Tumegundua ushirikina/nguvu za giza unaofanywa na kijana kwenye biashara

Mowwo

JF-Expert Member
Aug 15, 2015
345
266
Wasalaam
Wiki hii mwanzoni baada ya kutoka kwenye mizunguko ya kusaka tonge, niliongea na ndugu yangu mfanyabiashara nikaomba wakati anafunga hesabu nifike kujifunza mambo mawili matatu.

Ilikuwa mida ya saa 2 usiku Baada ya kufika ilipo biashara tulisalimiana vizuri tu na kijana anaepiga kazi pale. Baada ya kucheki mahesabu ambayo ndugu yangu anafanya kila akifika, tukagundua kuna upotevu wa pesa lakini sii pesa nyingi(Tsh2500).

Baada ya kumuuliza kama alitumia, yeye hakuwa na majibu imekuaje haionekani. Baada ya kucheki stock tukaona kuna bidhaa zimeisha inabidi mzigo ununuliwe mwingine, akaandika lists.

Ghafla muda amekaa kuandika list ya vitu vya kununua akaona kuna unyoya kama wa jogoo ule mkubwa umebanwa kwa kificho na gundi(solotape) kwenye droo analotunzia cash. Ikabidi tuhoji kwanini ameweka hapo, lakini bahati mbaya hakutupa majibu alisema atamwambia ndugu yangu maana yake kwa siku nyingine.

Muda huo huo mteja alikuja kununua kitu, pesa ilivyowekwa kwenye droo(alivuta droo) tukashangaa kuna kitu cha mviringo cheusi na muda tumekiona akakiwahi na kukishkilia mkononi. Kumuuliza kwanini kuna hivyo vitu jibu lake ni moja atamwambia ndugu yangu maana ya hivyo vitu siku nyingine.

Tuliondoka pale bila majibu sahihi, lakini ndugu yangu licha ya kukasirika anashauri kwasababu anapiga kazi vizuri na amepiga hiyo kazi muda mrefu atamvumilia huku akimfuatilia kwa karibu zaidi(mpaka sasa anapiga kazi).

Vipi maoni yako kwa hayo matukio? Kama faida unaipata, utamfukuza kazi? Una uzoefu wowote katika hili?

Ungemshauri nini kama ni ndugu yako? Wenye biashara halafu mmeajiri chukua tahadhari.

NB: Biashara ni ya vinywaji na uwakala
 
Sasa hapo kuna shida gani? Mimi kama kazi inafanyika na hakuna hasara kama ulivyosema hayo mengine sio shida zangu.

Halafu ulitakiwa kujiongeza kwanini dogo anasema ataongea na boss wake, pengine ni mpango kazi wao huo wewe unaleta ujuaji.
 
Wasalaam
Wiki hii mwanzoni baada ya kutoka kwenye mizunguko ya kusaka tonge, niliongea na ndugu yangu mfanyabiashara nikaomba wakati anafunga hesabu nifike kujifunza mambo mawili matatu.

Ilikuwa mida ya saa 2 usiku Baada ya kufika ilipo biashara tulisalimiana vizuri tu na kijana anaepiga kazi pale. Baada ya kucheki mahesabu ambayo ndugu yangu anafanya kila akifika, tukagundua kuna upotevu wa pesa lakini sii pesa nyingi(Tsh2500).

Baada ya kumuuliza kama alitumia, yeye hakuwa na majibu imekuaje haionekani. Baada ya kucheki stock tukaona kuna bidhaa zimeisha inabidi mzigo ununuliwe mwingine, akaandika lists.

Ghafla muda amekaa kuandika list ya vitu vya kununua akaona kuna unyoya kama wa jogoo ule mkubwa umebanwa kwa kificho na gundi(solotape) kwenye droo analotunzia cash. Ikabidi tuhoji kwanini ameweka hapo, lakini bahati mbaya hakutupa majibu alisema atamwambia ndugu yangu maana yake kwa siku nyingine.

Muda huo huo mteja alikuja kununua kitu, pesa ilivyowekwa kwenye droo(alivuta droo) tukashangaa kuna kitu cha mviringo cheusi na muda tumekiona akakiwahi na kukishkilia mkononi. Kumuuliza kwanini kuna hivyo vitu jibu lake ni moja atamwambia ndugu yangu maana ya hivyo vitu siku nyingine.

Tuliondoka pale bila majibu sahihi, lakini ndugu yangu licha ya kukasirika anashauri kwasababu anapiga kazi vizuri na amepiga hiyo kazi muda mrefu atamvumilia huku akimfuatilia kwa karibu zaidi(mpaka sasa anapiga kazi).

Vipi maoni yako kwa hayo matukio? Kama faida unaipata, utamfukuza kazi? Una uzoefu wowote katika hili?

Ungemshauri nini kama ni ndugu yako? Wenye biashara halafu mmeajiri chukua tahadhari.

NB: Biashara ni ya vinywaji na uwakala
Uchawi, uganga, ushirikina Ni Imani Ni kama vile ukimuona NG'OMBE JUU YA MTI LAZIMA KAPANDISHWA..

uchawi uganga ushirikina is just MYTHOLOGY
 
Back
Top Bottom