Jiajiri kabla ya kuajiriwa! Kijana huna nafasi ya kukaa kijiweni kisha kuilaumu Serikali haijakupa ajira

Abuu shaukan

New Member
May 2, 2024
2
1
KIJANA HUNA NAFASI YA KUKAA KIJIWENI KISHA KULAUMU SERIKALI HAIJAKUPA AJIRA.

Leo ukifatilia tabia za vijana walio wengi, ni kushinda kijiweni kujadili wanawake, kuvuta bangi na sigara, madawa ya kulevya, ukabaji, matokeo yake ni magonjwa ya Zinaa, uteja na mauwaji.

Lakini madai Yao makubwa kazi hakuna.

Jeee kama AJIRA hamna Serikalini Ndio tufanye upuuzi huu?

Vijana wengi, wengi hatupendi kujituma na kujiajiri wenyewe na hatusukumi akili zile Kwa kufikiria baadae!!!

Kama sikosei mara mwisho bangi niliona ikiuzwa 350 hapo imetimia nadhani kwasasa imesogea kidogo, sigara 200 mpaka 300 Kwa siku bangi 5 na sigara tano zinaenda kwenye mapafu yako Kwa mwaka umevuta bangi na sigara 3,600 Tsh 990,000 umezitumia kuharibu mwili wako.

Hapo bado hujanunua konyagi, banana na Aina nyingine za pombe Kali pamoja na vidonge vya valium Kwa mwaka kijana wa kimasikini asiye na kazi hutumia wastani wa milioni 2 kuharibu mwili wake njee ya Kula yake.

Kumbe ule muda wa kukosa AJIRA Serikalini tungeliweza kujipanga na kujiandaa ili ukipita muda fulani tuweze kujiajiri wenyewe, Kwa kujiwekeza kidogo kidogo baada ya kupunguza gharama Fulani kwenye maisha yetu ya starehe, DUNIA YA LEO YA KIAFIRIKA INAKUTAKA WEWE UJIJARI KWANZA NDIO WAZAZI NDUGU NA MARAFIKI WAKUUNGE MKONO.

Faida ya kujiajiri

Kujiajiri hakukubani wewe kufanya vitu vingine, ukijiajiri unajigawanya Kwa kiasi ambacho utaweza kuwa na vyanzo vingi vya mapito.

Na ziko AJIRA ambazo MTU anaweza akaziingia ili kulaumu kwake kuwa AJIRA hakuna kuishe.
Kwa sababu haipo serikali itakayoajiri watu wote.

Amini hivyo Kwanza.
Upo uswazi (uswahilini ni sehemu yenye maisha ya kiwango kidogo na kumejaa tabia zote za hovyo uswazi) Unashinda kijiweni kwanini hapo kijiweni kwako usiweke meza ukauza sumu zinazouwa wadudu warukao na watambaao ambao ni tishio katika jamii ya uswazi.
Ukaweka UDI wa mbu NK.

Na hili NI dogo ila 350 utaipata aidha ununie bangi au uitunze baada ya mwaka 1 utafute kubwa.

Na kijiajira hiki vijana baadhi wamekistukia wanaweka meza zao sehemu ambazo wapita Kwa mguu NI wengi na wamejikuta wakufanya biashara vizuri.

Tanzania tuna utajiri wa Ardhi yenye rutuba, Kwa kiasi ambacho kijana anaweza kujiajiri Kwa kuitumia Ardhi hiyo Kwa kilimo cha mboga mboga.

Mboga za majani NI mboga zinazoliwa Sana na watu wa Aina zote kwani usiboreshe zaidi Kwa kuzingatia usafi, umwagiliaji WA dawa ulio salama.

Ni kilimo ambacho hakili muda wako asubuhi utaenda SAA 5 utarudi maskani kuulizia mishe nyingine.

Kwanini usijiajiri Kwa kufanya biashara za ukopeshaji, biashara ambazo Kwa Aina ya ufanyaji wake kila siku unaweza kuleta bidhaa mpya, na biashara hii imekuwa inawasaidia wafanya biashara wadogowadogo na hata jamii zetu za Kiswahili zimenufaika na biashara hii, Kwa sababu mara nyingi watu kila baada ya muda fulani wanahitajia vitu Fulani ambavyo wanaweza kuvipata kulipia kidogo kidogo.

Kujiajiri kwenye ufugaji wa kisasa

Hii ni sekta muhimu katika jamii kwani ufugaji umekuwa niweje matokeo makubwa kwenye uchumi wa wafanya biashara.

Ufugaji wa kisasa hauhitaji eneo kubwa, ni vile tuu utaweza kujipanga na kupangilia mabanda Kwa ghorofa, Kwa kiasi ambacho sehemu ndogo unafuga kuku 100, na Anza kujiwekeza kidogo kidogo kwenye ufugaji kuku 5 ambao jogoo 1 na matetea 4 Kwa mwaka ukiwa makini na kuacha uroho unakusanya kuku zaidi ya 100, maana yake Kwa mwaka unaofatia utakusanya kuku kufikia 1000 au zaidi.

Maisha ni mahesabu.

Kujiajiri kwenye uvuvi.
Samaki ni maliasili pendwa, ni chakula kitamu kinacholiwa na watu wote isipokuwa wagonjwa.

Kwa jamii zetu za pwani inakuhitajia wewe kujiunga na kundi Fulani ambapo ndani yake utajifunza uvuvi Kwa muda mchache na utajipatia kipato chako halali.

Uzuri wa kujiajiri Una nafasi ya kuendelea kutafuta wanunuzi wa biashara yako hata Kwa njia ya kutumia mitandao ya kijamii.

Biashara ambazo unaweza kufanya ziko nyingi Mimi nimekutajia baadhi.

Kwanini ulaumu serikali wakati unavuta bangi?

Kwanini usiilaumu wakati ilipokuzuia kujiajiri?

VIJANA BADO TUNA NAFASI YA KUSOGEA MBELE.

Lau tukiwa makini na kujua familia tulizotokea tunaweza tukawa sababu ya ukombozi.
 
Umenena vyema ila ningeomba siku ingine usituponde watumiaji wa mjani. Kwa kuongeza ukombozi wa kifikra unahitajika katika kubadili mitazamo ya sisi vijana tulio wengi na kujikita kutazamia fursa zilizopo nchini mwetu na kwenye nchi za wengine.

Fursa zilizopo mkoa wa morogoro; kilimo cha ufuta, mbaazi, alizeti, choroko, maharage, kunde, mahindi, miwa, bamia, nyanya chungu, mahindi, mihogo na karanga. Mazao niliyoorodhesha kwa mkoa tajwa ni hayana gharama kubwa katika kuyalima mpaka kuvuna hivo kwa sisi wavivu na tusio na mtaji mkubwa (chini ya 300,000) tunaweza kumudu.
 
Dunia ina upungufu wa ajira lakini kazi za kufanya zipo nyingi sana...Dr.Rev.Eliona Kimaro
 
Umenena vyema ila ningeomba siku ingine usituponde watumiaji wa mjani. Kwa kuongeza ukombozi wa kifikra unahitajika katika kubadili mitazamo ya sisi vijana tulio wengi na kujikita kutazamia fursa zilizopo nchini mwetu na kwenye nchi za wengine.

Fursa zilizopo mkoa wa morogoro; kilimo cha ufuta, mbaazi, alizeti, choroko, maharage, kunde, mahindi, miwa, bamia, nyanya chungu, mahindi, mihogo na karanga. Mazao niliyoorodhesha kwa mkoa tajwa ni hayana gharama kubwa katika kuyalima mpaka kuvuna hivo kwa sisi wavivu na tusio na mtaji mkubwa (chini ya 300,000) tunaweza kumudu.
Basi broo asanteh Kwa kunielewa
 
Back
Top Bottom