JamiiForums
JF Official Account
- Nov 9, 2006
- 6,202
- 5,029
Mada hili inahusu matatizo ya Miguu kuwaka moto na namna ya kukabiliana nayo.
Maswali...
Nimekuwa na tatizo la miguu yote miwili kuwaka moto sana, hata kutembea nashindwa kukanyaga chini vizuri.
Nina umri wa miaka 38 na uzito wa 98Kg.Sijaugua ugonjwa mwingine zaidi ya malaria ya kawaida kwa mwaka mara mbili au moja.
Kwa ufupi sina mazoezi yoyote ya viungo nifanyayo.Sasa natembelea fimbo kama mlemavu.
WanaJF, Niangalizieni hili na kama kuna mtaalamu wa viungo humu basi anipe ushauri ni mazoezi gani nifanye kupunguza uzito.
Ushauri, Kinga na Tiba...
Mrejesho/Ushuhuda
Maswali...
Nimekuwa na tatizo la miguu yote miwili kuwaka moto sana, hata kutembea nashindwa kukanyaga chini vizuri.
Nina umri wa miaka 38 na uzito wa 98Kg.Sijaugua ugonjwa mwingine zaidi ya malaria ya kawaida kwa mwaka mara mbili au moja.
Kwa ufupi sina mazoezi yoyote ya viungo nifanyayo.Sasa natembelea fimbo kama mlemavu.
WanaJF, Niangalizieni hili na kama kuna mtaalamu wa viungo humu basi anipe ushauri ni mazoezi gani nifanye kupunguza uzito.
Mi nina tatizo la miguu kuchemka,yaani nahisi kama nyayo zimelowekwa motoni naomba ushauri tafadhari, pia nina tatizo la kuhisi kama nina baridi kali upande mmoja wa mwili wangu(wa kulia).
Nahisi kama ninakuwa na baridi kali hadi mkono wote wa kulia unakuwa kama umechoka na kulegea.
Msaada please
Habari.
Ndugu wana Jf, kwa takribani zaidi ya mwaka sasa, ninasumbuliwa na tatizo la nyayo za miguu kuwaka moto.
Wakati inaanza nilijua tatizo ni aina ya viatu ninavyo tumia, nikabadirisha na tatizo likabaki pale pale.
Nikaamua kwenda hospitali mara kadhaa bado tatizo halija ondoka,(dawa nilizo tumia, ni multvitamin, neurobine, na neuro support. na siku hizi, nyayo zina uma mda wowote tofauti na mwanzoni ambapo nyayo zilikuwa zinauma wakati wa usiku pekee.
Pia, nyayo zikiuma nnakuwa najisikia hali ya kuchoka sana, na kukosa nguvu.
Hospitali nilizo enda ni za serikali, moja ya wilaya na nyingine ni ya mkoa.
Sasa nnawaomba ndugu zangu, msaada wa mawazo wa jisni ya kupata ufumbuzi wa tatizo langu, eidha kwa kunielekeza hospitali ambayo nnaweza kwenda kupata matibabu kwa gharama yeyote ile nipo tayari.
Na kama kuna mtu aliwahi kupata hili tatizo, na likatatuliwa nnaomba unishirikishe na mimi nipate kupona maana nnateseka.
Asanteni.
Ushauri, Kinga na Tiba...
Pole sana kwa matatizo yako,niseme machache kutokana na uelewa wangu tu kuhusu tatizo lako ingawa mie sio daktari ila waweza kuchukua haya na kufanya vipimo.
Miguu kuwaka moto yaweza kuwa ni ugonjwa unaitwa peripheral neuropathy au nerve zako ambazo zinatoka kwenye uti wa mgongo kubanwa(pinched nerves)
Peripheral neuropathy husababishwa mostly na ugonjwa kama kisukari pamoja na aids,ingawa wataalam wanasema hata bakteria wengine pia huweza kusababisha.
Kama ni peripheral neuropathy hiyo kuwaka moto itaendelea mpaka mikononi in a course of time,while pinched nerve ikiwa serious huweza kusababisha uka-paralize.
Ushauri: Nenda kacheck kisukari,hiv infections,x-ray ya mgongo/MRI mara moja.Pia kuna mazoezi waweza kufanya yakakusaidia.Check na diet punguza carbohydrate,acha kabisa sigara na pombe kama unatumia,na lastly jaribu kusali sana kwani hata mambo ya ushirikina pia yapo
TATIZO LA MIGUU KUWAKA MOTO MIGUU
Katika mwili wa binadamu, kuna tatizo la kiafya ambalo huambatana na dalili za mtu kuhisi maumivu, kuhisi kuwaka moto na kufa ganzi kwa viungo vya pembezoni mwa mwili
yaani miguu na mikono. Tatizo hili kitaalamu hujulikana kwa jina la Peripheral Neuropathy.
Matatizo haya ya kiafya (miguu/mikono kuhisi ganzi, baridi au maumivu) husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili (miguuni au mikononi) na
hivyo kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika sehemu husika, miguuni au mikononi.
Dalili zinazoambatana na ugonjwa huu ni hizi zifuatazo
1.Mtu kuhisi ganzi
2. kushindwa kushika au kunyanyua kitu, kuchoka kwa misuli na kadhalika.
3.maumivu au kuwaka moto maeneo ya miguuni/mikononi,
Miongoni mwa mambo ambayo hupelekea neva hizi za pembezoni kudhoofika na kushindwa kufanya kazi vizuri ni haya yafuatayo:
1.Kupungua kwa virutubisho mwilini,hasa mkusanyiko wa vitamini B, (Vitamin B Complex).
2.Matumizi ya dawa, mfano dawa za kutibu kifua kikuu au za kupambana na virusi vya ukimwi
3.Uzito mkubwa wa mwili,
4.Ugonjwa wa kisukari,(diabetic polyneuropathy).
5.Shinikizo la damu,
Nina kuuliza Swali je una uzito wa mwili kilo ngapi? Una miaka mingapi? umeowa au umeolewa?
Unao ugonjwa wa kisukari? unao ugonjwa wa Maradhi ya Presha? Kapime huenda una Ukosefu wa Kupungua kwa virutubisho Mwilini? Ukipata majibu wasiliana na mimi kwa Private messege
Magonjwa haya ni upungufu wa vitamini B complex kuwa na matatizo ya kisukari,ulevi,uvivu wa mazoezi,kukaa eneo moja muda mrefu na nk.
Njia za kuepuka ugonjwa huu
- Kufanya mazoezi ya kukimbia na kunyosha miguu
- Usafi wa viatu na sox
Kama umeupata tumia njia hizi utapona kabisa
- Tumbukiza miguu kwenye maji ya uvuguvugu na ikiwemo chumvi kiasi na baada ya hapo paka limao maeneo yote yalio asilika
- Tumia sana vitunguu swaumu kuwa mda wa wiki moja tatizo litakuwa limekwisha.
Na pia kuna dawa ya vidonda vya tumbo ambayo huponya na kuviondoa kabisa na iyo daqa ina faida nyingi sana kam vile
- Kutibu kisukari
- Matatizo ya mgongo
- Nguvu za kiume
- Matatizo ya figo
- Matatizo ya moyo
Na mengine mengi san na pia natoa ushauli bure bila malipo yoyote kulingana na ugonjwa
waweza kunipigia kwenye namba 0752093410 au 0685299621.
Na dawa yangu ninaiuza kwa bei ndogo kuanzia 35000 tu kama uko mbali nitakutumia
MUNGU NA AKUBALIKI.
Asante kwa kusoma makala hii.
Mrejesho/Ushuhuda
Wakuu natumai mu wazima kwa kudra za muumba. Siku chache zilizopita niliweka Uzi hapa jukwaani, nikiomba msaada wa ushauri ili tatizo langu la miguu kuwaka moto nipate namna ya kulitatua kwani ilikuwa ni miezi miwili imepita nikiwa na tatizo hilo na nisingeweza kuvaa viatu kutokana na maumivu niliyokuwa nayo.
Msaada wa mawazo: Miguu inawaka moto
Nashukuru wanajukwaa mlinipa ushauri wa kila aina na niliufanyia kazi na sasa nimerudi kuwashukuru wanajukwaa wote kwa moyo uliojaa upendo kwa kuguswa na hali niliyokuwa nayo. Sasa tatizo nililokuwa nalo limeisha na viatu ninavaa na chuoni ninaenda bila tatizo.
Mungu aibariki JF na Wanajukwaa wote. Upendo wa namna hii udumu milele na milele.
Asanteni sana.
#Mavindozii.