SoC04 Siasa za Tanzania na utawala wa kesho

Tanzania Tuitakayo competition threads

Loyadom

Member
Jul 19, 2022
55
51
SIASA ZA TANZANIA NA UTAWALA WA KESHO
Siasa ni njia ya kufanya maamuzi katika njia tofauti tofauti katika jamii kwa mfano Miji, Taifa au hata dunia nzima, katika demokrasia kila mtu ana kiasi Fulani cha nguvu, Hivyo tunahitaji mwanasiasa awe na ukweli na uwajibikaji kwani siasa haimaanishi udanganyifu kama unaofanyika hapa nchini kwetu, vyama vya siasa vinatumia uongo mwingi na ahadi za uongo kujipatia kura kutoka kwa wananchi. Tunahitaji siasa safi na bora zaidi ya hii ya sasa ili tuijenge Tanzania iliyo bora na viongozi bora Zaidi wanaoweza kujali wananchi Zaidi ya masirahi yao binafsi.

Hivyo Tanzania ya kesho tunahitaji kua Na;- Upinzani imara bila uoga na vitisho. Tunahitaji siasa inayo maanishwa kweli kama kusudi la kufanya mfumo wa vyama vingi nchini, upinzani kwenye serikali kuu ndio unafanya mabadiliko makubwa nchini, kukemea mienendo isiyo na maana kwa viongozi wakuu nchini, inajenga uongozi bora na hiyo ndio siasa tunayo hitaji nchi hii.

Watu wasio waoga, mfano mzuri tutazame bunge letu la sasa baada ya uchaguzi mkuu wa 2020 upinzani umekua mdogo sana bungeni wengi wao ni wabunge wa Chama kimoja, wengi wao ni kusifia raisi wa jamuhuri tu, vipi kuhusu kuwasemea wananchi walio kupeleka bungeni.

Baadhi yao tunaona wakihoji sana kuhusu serikali wanazimiwa maiki au kupunguziwa muda wao wa kuchangia, kwa kisingizio cha TAARIFA SPIKA kwa mfano may 5, 2017 mkutano wa saba wa bunge, joseph mbilinyi alizimiwa maiki, Hivyo kutengeneza wanasiasa wanao sifia tu kiongozi mmoja, na Uoga wa viongozi kuogopa kuhoji . Tanzania hatuwezi kutoka hapa tulipo kwa namna hii ya siasa zetu Tunahitaji watu wenye nguvu ya kuhoji kwani Hakuna alie juu ya sheria kama katiba yetu ya jamuhuri ya muungano wa tanzania yam waka 1977 (CURT) inavyo eleza katika

Ibara ya 13 (Equality before the law) Iki maanisha hakuna alie juu ya sheria. Hii ndio Tanzania
tuitakayo kisiasa na kiutawala pia na vyote vinawezekana kama tutapata viongozi sahihi. Nchi yetu tunahitaji utawala wa sheria kwa vitendo na sio tu kuwepo kwa nadharia kwamba tunao utawala wa sheria wakati wanasiasa wengi wakiikosoa serikali wanawekwa ndani huo, sio utawala wa sheria, wakati tukiwa na mfumo wa vyama vingi nchini.

Uwajibikaji
Ni hatari sana kwa taifa letu lijalo kuona viongozi wetu wengi wanakua na tabia za UCHAWA. Pia taifa letu linakabiliwa na IMPUNITY (Ukosefu wa uwajibikaji) wale wanaotakiwa kuwajibishwa kwa makosa yao kama ubadhilifu wa fedha kutokana na ripoti za mgaguzi mkuu wa serikali wanaendelea kuwepo kinacho fanywa ni kuhamishwa tu, hii sio Tanzania tuitakayo.

Tunahitaji viongozi wenye maono makubwa na wazalendo katika nchi hii kwa mfano Mbunge mmoja kutoka jimbo la Geita vijijini alitoa hoja yake bungeni kwa kusema nanunuku “Viongozi wanotajwa kwenye ripoti ya CAG Mbona hawawajibishwi mnawahamisha tu? Nchi hii inayo maeneo mengi sana ya wazi wakamatwe wafungwe wapewe mashamba walime hadi pesa walizokula zirudi kupitia kazi hizo” Kwa namna moja au nyingine wazo lake linaweza kusaidia sana.

UWAJIBIKAJI na kutengenea taifa lenye viongozi imara na wenye maono mazuri nan chi yao, sasa kwa sasa nani wa kuwawajibisha kwa makossa yao yanayo jirudia kila mara. Katika bunge la la 10 mwaka 2015 aliekua mbunge wa singida mh. Tundu lissu alisema nanukuu “majaji wamekamatwa wamekura rushwa na riporti ipo mpaka sasa wameachwa bado wanafanya nini?

Wakamatwe na wezi wengine wakiwemo mawaziri wasiachiwe kwenda kula pesa za wizi” mwisho wa kunukuu, Hivyo inaonekana bado kuna changamoto sana nchi yetu kwa upande wa siasa. Hatuhitaji uongozi wa namna hii, kujenga Tanzania bora. Vijana imra wenye hoja thabiti na sio Uchawa na Uoga.

Vijana kwa sasa kuingia kwenye siasa kumekua na ugumu sana ukiangalia mwenendo wa siasa nchini kwetu hapa ukisema vibaya serikali unakamatwa kama ilivyo onekana mwaka 2020 kwenye uchaguzi na baadhi ya wanaharakati wengi kukimbia nchi yao. Nikinukuu maneneo ya baba wa taifa mwalimu nyerere Alisema “Tunataka kuona taifa lina vijana jeuri na wenye kujiamini, vijana wanaojoji na kupiga vita mifumo isiyoshabihana na matakwa na matarajio ya kitanzania.

Tunataka vijana waasi dhidi ya mifumo kandamizi, ubwana na ufisadi katika Taifa” Hiyo ndo Tanzania ata baba wa Taifa hili alitamani kuiona kwasasa tutaipata wapi Vijana, wengi wamekua waoga kwa Vitisho na mwenendo wa siasa za nchi yetu Ukihoji sana kuna vikundi vya watu wasiojulikana Serikali haiwatambui pia!? April 10, 2017 mbunge wa nzega mjini aliomba bunge lisikilize kikundi hicho kinatoka idara ya usalama wa Taifa, kinacho teka watu kama ilvyo ripotiwa na millardayo kupitia youtube yake. Hivyo vijana wengi wanatumika vibaya kama machawa kwa pesa wanazo pewa Tunahitaji Vijana imara na bora kama mwalimu nyerere alivyo tamani tutengeneze taifa bora na siasa imara nchini.

Imekua nikwa muda mrefu sasa tangu mfumo wa vyama vingi uanze katika taifa letu hili, Siasa haibadiliki, michezo ndio ileile kwa mfano katika hotuba ya kiongozi wa chama cha siasa hapa nchini akiwa mkoa wa Iringa amesema nanukuu “Kuna mgogoro mkubwa sana ndani ya chama chetu, hasa wakati huu wa uchaguzi ndugu zangu tuwe makini na mtego huu, sababu kubwa ni pesa chama hakina pesa sijui hizi za kugawa zinatoka wapi?” Hii inaonekana ni kama kuna vitu vinaendelea ndani ya chama na kiongozi wa ngazi ya juu kama huyo anashindwa kujua pesa zinatoka wapi. Hivyo unabaki kujiuliza Kwahiyo chama kinanunuliwa? Kama ndivyo ina maana gani kwenye nchi ya kidemokrasia, na vitaisha lini vituko vya namna hii.

Hitimisho; Kazi ya uongozi ni kujenga watu wawe na umoja mambo ya kuchochea, chuki sio lengo la uongozi Hivyo tunahitaji wale wanao weza kuongoza watu kwa kuwaunganisha kupitia hoja zao na sio kwa kutumia njia mbalimbali Zaidi ya hoja zao.
 
Tanzania iliyo bora na viongozi bora Zaidi wanaoweza kujali wananchi Zaidi ya masirahi yao binafsi.
Napendekeza viongozi wayapate maslahi yao binafsi wakati huohuo wakiwajali wananchi. Kila mtu awajibike tu. Haki ndiyo inataka hivyo.

Mi nikigombea sitawadanganya wananchi kwamba nitajimima nisile chakula ili nchi ineemeke. La. Hiyo haitakuwa haki. Sema nitawaambia ukweli nitatimiza majukumu yangu kikamilifu huku nikiridhika kwa mshahara na marupurupu yaliyo haki yangu kabisa 😆.

Watu wasio waoga, mfano mzuri tutazame bunge letu la sasa baada ya uchaguzi mkuu wa 2020 upinzani umekua mdogo sana bungeni wengi wao ni wabunge wa Chama kimoja, wengi wao ni kusifia raisi wa jamuhuri tu, vipi kuhusu kuwasemea wananchi walio kupeleka bungeni
Ninakubali, kusifia tu pasipo kukosoa ili kujenga haitatufikisha mbali kama Taifa. Kweli ni lazima tuwe na vyama tofauti ili kuzipa changamoto hoja kwa nia ya kuziimarisha zitoke katika tanuru kama dhahabu safi. Isisomeke kama upinzani ni kupinga tu kila kitu, tutarudi palepale mraba wa kwanza.

Hoja zikosolewe na kusifiwa na kusukwa upya kwa ushieikiano wa uoinzani na chama tawala. Maana tunajenga nchi moja mazee.

Uwajibikaji
Ni hatari sana kwa taifa letu lijalo kuona viongozi wetu wengi wanakua na tabia za UCHAWA. Pia taifa letu linakabiliwa na IMPUNITY (Ukosefu wa uwajibikaji) wale wanaotakiwa kuwajibishwa kwa makosa yao kama ubadhilifu wa fedha kutokana na ripoti za mgaguzi mkuu wa serikali wanaendelea kuwepo kinacho fanywa ni kuhamishwa tu, hii sio Tanzania tuitakayo.
Hakika, kitu tunachohitaji kutupatia kasi kama taifa. Ni kila mmoja tu kuwajibika kwa kile anacholipwa kukifanya. Ova.

“Viongozi wanotajwa kwenye ripoti ya CAG Mbona hawawajibishwi mnawahamisha tu? Nchi hii inayo maeneo mengi sana ya wazi wakamatwe wafungwe wapewe mashamba walime hadi pesa walizokula zirudi kupitia kazi hizo” Kwa namna moja au nyingine wazo lake linaweza kusaidia sana.
Hesabu zinafanyika, mtu analipia na fidia juu. Kwa haki haitamsumbua mtu. Lakini tuwe makini, iww ninkwa haki ili isije kutumika kuzima upinzani tena na mawazo tofauti mfano ile ya mtu akihiji ndio aanze kukaguliwa mapato na uraia. La hii si sawa. Kipimo kilekile anachopimiwa anayesifu, na anaye kosoa kujenga pia. HAKI.
Hitimisho; Kazi ya uongozi ni kujenga watu wawe na umoja mambo ya kuchochea, chuki sio lengo la uongozi Hivyo tunahitaji wale wanao weza kuongoza watu kwa kuwaunganisha kupitia hoja zao na sio kwa kutumia njia mbalimbali Zaidi ya hoja zao.
Mtoa mada machachari kabisa umetufungia vizuri kwa kusisitiza umoja wa kitaifa. Tanzania tuitakayo✔
 
Napendekeza viongozi wayapate maslahi yao binafsi wakati huohuo wakiwajali wananchi. Kila mtu awajibike tu. Haki ndiyo inataka hivyo.

Mi nikigombea sitawadanganya wananchi kwamba nitajimima nisile chakula ili nchi ineemeke. La. Hiyo haitakuwa haki. Sema nitawaambia ukweli nitatimiza majukumu yangu kikamilifu huku nikiridhika kwa mshahara na marupurupu yaliyo haki yangu kabisa 😆.

Ninakubali, kusifia tu pasipo kukosoa ili kujenga haitatufikisha mbali kama Taifa. Kweli ni lazima tuwe na vyama tofauti ili kuzipa changamoto hoja kwa nia ya kuziimarisha zitoke katika tanuru kama dhahabu safi. Isisomeke kama upinzani ni kupinga tu kila kitu, tutarudi palepale mraba wa kwanza.

Hoja zikosolewe na kusifiwa na kusukwa upya kwa ushieikiano wa uoinzani na chama tawala. Maana tunajenga nchi moja mazee.

Hakika, kitu tunachohitaji kutupatia kasi kama taifa. Ni kila mmoja tu kuwajibika kwa kile anacholipwa kukifanya. Ova.

Hesabu zinafanyika, mtu analipia na fidia juu. Kwa haki haitamsumbua mtu. Lakini tuwe makini, iww ninkwa haki ili isije kutumika kuzima upinzani tena na mawazo tofauti mfano ile ya mtu akihiji ndio aanze kukaguliwa mapato na uraia. La hii si sawa. Kipimo kilekile anachopimiwa anayesifu, na anaye kosoa kujenga pia. HAKI.

Mtoa mada machachari kabisa umetufungia vizuri kwa kusisitiza umoja wa kitaifa. Tanzania tuitakayo✔
Kweli, Tukizingatia hayo nchi itakua Bora , Tatzo kubwa pia tunaishi Sana na nadharia kuliko kutenda .
 
Back
Top Bottom