SoC04 Tulinde mazingira ili kuweka chachu ya maendeleo

Tanzania Tuitakayo competition threads

cli

New Member
Apr 25, 2024
2
3
Maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa sasa yamekua yakiongezeka kwa kasi siku baada ya siku. Ikiwa yote hayo yanahitaji mazingira pamoja na rasilimali zilizopo katika mazingira husika, uhusiano mkubwa uliopo baina ya maendeleo kwa ujumla na mazingira ni mkubwa sana kiasi kwamba ni lazima tuweze kuyalinda na kuyaweka katika hali ambayo mahusiano haya hayatapelekea matokea hasi kwa viumbe wote waliopo katika mazingira.

Baadhi ya matokeo hasi yanayoweza kutokea ikiwa maendeleo hayatazingatia usalama wa mazingira;

1. Ongezeko kubwa la joto; ongezeko hili la joto linasababishwa kwa ukaribu zaidi na shughuri za kibinadam haswa katika maendeleo ya viwanda.

2. Ongezeko la majanga kama vile mafuriko na ukame; majanga haya pia yanasabishwa na baadhi ya shughuli za kibinadam zisizozingatia utunzaji wa mazingira kama ukataji ovyo wa miti.

3. Kupungua kwa kiwango cha hewa ya oxygen;kwa upana zaidi kunauwezekano mkubwa wa Kupungua kwa kiwango cha oxygen hali inayosababishwa na uchafuzi na matumizi yasiyo zingatia usalama wa mazingira.

HIVYO BASI, Kwa kuyazingatia matokeo hasi yatokanayo na maendeleo yasiyo zingatia usalama wa mazingira. Ikiwa pia nchi yetu TANZANIA ipo katika jitihada za kuongeza maendeleo yake kwa kasi,hali ambayo kama uzembe utajitokeza katika namna za kuyalinda mazingira basi huenda ikapelekea kilio kikubwa sana katika mazingira pamoja na vilivyomo katika mazingira husika.Na kwa kutambua hayo tunahitaji kuyafanya yafuatayo kuelekea TANZANIA ya miaka 25 ijayo yenye maendeleo makubwa na mazingira salama na bora.

Kuhakikisha matumizi ya nishati mbadala yanapewa Kipaumbele; kuelekea TANZANIA ya hadi miaka 25 itakayo kua na maendeleo makubwa katika mazingira bora kuna haja ya kuhama na kuachana kabisa na matumizi ya nishati zisizo mbadala kama kuni na mkaa kwani hizi zibapelekea uharibifu mkubwa sana wa misitu hasa katika mazingira ya vijijini,ili tuweze kuyafikia maendeleo makubwa na mazingira bora angalau tunahitaji kufanikiwa katika matumizi ya nishati mbadala kwa zaidi ya asilimia 90 kwa maeneo yote.hivyo uhakika na upatikanaji wa nishati mbadala hasa katika mazingira ya vijijini itatuweka katika hali nzuri kuyafikia maendeleo makubwa katika mazingira bora.

Kuboresha kampeni za utunzaji wa mazingira; ikiwa mazingira hayatakua katika hali ya usalama basi hata maendeleo hayatakua na maana kabisa hivyo basi kabla ya kujikita katika sera kali za kimaendeleo kufikia mwaka 2050 bado kunahaja ya kuziangalia upya na kuongeza mkazo katika sera za mazingira.

Kuongeza maeneo kwaajili ya hifadhi za taifa; pia kuelekea TANZANIA ya tuitakayo kufikia mwaka 2050 bado ipo haja ta kuyatenga maeneo mengine zaidi kwaajili ya kuhakikisha uhifadhi wa mazingira

Kuanzisha project mbadala kwa baadhi ya maeneo yatakayo ongezwa katika hifadhi za taifa,ambapo ukiachana na shughuli za utalii pia tunaweza kua na project nyingine mbadala ili kuhakikisha kua tunayalinda mazingira huku tukizidi kunufaika nayo. Mfano wa project ni kuanzishwa kwa michezo mbalimbalu katika maeneo hayo hivyo tunapaswa kua na hifadhi za taifa katika aina mbalimbali kutokana na matumizi ambayo yatakua katika uangalizi mkubwa.

MWISHO
Kwakuzingatia kua hakuna maendeleo yatakayofaa ikiwa mazingira yataharibiwa hivyo maendeleo yana husiana mojakwamoja na mazingira hivyo tunapaswa kuwaza kwa upana zaidi juu ya mazingira kabla ya maendeleo tunayoyahitaji.
 
MWISHO
Kwakuzingatia kua hakuna maendeleo yatakayofaa ikiwa mazingira yataharibiwa hivyo maendeleo yana husiana mojakwamoja na mazingira hivyo tunapaswa kuwaza kwa upana zaidi juu ya mazingira kabla ya maendeleo tunayoyahitaji.
Nakubali kuwekeza katika teknolojia zilizo na athari kidogo kwa mazingira lakini sio kwa gharama ya kuikosa teknolojia ati kisa mazingira tu. Kimahesabu Tanzania ipo na uchache katika uchafuzi wa mazingira yaani tunayo mapori mengi kuliko uchafuzi.

Na hili linanileta kwenye pointi ya kuongeza maeneo ya hifadhi. Mmmmh, labda kama kutakuwa na kitu cha kipekee ndio eneo liwekwe kuwa tengefu. Ahsante
 
  • Thanks
Reactions: cli
Back
Top Bottom