Sio kila hela kubwa unayopata ujengee au ufanyie biashara nyingine kula Bata ila kumbuka kununua mashamba bado utaonekana mjanja tu

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,945
45,919
Kama unajijua huna madeal ya million 50 huko na unajinyima kisa tu ujenge nyumba kali kama unazoziona za wengine za million 200 eti udundulize kila hela unayopata unakuwa Mpaka mchoyo kila pesa unaielekeza kwenye mjumba. Huku bado unaishi maisha ya shida ukiendelea kujisifu nyumba imekukula million 80 na bado inadai finishing.

Me kuna mzee wangu yeye kipindi ana nguvu za kazi madeal yake akipata million tano, nne anakula Bata hawazi Sema yeye alikuwa hanywi pombe ila wanawake sana so anachofanya ile million moja anaenda kununua Shamba anapanda mikorosho anatulia..

Hivyo hivyo anakuja kustaafu ana mashamba zaidi ya 20 sehemu tofauti tofauti kapanda minazi, korosho, miembe, migomba n. K.

Hakunaga mwenye kutaka kwenda nyumbani kwake watu wako interested kwenda kuona mashamba yake..

Point yangu ni kwamba Kama unajijua hauko katika network ya kushika hela zaidi ya million 10 Kwa Mara moja Mara Kwa Mara basi achana na mambo za kujenga mijumba mikubwa utafika umechoka sana heri uendelee kukaa sehemu ya kawaida ila ununue mashamba kila mwaka mashamba hata manne mazuri una panda vya kupanda.

Nimetolea case study ya minazi na korosho Kwa sababu niko kusini ila ukiwa huko ulipo yako mazao ya muda mrefu ya matunda sio mbaya utakuja kuwa hauishiwi hela ila nyumba kubwa zuri hailingizi chochote.

Ni heri ulijenge mwishoni hapo umeuza korosho zako au baadhi ya mashamba yako.
 
Umeongea point kuna muda nilikuwa najibana ili kujenga ile nimehamia nikagundua hakuna jipya baada ya miaka tano wenzangu wakashusha majengo mengine ya kisasa nikaamua kuuza nyumba yenyewe nikanunua mashamba saiv kila baada ya mwaka ninauwezo wa kujenga popote tz kupitia yale yale mashamba mana nilinunua mashamba ya umwagiliaji kama hekar 50 hv kila miez tano nimefeli sana naweza vuna mazao yasiopungua milion 22 faida je ningebaki na nyumba ningeweza shika pesa hiyo? kuna jamaa yangu ye anajenga na kuuza akipata hela anajenga tena anauza
 
Back
Top Bottom