Katika kizazi cha sasa Wanawake wengi hawatafuti Mapenzi, wanatafuta msaada- Rev lucy natasha

Analog

Senior Member
Apr 4, 2024
180
395
Mwanamke pia sharti uwe na uwezo wa kuleta mezani vitu kama title deed, logbook, biashara, kampuni. Ni lazima tuwe na kizazi cha wanawake ambao kazi yao sio tu kuchora eyebrows, chora eyebrows na mipango ya kibiashara pia,” alisema.

Muhtasari

• “Kwa hiyo hawa hawako kwako kwa sababu ya moyo bali kwa sababu ya mkono, hawa huja kimakusudi kwa sababu ya kile ambacho watapata kifedha kutokana na uhusiano,” aliongeza.



Mchungaji Lucy Natasha ametoa vidokezo muhimu kwako wewe uliyeko sokoni kutafuta mpenzi wa kuoa au kuolewa naye.

Kupitia mazungumzo kwenye chaneli ya YouTube ya Obinna, Lucy Natasha alisema kwamba kwa upande wa wanawake, mrembo yeyote anayeomba pesa katika mapenzi huyo hajafuata ndoa bali msaada.

“Aina ya kwanza ya mwanamke ambaye mwanamume yeyote anayetafuta mke hafai kumuoa, ni yule anayekupenda kwa sababu ya pesa. Kwa sababu katika kizazi cha sasa, wanawake wengi hawatafuti mapenzi, wanatafuta msaada, ambapo ni kizazi kibaya sana,” Natasha alianza kushauri.

“Kwa hiyo hawa hawako kwako kwa sababu ya moyo bali kwa sababu ya mkono, hawa huja kimakusudi kwa sababu ya kile ambacho watapata kifedha kutokana na uhusiano,” aliongeza.

Hata hivyo, mchungaji huyo alisema kwamba si vibaya kwa mtu kumpa pesa umpendaye lakini tatizo moja tu analo kwa wanaojificha ndani ya pesa kwa lengo la kupata pesa ni kwamba wengi wanataka kupokezwa bila wao kutoa.

“Kama mwanamke wakati unaolewa, kitu pekee ambacho unaleta mezani kisiwe ni cheti chako cha kuzaliwa. Ukiolewa kama mwanamke pia sharti uwe na uwezo wa kuleta mezani vitu kama title deed, logbook, biashara, kampuni. Ni lazima tuwe na kizazi cha wanawake ambao kazi yao sio tu kuchora eyebrows, tuwe na wanawake wanaoweza kuchora eyebrows na mipango ya kibiashara pia,” alisema.

Kwa upande wa wanawake walioko kwenye saka saka za mpenzi, Natasha aliwashauri kuangalia kwa mtu aliyeokoka.
 
Nyie si huwa mnataka tuwe na pesa halafu tuishi na mke m'moja, basi na ninyi muwe na hela halafu muwe pisi kali halafu msiwe na ghubu ni adabu kwenda mbele.

Kama hamtaki basi kazi iendelee.
Hiko kitu hakiwezekani abadani, ukitaka kumtawala mwanamke kuwa na PESA kila kitu atakusikiliza.
 
Wanawake niwavivu na hawapendi kujishughulisha kiuchumi NB (wanawake wa kiafrica) Ukitaka kujua wanawake kwa asilimia kubwa wanatafuta misaada akikuona unahuo msaada hata umkate kidole kimoja kimoja kila siku Hana uwezo wakutoka kwako😅
 
Wanawake niwavivu na hawapendi kujishughulisha kiuchumi NB (wanawake wa kiafrica) Ukitaka kujua wanawake kwa asilimia kubwa wanatafuta misaada akikuona unahuo msaada hata umkate kidole kimoja kimoja kila siku Hana uwezo wakutoka kwako😅
😀😀😀Kabisa mzee wengi wavivu na wako tayar wawe watumwa kwa ajili ya hela.
 
Utandawazi unaivuruga sana dunia au sijui ndiyo binadamu tumekuwa updated!?nimekua simjui baba (deceased) lakini nikikumbuka walivyokuwa wakiishi wazazi wa rafiki zangu na majirani sikuwahi kufikiria kama nao walikuwa na uoni wa kizazi cha leo.

Ningetegemea kuona huyo mchungaji wa kike akifundisha namna bora ya familia kushirikiana malezi huyu atafute kipato cha familia huyu akae karibu na watoto lakini yale yale tafuteni vipato muweke mezani ili muheshimiane,ukweli hii ni shida kubwa kwa sasa hatuwezi kuiona lakini ipo siku tutarudi kujadiliana hapa.
 
Back
Top Bottom