Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
14,770
10,660
Wakuu, nawatakieni amani na furaha mioyoni mwenu. Leo nina mada fupi tu kwa wote ambayo naomba tujadili.

Katika mahusiano ya mapenzi, hasa kwenye ndoa, kuna tofauti kubwa sana kati ya nini atakacho mwanamume na nini atakacho mwanamke.

1. Kwako mwanamke- Elewa kwamba heshima (respect) pekee ndiyo inayomweka mwanamume kwenye nafasi yake. Mwanamume anaweza kuwa anapendwa na kila aina ya mwanamke hapa duniani lakini ni heshima ndiyo itamtofautisha mwanamke wa maisha kwa mwanamume wala sio upendo. Mwanamke hakupewa kupenda, hii ni fact, ndio maana kwa wanawake utu wa ndani sio muhimu kuliko mafanikio ya nje. Kila mwanamke angetamani aolewe na Bill Gates au SS Bhakresa, ila tu kutokana na nafasi finyu na ushindani.

Hii ni kwa sababu mwanamke hana uwezo wa hisia za mapenzi ambazo ziko wazi (clear) bali huwa zimechanganyika hovyo (vague). Kama uko kwenye ndoa ama unataka ndoa imara, ni vema ukajifunza kumheshimu huyo aliye karibu yako, kwani hiyo ndio aina pekee ya upendo kutoka kwa mwanamke ambayo kila mwanamume huutafuta. Heshima humaanisha mapenzi ya kweli.

2. Kwenu wanaume - Mwanamke anataka upendo. Kama ni heshima, mwanamume huwaheshimu wanawake wote, kuanzia makahaba mpaka masista. Huu ni wajibu wa kila mwanamume hali, kumheshimu mwanadamu mwenye jinsia ya kike. Ndio maana zamani zetu haikuingia akilini mwanamke amesimama kwenye usafiri wa umma halafu kuna dume limekalia kiti, huu ulikuwa ni ukatili wa kijinsia. Kwa hiyo kinachomtofautisha mwenzi wako na wanawake wengine ni jinsi unavyompenda. Kumbuka heshima ni kwa wanawake wote lakini upendo ni kwa mkeo pekee.

Tatizo vijana wa siku hizi wamevurugwa kweli kweli na upuuzi wa kimagharibi. Unakuta kwa vile mwanamume anataka kuheshimiwa, mwanamke naye anatilia heshima, tena kwa kuwa mwanamke ànataka upendo basi mwanamume naye analilia kupendwa na mkewe. Aina hii ya mahusiano huwa haina safari ndefu kwani kila mmoja ataishi kwa kuigiza ili kumridhisha mwenza wake, lakini ikitokea tofauti ndogo tu ukweli hujidhihirisha.

Ndiyo hapo utasikia kauli mfano, nimekuvumilia sana. Ukweli si kwamba kakuvumilia bali kavimilia kuigiza kama anakuheshimu ama anakupenda, bali tangu mwanzo haikuwa hivyo. Alifanya tu ili akupate, na sasa hajakuchoka kama anavyodai ila amechoka kuishi maisha yasiyo halisi ya kuigiza, sasa anakuonysha rangi yake halisi.

Kumbuka, upendo wa mke kwa mume ni kumheshimu na heshima ya mume kwa mke kumpenda. Vyote vitoke moyoni kwa dhati, hapo mtaishi.
 
Wakuu, nawatakieni amani na furaha mioyoni mwenu. Leo nina mada fupi tu kwa wote ambayo naomba tujadili.

Katika mahusiano ya mapenzi, hasa kwenye ndoa, kuna tofauti kubwa sana kati ya nini atakacho mwanamume na nini atakacho mwanamke.
Mkuu ungefunguka zaidi kumheshimu mwanaume ni kufanyaje labda? Mfano kutii kila anachokuagiza au kusema au
 
Ili kuthibitisha kuwa mwanamke hakuumbiwa kupenda tazama pale mwanamume anapotaka mwanamke. Hutokea kijana kumtongoza binti ambaye wala hampendi kabisa kijana huyo. Siku za mwanzo aweza hata kumshitaki kwa wazazi kuwa anasumbua, akaacha hata kuitikia salamu.

Lakini kadri siku zinavyosonga, kama kijana huyu atakomaa kumtaka binti huyu jeuri, hali polepole itaanza kubadilika. Ghafla binti ataanza kujifunza kumpenda huyu kijana na kuanza kumwonea huruma kwa mateso anayomsababishia. Mwishowe kijana huyu ng'ang'anizi huibuka mshindi. Mwanamke hufundishwa kupenda na ndio maana mazingira yanayopelekea upendo huo yakitoweka penzi nalo huyeyuka.

Hii pia ndio sababu kwa nini si vema mwanamke awe exposed kwa watu hovyo hovyo tu. Kama mke ameona mazingira anayodhani ndio yaliyoamsha upendo hayapo tena, akipata mtu wa kumshika sikio kwa kumpa matumaini bandia hunasa kirahisi tu. Mwanamke huongozwa kwa hisia (emotions) ndio maana unapomtongoza ukienda na vesi za ukweli ni nadra kumpata.

Mwanamke hutekwa (respond) kwenye maneno matamu yanayomjengea picha ya kuwa sayari tofauti na wanawake wengine wote, na hana uwezo wa kuamua kama ni kweli ama ni uongo, hii ni fact bila kujali elimu ya kidunia. Mambo haya hayajali kama mwanamke ameolewa ama ni single, ni nature yao. Ndio maana si sahihi mwanamke eti awe busy anazunguka kwenye biashara na vijiweni, mara kwa mashoga zake wasio kichwa wala miguu. Elewa kuwa awapo huko ni easy target kwa snipers.
 
Ili kuthibitisha kuwa mwanamke hakuambiwa kupenda tazama pale mwanamume anapotaka mwanamke. Hutokea kijana kumuongoza binti ambaye wala hampendi kabisa kijana huyo. Siku za mwanzo aweza hata kumshitaki kwa wazazi kuwa anasumbua, akaacha hata kuitikia salamu.
Nimekuelewa Sana hapa mkuu
 
😂😂😂 yule manzi nilitaka niweke kambi kabisa....kosa kubwa alilolifanya ni kuniita mlugaluga.......nilimkatia waya zote kama haitoshi akala na block........sipendi dharau kutoka kwa wavaaa chupi zenye maua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom