. Unaweza kutazama vitu vitakavyouzwa siku ya Alhamisi, tarehe 8 Februari, na Ijumaa, tarehe 9 Februari kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 11 jioni.

======

Mnada mkubwa kwa idhini ya Ubalozi wa Marekani, Uingereza, World Bank, Corus International na Umoja House.

Wiki hii, kwa idhini tuliyopewa tutauza kwa mnada wa hadhara Toyota L/Cruiser Prado (3),Toyota L/Cruiser V8(1), Nissan Patrol(1), Suzuki Grand Vitara(1), Ford Everest(1), Generator 500KVA (3phase),Fridge, Dinning Tables, reception chair,magodoro, Furniture za nyumbani pamoja na vitu vingine vya ofisini.

Mnada utafanyika siku ya Jumamosi tarehe 10.2.24 kuanzia saa 4, Plot 5 "E", Lion Street Sinza jirani na Lion Hotel
 
Minada yao huwa inashangaza sana kwani Kwa jinsi Watanzania tulivyo malimbukeni tunapandishiana bei nadhani hadi wao wanatushangaa.........anyways mara nyingi huwa ni samani,majokofu,majiko,pasi,vyombo.n.k.
Vitu hivi mara nyingi vinakuwa vimetoka kwenye ofisi zao na majumbani kwani wao wana utaratibu wa kubadilisha vitu kila baada ya muda fulani
 
Back
Top Bottom