Soma stori hii kabla haujaamua kuoa mke wa pili

Mbahili

Senior Member
Nov 28, 2016
185
283
Baada ya kukaa kwenye ndoa kwa miaka miwili Ally alitaka kuoa mke wa pili, Mama yeke alimuuliza sababu akasema kuwa mke wake kabadilika sana, tangu amekuoa amekua mtu wa kisirani, mtu wa kumfuatilia kila hatua, amekua mtu wa kulalamika na kila siku nyumbani ni kelele, alimuambia kuwa siku hizi hawezi kukaa nyumbani kwa amani, nyumba ni chafu akija hata na wageni anaona aibu, akasema naahitaji kuoa mwanamke mwingine ili angalau roho yeke itulie.

Mama yake alimkubalia na kumuambia sawa, lakini alimuomba kitu kimoja, alimuomba kuwa kabla ya kuoa basi kuna sehemu anataka waende na mtoto wao ambaye ndiyo alikua na mwaka mmoja tu. Alimuambia kuwa atakaa huko wiki moja na akirudi basi atakua ashamtafutia mke mwingine mzuri ambaye hatakuja kumsumbua. Ally alikubali, alimchukua binti yake wa mwaka mmoja na kuongozana na Mama yake.

Walienda katika mji mpya kabisa, ulikua ni mji mzuri, Mama yake alimuambia ampe simu yake na kila pesa aliyokua nayo, ndani kulikua na kila kitu, lakini Mama yake alichukua pesa na ATM card yake na kuondoka navyo, alimuachia simu ambayo ilikua na namba yake tu. Aliondoka na kumuambia kuwa kama akiweza kuishi pale kwa wiki moja bila kumtafuta kwenye simu basi anaweza kuoa mwanamke mwingine. Mama yake aliondoka na kumuacha pale, siku ya kwanza ilikua nzuri alikula na kucheza na mtoto.

Siku ya pili mtoto alilia sana, hakupenda vyakula vya mule ndani alikua akitaka maziwa ambayo yaliisha, alihangaika kumbembeleza kwani hakua na pesa kabisa, alifanikiwa lakini siku iliyofuata alimpikia chakula mtoto akagoma kula ikabidi kupika kingine akaanza kula ila alipomaliza alikitapika chote. Ali alikua akifanya usafi lakini ile akipitiwa na kausingizi kidogo anaamka na kukuta mtoto kamwaga kila kitu chini, alikua yeye na mtoto tu lakini alichoka, Pampas ziliisha na hakua na pesa, aliwaza kumpigia simu Mama yake lakini akaona hapana.

Alijitahidi kumfunga khanga lakini mtoto alianza kuumwa na hakua na hata Shilingi kumi hapo ndipo alilazimika kumpigia simu Mama yake. Mama yake alikuja na kukuta nyumba imechafuka haitamaniki. Alimuangalia mwanae ana kumuuliza kama bado anadhani mke wake ni kisirani? Ally alimuambia hapana nadhani natakiwa kumpenda mke wangu zaidi na kumsaidia, kuwa Mama ni kazi ngumu, mimi sijaweza kumaliza wiki moja lakini yeye anafanya hivi kila siku ya maisha yake.

Aliondoka na kurudi kwa mkewe, alimpelekea zawadi na kila mara alipopata nafasi alienda kumsaidia kazi za nyumbani ili asichoke. Alishangaa nyumba inakua na amani, mke wake anakua na furaha kwania ngalau ana mtu wa kuongea naye.

Siku moja Mama yake alienda kumsalimia na kumuambia kuwa kama ukioa mwanamke ana akawa Mama asibadilike kukusumbua kuhusu maisha basi jua huyo atakua anaigiza au si Mama bora kwani wajibu wa kwanza wa Mama ni kuwa na wasiwasi kuhusiana na wanae hivyo hata ukinywa bia moja basi lazima awaze unechezea pesa kwakua anawaza ungenunua tofali au nguo za watoto!
 
Kwanza kuoa mke wa pili ni dhambi
 
Sasa ilitakiwa na baba ake ally amchukue mke wa Ally aende nae mjini kazini kwa Ally kwa muda wa mwezi mzima, akapambane na mitikasi za kutafuta ela halafu kila akirejea Ally awe anamsomea mkeka wa mahitaji bila kujali utulivu wake wa akili na uchovu, amuombe hela za madeni ya marejesho ya vikoba sijui songesha ambayo hata hajui imetokea wapi, halafu aanze kuomba simu atolewe password anataka kupiga kwao kusalimia halafu akirejea amuulize Juma ndio nani na kwann mnachat chat hovyo?

Halafu anune bila sababu awe anabamiza bamiza milango na kutupa vitu, awe anamjibu vifupi kwa jazba na kadhalika.

Kimsingi amsumbue kichwa, halafu tuone kama mke wa Ally ataweza vumilia hizo Drama.
 
Back
Top Bottom