TMA: Kimbunga “HIDAYA” kipo umbali wa Kilomita 120+ kutoka Pwani ya Dar es Salaam

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,327
5,510
WhatsApp Image 2024-05-04 at 08.42.37_2e797699.jpg

Dar es Salaam, 04 Mei 2024 saa 12:00 Asubuhi:​

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa ya mwenendo wa kimbunga “HIDAYA” kilichopo karibu na maeneo ya pwani ya nchi yetu.

Hadi kufikia saa 9 usiku wa kuamkia leo, Kimbunga “HIDAYA” kilikuwa katika eneo la bahari takriban kilomita 125 kutoka pwani ya Kilwa (Mkoa wa Lindi), kilomita 93 kutoka Pwani ya Mafia na kilomita 128 kutoka pwani ya Dar es Salaam kikiwa na mgandamizo wa hewa wa kiasi cha 985 hPa na kasi ya upepo unaofika kilomita 120 kwa saa.

Uwepo wa kimbunga “HIDAYA” karibu kabisa na pwani ya nchi yetu umeendelea kutawala mifumo ya hali ya hewa katika maeneo hayo, ambapo katika kipindi cha masaa 6 yaliyopita, vipindi vya mvua kubwa na upepo mkali vimeendelea kujitokeza. Mfano katika vituo vya hali ya hewa vya Mtwara, Kilwa, Zanzibar na Dar es Salaam upepo mkali unaozidi kilomita 50 kwa saa umeweza kupimwa katika nyakati tofauti kuanzia usiku wa kuamkia leo hadi asubuhi hii. Vile vile katika kipindi hicho, vipindi vya mvua kubwa vimeendelea kushuduhiwa katika maeneo ya Mtwara na Lindi ambapo hadi kufikia saa 9 usiku kituo cha Mtwara kiliripoti jumla ya milimita 75.5 za mvua ndani ya masaa 12.

Kiwango hiki cha mvua ndani ya masaa 12 ni kikubwa sana ukizingatia kuwa wastani wa mvua kwa mwezi Mei kwa kituo cha Mtwara ni milimita 54 tu. Hivyo kiasi cha mvua kilichonyesha ndani ya masaa 12 katika kituo cha Mtwara ni takribani asilimia 140 ya wastani wa mvua kwa mwezi Mei kwa kituo cha Mtwara.

Aidha, kimbunga “HIDAYA” kinatarajiwa kuendelea kusogea karibu zaidi na ukanda wa pwani ya nchi yetu huku kikipungua nguvu yake taratibu kuelekea usiku wa kuamkia Jumapili tarehe 05 Mei 2024.

Katika kipindi hiki, kimbunga “HIDAYA” kinatarajiwa kuendelea kusababisha matukio ya vipindi vya mvua kubwa na upepo mkali katika maeneo ya ukanda wa pwani hususan mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Dar es salaam pamoja na kisiwa cha Unguja na maeneo ya jirani. Vilevile, matukio ya mawimbi makubwa baharini yanatarajiwa kuendelea kujitokeza katika ukanda wote wa mwambao wa pwani ya Bahari ya Hindi.

USHAURI: Wananchi katika maeneo tajwa na wote wanaojihusisha na shughuli mbalimbali baharini wanashauriwa kuchukua tahadhari kubwa na pia kuendelea kufuatilia na kuzingatia taarifa za utabiri na tahadhari kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania pamoja na kupata ushauri na miongozo ya wataalam katika sekta husika ili kujikinga na athari zinazoweza kujitokeza.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga “HIDAYA” na athari zake kwa mifumo ya hali ya hewa hapa nchini na itaendelea kutoa taarifa kila baada ya masaa matatu, na mara kwa mara kila inapobidi.

Imetolewa na:
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.


================

Dar es Salaam, 03rd May 2024 at 3:00 pm:

The Tanzania Meteorological Authority (TMA) is continuing to issue updates on the development of the Tropical Cyclone “HIDAYA” currently over the Indian Ocean, east of the Mtwara coast. The Tropical Cyclone “HIDAYA” has continued to strengthen (deepening) and moving west-ward close to our coast, and currently at approximately 342 kilometers east of the Mtwara coast, with a maximum wind speed of 140km/hr.

The analysis of weather systems over the ocean shows a probability of Tropical Cyclone "HIDAYA" to slightly decrease in strength in the next 12 hours as it continues to move very close towards the coast of Tanzania. This cyclone is expected to continue until 05 May 2024 and weaken (fill up) after 05 May 2024.

The presence of Tropical Cyclone "HIDAYA" near the coast of our country is expected to dominate and affect the weather patterns, causing periods of heavy rains and strong winds in some areas of Mtwara, Lindi, Pwani regions (including the islands of Mafia), Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, the islands of Unguja and Pemba, and the surrounding areas.

Periods of rains and strong winds exceeding 40 km/hr, have been observed in some parts of Lindi and Mtwara regions consistently until 3 pm this afternoon. Even though, the Tropical Cyclone "HIDAYA" shows some slight weakening trend, clouds within the spiral bands are expected to trigger heavy rains and strong winds in some areas along the coastal belt on 4th to 5th May 2024.

ADVICE: The public, particularly in the named areas and those involved in marine activities over the Indian Ocean are advised to take maximum precautions, and continue to make follow-ups of latest weather forecasts and updates from Tanzania Meteorological Authority as well as to seek advice and guidance from experts in the relevant sectors to minimize potential impacts.

The Tanzania Meteorological Authority continues to monitor the development of Tropical Cyclone “HIDAYA” and its associated impacts and will provide forecast updates after every three hours, and whenever necessary and as appropriate.
Issued by: Tanzania Meteorological Authority.
 
Back
Top Bottom