SoC04 Sitasahau nilivyokoswa na kiberenge enzi za utoto wangu

Tanzania Tuitakayo competition threads

Yuh003

Member
Mar 25, 2022
5
5
Katika kipindi cha makuzi watoto wengi huwa wanapitia nyakati ambazo huatarisha maisha yao hususani watoto ambao ni watundu sana.Sasa kuna kipindi cha utoto wangu tulikuwa na kawaida ya kuzurula sana.

Tunajikusanya watoto wa mtaa mzima kila ifikapo wakati wa jioni tunaelekea Relini kucheza katika Daraja la Treni.Nakumbuka wakati huo nilikuwa Darasa la tatu siku moja nilichelewa kurudi nyumbani hivyo nikakuta wenzangu wameshaondoka kuelekea Relini.Basi nilipomaliza kubadili uniform nikatoka mbio mkukumkuku kuwahi wenzangu waliokuwa wametangulia Relini.

Pindi nilipofika Relini nikawaona wenzangu kwa mbali wameshavuka lile Daraja wapo upande wa pili kwa bahati nzuri ama mbaya na wao pia wakaniona wakaanza kuniita ili niweze kuwafuata upande wao.

Nikasogea katika lile Daraja na kuanza kuwafuata kwa wakati huo kutokana na umri kuwa mdogo hivyo sikuweza kuvuka kwa haraka,Daraja lilikuwa linatisha sana kwa upande wangu kwasababu chini ni mbali na muundo wake ulikuwa ni wa kupangwa magogo hivyo ilinibidi nipige hatua moja moja niweze kuvuka upande wa pili.

Wakati nipo katikati ya Daraja nikasikia king'ora kuashiria kuna chombo kinakuja nilipotazama vizuri nikaona chombo chenye rangi ya njano kinakuja kwa speed kali.Hivyo muda huohuo nilishauriana na Halmashauri ya akili yangu kwa haraka sana niligeuza nikaweka woga pembeni wa kuanguka chini ya lile Daraja ili niinusuru roho yangu kubutuliwa na Treni.

Namshukuru Mola wangu alinipa nguvu ya ajabu nikaanza kukimbia kama ninapaa mpaka nikafanikiwa kufika mwisho wa Daraja na kupata nafasi ya kurudi pembeni ili kile chombo kipite kwasababu Daraja halikuwa na nafasi sehemu za pembeni kwa wanaotembea kwa miguu.

Nakumbuka nilipewa zawadi za matusi kutoka kwa watu wazima waliokuwa wakishuhudia kinachoendelea wakati ule.

Hivyo sitaweza kusahau hii siku abadan.

Comment kisa chako na wewe cha hatari.
 
Back
Top Bottom