Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,967
- 25,635
Kwa wale mliopitia habari za barabara ya Dar es salm, Kibiti, Lindi Mtwara hivi karibuni, sasa tunajionea madudu ya kale.
Barabara hii imejengwa chini ya viwango.
Na tukumbuke waziri aliyehusika na barabara hii kwa kupewa misifa mingi isiyo stahili.
Barabara ina katika kila leo kwa mvua ambazo ilistahili kuhimili.
Kiwango cha ujenzi wa barabara hii huwezi kabisa kulinganisha na kiwango cha kwa mfano Iringa-Makambako.
Wakandarasi ni wale wale -wachina.
Serikali ijionee sasa na msimamo wake usioendelevu- ati anapewa kazi-LOWEST BIDDER!
Ujinga huu sasa unasababisha usumbufu kwa maelfu ya wananchi, ukiacha ajali zinazosababisha vifo kutokana na barabara kutokidhi viwango.
Tunavuna tulichopanda kwa misifa isiyostahili.
NB INAHITAJIKA TECHNICAL REVIEW/AUDIT
Sasa hivi kunahitajika kuwepo a Technical Review au Audit ya ujenzi wa barabara hii. Nina uhakika madudu mengi tu yatagundulika.
Pia soma - Mbunge Maimuna: Barabara ya Kibiti-Lindi ina viraka milioni 10 kabla haijakabidhiwa