Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,865
- 3,810
Mwaka 2021 majira ya joto Manchester City walipeleka ofa Tottenham ya Dola mil 100 kutaka kumnunua Kane. Tottenham wakatia ngumu kumuuza. Kane akagoma kujiunga na timu yake kwa ajili ya mazoezi ya pre-season ili kushinikiza kuuzwa.
Tottenham hawakutishika wakashikilia chuma na hawakuwa tayari kufanya mazungumzo yoyote na Man City kwani walikuwa bado wanamuhitaji Harry Kane.
Gaudiola alipoulizwa kuhusu hili swala alisema" Kane ni mchezaji halali wa Tottenham, kama hawataki kufanya mazunguzo (Negotiations) nasi basi imeisha hiyo hatuna cha kufanya." Mwisho wa siku Kane alisitisha mgomo wake na kurudi kujiunga na timu hadi leo.
Maswali ya kujiuliza;
Kwanini Kane hakuondoka kwa nguvu ili alipe faini kama Mawakili wa Feitoto wanavyoshinikiza? Mbona watu hawakuilaumu Tottenham kugoma kumuuza wakati mchezaji aliweka wazi kuwa anahitaji changamoto mpya?
Leo kuna watu wamekazana kuipigia kelele Yanga imuuze Fei kwa sababu hajisikii kuendelea kucheza Yanga wakati bado yuko ndani ya mkataba. Hivi kama kila mchezaji ataondoka kienyeji hivo sasa nini maana ya mkataba?
Shida Tanzania tunaendesha soka letu kwa hisia (mihemko) zaidi kuliko kufuata sheria na kanuni. Inashangaza kuona hadi sasa Feitoto hajachukuliwa hatua zozote za kinidhamu. Harry Kane aliona mwisho wake ni mbaya ndio maana alifanya maamuzi ya kurudi klabuni.
Nasikitika jinsi ujinga wa Wanasheria wa mchongo na wachambuzi uchwara unavyoenda kupoteza kipaji cha Fei.