SoC04 Tanzania yenye Utawala Bora na Adilifu

Tanzania Tuitakayo competition threads

NYANOHA

Member
Sep 2, 2022
5
3
Kabla ya yote, nachukua nafasi hii kumshukuru allah (sw) kwa kunijaalia uzima wa afya na uhai pia kuniwezesha kushiriki katika shindano hili la kuandika andiko la kutoa mawazo ya kibunifu kuhusu Tanzania tuitakayo yanayoweza kutekelezeka ndani ya Miaka 5 hadi 25 ijayo. Nmemeandaa mawazo kadhaa na naimani mawazo haya yanaweza kutekelezeka na yataleta mapindinduzi makubwa chanya katika maendeleo ya nchi yetu ya Tanzania. mawzo haya yamejikita zaid katika kuipata Tanzania yenye utawala bora, adilifu, na weyenye kujali wanachi.

Tanzania hii tutaipata kwa kufanya yafuatayo.

  • Katiba mpya. Kwa kua tunahitaji tanzaia yenye utawala bora na adilifu, basi katiba iliyopo haitufai hata kidigo, kwani katiba hii inawapendelea sana na kuwalinda viongozi, inawakandamiza na kuwanyanyasa raia, hivyo basi tunahitaji katiba mpya ambayo itatoa haki sawa kwa watu wote bila ya kuangalia cheo au nafasi ya mtu. tunahitaj katiba ambayo itakua ni sababu ya kila mutumishi wa serikali kufanya kazi kwa bidii na kuwajibika kikamilifu katika kukamilisha majukumu yake ya kila siku kwa kuanzia kuchunga na kujali muda wa kuingia na kutoka kazini hadi kutoa huduma bora kwa raia. Pia katiba hii itakua inawajali sana wananchi kwani ndio lengu kuu la kuwepo serikali ni kuwatumikia wananchi na sio kuwanyanyasa na kuwadhulumu mali zao.
  • Jeshi huru. Kwa kua tunahitaji Tanzania yenye utawala bora na adilifu, basi pia tunalazimika kupata jeshi huru, jeshi ambalo litafanya shughuli zake bila ya kuingiliwa na viongozi waliopo madarakani na liwe na uwezo wa kuwachukulia hatua viongozi watakao enda kinyume na sheria, kwani jeshi letu tulilonalo sasa lipo kwa ajili ya viongozi waliopo madarakani sio kwa jili ya wananchi, ndio mana kila kona raia wanapigwa, wananyanyaswa, wanaporwa mali zao na jeshi, jeshi hili lililotakiwa kuwalinda leo ndio lina waadhibu kutokana na kupokea maagizo na kutii amri za viongozi waliopo mdarakani.
  • Tume huru. Chaguzi zote zilizopita sio huru na haki, kwani tumeshuhudia matukio mabalimbali yasio ya kibinaadam katika vtuo vya kupiga kura, kama vile watu kupigwa hususani wapinzani au kutolewa nje kwa nguvu ya kijeshi mawakala wa kuhesbu kura wa vyama vya upinzani wakati wa kuhesabu kura. Hii ni ishara kua uchaguzi sio wa haki kwani tume itakua imepokea maagizo kutoka uongozi mkuu. Kwa nini tume iingiliwe kupangiwa cha kufanya katika shughuli zake na ishindwe kujisimamia yenyewe, kwa hiyo tunahitaji kua na tume huru itakayoweza kuendesha shughuli zake zote bila kuingiliwa wala kuagizwa na uongozi mkuu.
  • Bunge huru. Bunge ni muhimili mkuu wa serikali hivo sio jambo jema kuona bunge letu hailina uhuru wa kundesha shughuli zake katika kutekeleza majukumu yake kisheria kwani wakuu wanchi wamelitawala bunge kuanzia kwa spika had wajumbe wa bunge, sote tumekua tukiona spika wa bunge baazi ya wakati akiwanyamazisha wabunge wanaosema ukweli bungeni au kuna baazi ya wabunge wamekua wakisema vitu visivyo na tija kwa wananchi na nchi kiujumla kwa kuhawahofia wakuu wa wanchi na muda mwengine kuishia kuwasifia tu wakuu wanchi na kuna baazi ya wabunge hawaongei kitu chochote mwanzo hadi mwisho wa bunge wao wanaishia kugonga meza tu. Hawa hawafai kuwepo bungeni. Hili halikubaliki tunahitaji kua na bunge lenye uhuru wa kufanya shughuli zake kisheria bila kuogopa wala kuingiliwa na wakuu wa nchi ili tufike kule tunakokutaka.
  • Baraza huru la Mawaziri. Tunahitaji kua baraza huru la mawaziri, mfumo wa sasa wa upatikanji wa baraza hili ndio sababu ya kwa nini baraza hili sio huru, raisi ndie anaechagua mawaziri baada ya kuapishwa, hivo mawaziri wote anawachagua yeye hivo sio ajabu kuona hawa mawaziri wanafanya kazi kutokana na matakwa ya raisi. kwa hiyo ili tuwe na baraza huru basi tunatakiwa tubalishe nyia ya upatikanaji wa mawaziri kutoka kuteuliwa na raisi badala yake tutumie njia ya kuwapigia kura sisi wananchi ili waende kufanya kazi kwa ajili ya wananchi na nchi kwa ujumla na sio kwa ajili ya raisi.
  • Mahakama huru. Mahakama zote hapa nchini zimekua hazitendi haki kwani zimekua ndio sababu ya kupindisha haki kua batili na batili kua haki kwa kungalia nafasi, cheo na utajiri wa mtu. wanachi wamekua wakichukua hatua mkononi juu ya wale wanaovunja sheria huko mitaani kwa kuwadhibu na ahata kupelekea kuwa ua kutoakana na hata kama wakiwapeleka mahakamani wale waliofanya makosa hakuna haki itakayopatikana huko mahakamani. Kwa hiyo tunapaswa kufanya juu chini kuhakikisha tunapata mahakam huru ziweze kutenda na kutoa haki kwa wote, mwenye haki apate haki yake na alievunja sehria au kufanya makosa aadhibiwe kisheria kutokana na kosa alilolifanya.
  • Kuondosha kipengengele cha ukomo wa muda kwa viongozi. Tanzania imekua ikijaaliwa na viongozi waadilifu, wachapakazi, wawajibikaji, pia wameonyesha nia nzuri kwa kutekeleza ahadi zao zote walizo ziahid na kufanya miradi mikubwa mikubwa ya kimaendelo. Viobgozi hawa hawatakiwi kuondoka hivhivi tu kwa kisingizio eti muda wa wao kuongoza umeisha kisheria, tukumbuke sio rahisi kumpata kiongozi wa namna hii katika dunia ya sasa, kwa hiyo tunapaswa kuondosha kipengele cha ukomo ili tukimapata kiongozi wa aina hii basi tuendelee nae mpaka anatakapo choka yeye mwenyewe kwa lengo la kuendeleza maendeleo nchini.
  • Kuwa adhibu viongozi wanaoshindwa kufikia malengo ya majukumu yao au ahadi zao kwa angalau 65%. Tanzania imekua ipo nyuma kimaendeleo kutokana na kukosa vifungo vya katiba vya kuwawajibisha viongozi walioshindwa kutekeleza na kukamilisha majukumu yao kisheria au ahadi zao walizo zitoa wakati wa kampeni kwa mda wote walikuwepo kwenye nafasi za uongozi. Hivo tunapaswa kuweka vifungu hivi ili tupate wagombea wenye nia njema na nchi na sio wenye nia ya kwenda kujinufaisha kiuchumi, pia kuwekwe form inakayo elezea vifungu hivi vyote, form ambayo kila mwenye nia ya kugombea nafasi yoyote katika serikali basi kwanza atatakiwa aisome vizuri na kwa umakini na akubali vipengele vyote na mashart yake kabla ya kujaza form au kugombea, likiwemo hili la kuwajibishwa endapo muhula wa muda wake wa kuwepo madarakani ukiisha na ameshindwa kutimiza majukumu yake kisheria au ahadi zake, basi sheria ichukue mkomdo wake kwa kuchukulia hatua za kinidhamu kisheria. Tukifanikiwa kuweka kipengele hiki kwenye katiba yetu zidi ya viongozi basi naiona Tanzania yenye maendeleo kuliko hata nchi za ulaya.​
Hayo ndio mawazo yangu kuhusu Tanzania tuitakayo na kiukweli mawazo haya ni mzuri sana na yanatekelezeka kiurahisi endapo tutakua na nia ya kweli ya kufanya mabiliko ili tupate maendelo nchini kwetu.
 
Umezungumza vizuri, mambo kama katiba na uhuru wa mihimili ya serikali. Nimelipenda hasa wazo la kuwawajibisha watendaji na viongozi wasiofikia japo asilimia fulani za kazi walizoapa kuzitekeleza.
.....Kuwa adhibu viongozi wanaoshindwa kufikia malengo ya majukumu yao au ahadi zao kwa angalau 65%....


Naona tu kauli za kujumuisha kuweka asilimia zote hazitufai.

Ni kweli tunahitaji mabadiliko kadha wa kadha katika katiba, mahakama na taasisi ulizotaja. Lakini sio kusema mojakwamoja kwamba. Kilichopo hakifai kabisa mfano kauli kama;
ahakama zote hapa nchini zimekua hazitendi haki kwani zimekua ndio sababu ya kupindisha haki kua batili na batili kua haki kwa kungalia nafasi, cheo na utajiri wa mtu
Na

Chaguzi zote zilizopita sio huru na haki,
Kwa hiyo hata wakati anashinda chama tawala, au anashinda mpinzani je? Bado sio huru?

Sitaweka kauli zote lakini nakubaliana nawe kuwa tunahitaji mabadiliko kadha wa kadha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom