Tundu Lissu: Tuna Rais Mzanzibari anayeweza kwenda Ngorongoro na kutoa Amri kwa Wanajeshi wafukuze wamasai wote

Heparin

Senior Member
Sep 24, 2021
149
563
"Leo tuna miaka 60 tukiitwa Tanzania, ndiyo maana tuna rais ambaye ni mzanzibari, siyo mtanganyika. Anaweza kwenda ngorongoro akatoa amri kwa wanajeshi hawa, akasema fukuza wamasai wote ngorongoro wapeleke Msomera Handeni, 547Km kutoka ngorongoro."

"Huyu rais Mzanzibari siyo Mtanganyika, hajazaliwa upande huu, miaka 60, huyu mzanzibari anaweza kutoka alikotoka akaja kuvuruga watu huku. Kusingekuwa na huo muungano asingefanya hivyo kwasababu asingekuwa rais wetu"

"Na siyo ngorongoro tu, sasa wanasema Longido yote, Monduli ya mbugani yote, ule upande wa kwenda Siha nyuma ya mlima Meru yote ile, Simanjiro yote mpaka huku minjingu na maeneo mengine ya wafugaji yote. Wanasema hivi, na haya maeneo wanapanga kuyafanya kuwa mapori tengefu na wakiyatenga kuwa maeneo tengefu maana yake wamasai wanafukuzwa kote"

"Mimi nimetembea nchi hii mwaka jana, kila mahali ni kilio cha ardhi, nchi hii kuna kilio kikubwa cha Ardhi nchi nzima na sababu ni moja, rais anaamuru watu wake mapolisi, DC, wanajeshi wahamishe wananchi"

Pia soma:
 
ila tuache uongo Lissu anajua mengi kuhusu hii nchi
Hao anaoingia nao mikataba ya ardhi ndio hao hao wanaompigania ashike awamu nyingine!!!?

Dola inajua hayo yoote lakini imekaa kimya sijui kwanini!!
He Dola ni wanufaika was haya!!?

Nani mnufaika!!?

Labda kama hizi no juhudi za kuvunja muungano sawa!labda ili tujae upepo watanganyika tuukatae muungano kwasababu ya haya yanayoendelea Zanzibar ipate chake!!

Nasema labda maana sielewi mantiki ya hay kuwepo nchini!!
 
Katiba yetu ina mapungufu mengi sana.Mtanganyika hawezi kuuza ardhi ya Zanzibar yenye ukubwa wa kaburi !.Utashangaa sana Mzanzibar anauwezo wa kuuza ardhi ya Tanganyika yenye ukubwa kuliko nchi yote ya Zanzibar.
 
Au hata ile mbuga ya Serengeti upande wa Tarime kule alikoonekana Mwita Waitara akitembea na Wakurya kabla ya kwenda kumwaga machozi pale Bungeni?
Kwako Waitara.
 
Hao anaoingia nao mikataba ya ardhi ndio hao hao wanaompigania ashike awamu nyingine!!

Dola inajua hayo yoote lakini imekaa kimya sijui kwanini!!
He Dola ni wanufaika was haya!!?

Nani mnufaika!!?

Labda kama hizi no juhudi za kuvunja muungano sawa!labda ili tujae upepo watanganyika tuukatae muungano kwasababu ya haya yanayoendelea Zanzibar ipate chake!!

Nasema labda maana sielewi mantiki ya hay kuwepo nchini!!
Badala ya kuwawezesha watanzania wawekeze kwenye ardhi yao yeye analeta waarabu kuwekeza na kuua hata uwekezaji mdogo waliofanya watanzania
 
Hekima ni pale unapofanya kitu huku ukiepuka athari za maamuzi au jambo unalofanya kwa sasa au baadae.

Nahisi Mbowe ana hekima!
 
Back
Top Bottom