Ndoa ya mke mmoja ni mpango wa shetani tusiache uzinzi?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,372
104,447
Nauliza kwa upole, tujadiliane bila jazba.
Sidhani kama kuna mwanaume mwenye mpenzi au mke mmoja tu. Katika marafiki zangu milioni moja huyo mtu hayupo, labda useme huko hali ipoje.

Nimejaribu tu kuwaza, labda ni mpango wa shetani kuchomekea hii itikadi. Alichomekea akijua huu mtego hawa hawatauweza badala yake watadumbukia kwenye dhambi ya uzinzi...simple. Mfano mimi kama kuzini isingekuwa dhambi basi ningeingia mbinguni mapema kabisa.

Mimi sio mtaalamu sana wa biblia, walioichimba vizuri mtueleze kivipi na wapi Mungu alikataza mke zaidi ya mmoja? Isije kuwa ni mpango wa shetani kupotosha ili tubaki na mke mmoja halafu tukazini nje kisha tupate dhambi kizembe kabisa?
 
Hizi ni drama za dini na vitabu vyake vilivyo tungo na vilivyo haririwa na mwanadamu ili kukidhi vionjo vyao na kukuza propaganda zao.

Kama mwanadamu angekuwa mtiifu kwa asili kama walivyo wa nyama na viumbe vingine tunavyo viita havina akili nusu ama robo tatu ya changamoto zilizopo leo zisingekuwepo.
 
Muswati ana 17,nadhani atakuwa na 20 mwaka huu,kila mwaka vigori wanapanga mstari achague mwingine.

Hajawahi kusema wanatosha.
 
Kama ni muwaka tamaa utawaka tu hata uwe na wake 700 kama Mfalme Sulemani; na sitashangaa kusikia kwamba hata waliooa wake wengi nao hawako nyuma kwa kuwa na michepuko. Suala la michepuko linachagizwa na sababu za kibayolojia, kisaikolojia, kinafsiya, kiuchumi pamoja na mfumo mzima wa jamii.

Kwa hivyo sidhani kama kuna uhusiano wa kiusababishi (causal relationship) kati ya kuwa na mke mmoja na utitiri wa michepuko.

➡️➡️➡️ Eti hali ya uzinzi kwa wanaume ikoje huko Mashariki ya kati na kwingineko ambako ni kawaida watu kuoa mke zaidi ya mmoja? Hapa kwetu Zanzibar hali ikoje? Wanaume hawachepuki? 😳
 
(Mathayo 19:4-6)

NDOA ilianzia bustani ya Eden, Hakuna popote pameandikwa Adam alichepuka,

Ikupe kujua ikiwa u mzinzi, ni pekeako, wapo wanaume wangi ndani ya NDOA waaminifu.

Alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe, na NDOA iheshimiwe na watu wote.

Amen
 
Back
Top Bottom