Je, Harry Kane atamaliza gundu la makombe Bayern?

Avicii

Member
Sep 16, 2023
56
68
Habari Wana jf wote. Moja Kati ya washambuliaji bora wa wa Kati kwa Sasa ni Harry kane mshambuliaji anayeichezea Bayern Munich ya ujerumani katika bundesliga.

Kabla ya kujiunga na Bayern alikuwa akiichezea Tottenham Hotspurs ya uingereza na akiwa huko aliifungia zaidi ya magoli 200 akifunga magoli zaidi ya 20 kwa misimu mitano mfululizo. Punde baada ya kujiunga na Bayern alivunja rekodi ya mabao iliyowekwa zaidi ya miaka 40 pia ndio anaongoza kwa mabao kwenye ligi tano kubwa ulaya.

Pamoja na mafanikio yote hayo Jambo la kustaajabisha ni kuwa Harry kane hajawahi kuchukua kombe lolote katika Maisha yake ya soka! .

Inashangaza wakati wachezaji wa kawaida Kama Olivier giroud Ana kombe la dunia kane Hana hata carabao. Ndipo kane akachukua uamuzi wa kuachana na Spurs na kujiunga na Bayern wengi tuliamini kane anaenda kuchukua MAKOMBE.

Picha linaanza Bayern anatolewa na timu ya ligi daraja la tatu kwenye dfb pokal ambalo ndio FA ya ujerumani hatujakaa sawa inaibuka bayer Leverkusen ya legend xabi Alonso inauwasha Moto na kushangaza Kila mpenda soka inatangaza ubingwa ikiwa na zaidi ya mechi nne mkononi Tena bila kupoteza mchezo katika michuano yoyote. Na mojawapo Kati ya mechi iliyowapa ubingwa alimpiga Bayern mwenyewe 3-0.

Na misimu huo huo Bayern amefungwa nyumbani alianz arena na mahasimu wao borrusia dortmund baada ya zaidi ya misimu 10. Wakati kane anajiunga na Bayern walikuwa wanachukua back to back ya bundesliga. Binafsi Mimi ni die fans wa arsenal the Gunner's niliangalia wakati Bayern wanatuondosha na niliiona sura ya kane.

Sasa wamefanikiwa kufuzu nusu fainali na watakutana na wenye kombe lao real Madrid waliowaondoa wazee wa total football man city wakati huo mahasimu wao borrusia dortmund wao watakutana na psg ya kyllian mbappe ndio kombe pekee walilobakiwa nalo Bayern na Harry kane kuondoa mkosi UEFA CHAMPIONS LEAGUE ni ngumu lakini inawezekana
 
Kwani huu ni msimu wake wa mwisho baada ya hapa anastaafu?
 
Habari Wana jf wote. Moja Kati ya washambuliaji bora wa wa Kati kwa Sasa ni Harry kane mshambuliaji anayeichezea Bayern Munich ya ujerumani katika bundesliga. Kabla ya kujiunga na Bayern alikuwa akiichezea Tottenham Hotspurs ya uingereza na akiwa huko aliifungia zaidi ya magoli 200 akifunga magoli zaidi ya 20 kwa misimu mitano mfululizo. Punde baada ya kujiunga na Bayern alivunja rekodi ya mabao iliyowekwa zaidi ya miaka 40 pia ndio anaongoza kwa mabao kwenye ligi tano kubwa ulaya. Pamoja na mafanikio yote hayo Jambo la kustaajabisha ni kuwa Harry kane hajawahi kuchukua kombe lolote katika Maisha yake ya soka! . Inashangaza wakati wachezaji wa kawaida Kama Olivier giroud Ana kombe la dunia kane Hana hata carabao. Ndipo kane akachukua uamuzi wa kuachana na Spurs na kujiunga na Bayern wengi tuliamini kane anaenda kuchukua MAKOMBE . Picha linaanza Bayern anatolewa na timu ya ligi daraja la tatu kwenye dfb pokal ambalo ndio FA ya ujerumani hatujakaa sawa inaibuka bayer Leverkusen ya legend xabi Alonso inauwasha Moto na kushangaza Kila mpenda soka inatangaza ubingwa ikiwa na zaidi ya mechi nne mkononi Tena bila kupoteza mchezo katika michuano yoyote. Na mojawapo Kati ya mechi iliyowapa ubingwa alimpiga Bayern mwenyewe 3-0. Na misimu huo huo Bayern amefungwa nyumbani alianz arena na mahasimu wao borrusia dortmund baada ya zaidi ya misimu 10. Wakati kane anajiunga na Bayern walikuwa wanachukua back to back ya bundesliga. Binafsi Mimi ni die fans wa arsenal the Gunner's niliangalia wakati Bayern wanatuondosha na niliiona sura ya kane . Sasa wamefanikiwa kufuzu nusu fainali na watakutana na wenye kombe lao real Madrid waliowaondoa wazee wa total football man city wakati huo mahasimu wao borrusia dortmund wao watakutana na psg ya kyllian mbappe ndio kombe pekee walilobakiwa nalo Bayern na Harry kane kuondoa mkosi UEFA CHAMPIONS LEAGUE ni ngumu lakini inawezekana
Mkuu ushasema wanakutana na wenye kombe lao unadhani nini kitatokea?😃😃
 
Atachukua tu just a matter of time..na uhakika msimu ujao Bayern atabeba taji la Bundesliga
 
Basi makombe bado nafasi anayo kuyapata.
Possibility hiyo ipo Ila kwa kukutana na Real Madrid nusu fainali na kikosi kile cha vijana wenye uchu wa Real possibility ya kusonga mbele Buyern ni ndogo sana. Ila mpira unadunda ngoja tuone itakuwaje...
 
1713460517267.png

Huyu Babu hakuna mwenye atapingana naye UEFA hii.Ataibeba tena...waliobaki wote watoto wadogo mziki ni mkubwa Madrid kule😀😀😀😀😀😀
 
Mnaipigia hesabu kuiondoa Madrid UEFA? Kimpira inawezekana sababu matokeo huwa yanadunda ila ukitazama uchezaji wa mpira, tactics etc Madrid anabeba hili kombe la UEFA 2023/2024.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom