Heparin
Senior Member
- Sep 24, 2021
- 152
- 571
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wa Tanzania, Nape Nnauye amelaani vikali kauli iliyotolewa na Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu kuhusu madai ya Rais Samia kuwaondoa Wamasai wa Ngorongoro kisa yeye ni Mzanzibari.
Waziri Nape amesema kauli hii inapaswa kupingwa na kila mwenye akili timamu kwani ni hoja za watu waliofilisika kisiasa.
"Watanzania tusikubali upuuzi huu, na mimi nitawashangaa watanzania waliozaliwa wakati wa Muungano hata wanaokwenda kumsikiliza mpuuzi huyu, tumkemee, tumtenge, tumlaani" amesema Nape.
Amebainisha ikiwa watanzania wataendelea kuangalia vitendo hivi vya ukosoaji kwa Rais kwa kutumia jinsia, kabila au sehemu anakotoka watakuwa hawaitendei haki nchi.
Ameongeza, "Ni Rais huyu ndiye amesema andamaneni, polisi kawalindeni, na leo walikuwa wanaandamana hapa. Wamelindwa na Polisi, wamesindikizwa walipoenda, wamesababisha foleni dodoma hapa, magari yamesimamishwa ili wao waandamane, kwa uungwana wa huyu mama anayemtukana"

Pia soma: