Simulizi ya kipelelezi: Jiji la kamari (gambling city)

HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 34
“Kazi imefikia wapi?”
“Sumu tayari ipo ya kutosha na ishapakiwa tayari”
“Inafanya kazi kama tulivyo kubaliana?”
“Ndiyo kiongozi” mwanasayansi mkuu alikuwa anajibu kwa hofu sana.
“Unajua kabisa kama ukiniletea uhuni ni kitu gani nitakifanya kwa familia yako”
“Ndiyo ndiyo naelewa ndiyo maana nipo makini sana na kazi”
“Huwa siwezi kumuamini mtu kwa maneno tu”
“Unamaanisha nini?”
“Tunatakiwa kupata mtu wa kuweza kuijaribu”
“Unataka niwaue watu ambao hawana hatia kwa sumu?”

“Kwani wewe unahisi hiyo sumu inatumika kwenye nini? Na hao watu ambao hawana hatia kwahiyo familia yako ina hatia?”

“Nitafanya hivyo” mwanasayansi huyo aliongea kinyonge sana huku akimimina chai na kuweka tone moja tu la sumu ambayo ilikuwa kwenye kichupa kidogo kwnye mikono yake kisha akamuita mwanasayansi mmoja na kumpa ile chai ambapo mwanaume huyo alikuwa na wasiwasi sana lakini aliambiwa anywe.

Hakuwa na namna zaidi ya kufanya hivyo, baada ya kuinywa chai hiyo alianza kutetemeka, damu ikaanza kumtoka puani na masikioni na hakuchukua hata muda akaanza kukakamaa na kuakuka kabisa.
“Safi sana, wateja wetu wa nje wanaihitaji haraka sana. Ni sumu ambayo inauzwa bei ghali mno kwahiyo nina imani kwamba itatupatia mabilioni ya fedha, kazi nzuri dokta” alimpiga piga mgongoni na kutoka humo ndani dokta akiwa anakaa chini na kusikitika sana maana mambo ambayo yalikuwa yanaendelea yalikuwa yamevuka kwenye ubinadamu wa kawaida.


Wakati watu wanalalamika kwa baridi kali ambayo ilikuwa inaendelea ndani ya jiji la Dar es salaam kwa sababu ya hali ya mvua ambayo ilikuwepo, ilikuwa ni tofauti kabisa kwa watu wawili, watu ambao miili yao ilikuwa sehemu ya kuwapa burudani ambayo huenda watu wengi sana walikuwa wameikosa kabisa kwenye maisha yao. Max na Brandina walikuwa wanavinyoosha viungo vyao kitandani huku kila mmoja wao akiwa anamsifia mwenzake kwa namna alivyokuwa anajua kukitumia kiungo chake kuweza kumnyooshea mwenzake viungo vyake.

Mapenzi yao yalikuwa ya muda mfupi sana lakini walijikuta wanaanza kuaminiana kiasi kwamba mara nyingi walianza kulala pamoja na kazini wangewahi pamoja kisha wangeachana pamoja kwa sababu ilikuwa ni hatari sana kama wangejulikana kwamba walikuwa wamezama kwenye mapenzi kutokana na asili ya kazi yao hawakuwa wanatakiwa kabisa kuingia kwenye mapenzi kwa namna yoyote ile hata kwa bahati mbaya tu.

Mwanaume baada ya kutoka kitandani akiwa uchi, alikaa kwenye sofa ambalo lilikuwa karibu na kitanda huku akiwa anamwangalia mrembo Brandina naye akiwa uchi kabisa kwenye mwili wake. Alikuwa anamkadiria mrembo huyo anashindwa kummaliza, licha ya kwamba alikuwa ameanza kumzoea sana na kumpenda kwenye moyo wake lakini alikuwa na wasiwasi naye kwani alikuwa amekuja kwa kasi sana na kazi yake haikumruhusu yeye kuweza kumwamini mtu yeyote yule na kwa namna yoyote ile.

“Unataka nini kwangu?” ndilo swali ambalo alimuuliza mwanamke huyo akiwa amemkazia macho. Mrembo huyo licha ya kushtuka sana kutokana na aina ya swali ambalo alikuwa ameulizwa ila hakutaka kuonyesha mshtuko huo kwani ungethibitisha kwamba alikuwa na jambo lake. Alijizoa zoa na kusogea kwenye kile kiti ambacho Max alikuwa ameketi, alimkalia na kuanza kumnyongea kiuno chake mithili ya feni iliyokuwa inaongezeka kasi sana mwisho wakajikuta wamezama tena kwa penzi zito sana.

“Mimi nahitaji msaada wako Max” lilikuwa ni jibu lake baada ya kumaliza shughuli nzito ambayo iliwaweka kitandani kwa muda huo.
“Msaada upi?”

“Unajua nimepewa nafasi kubwa sana ya kumlinda raisi wa nchi nikiwa kama mlinzi wake mkuu”
“Brandina hayo siyo mambo ya kuongelea hapa saivi ni hatari sana, achana kabisa na hayo mambo”
“Nadhani wewe umeniuliza kwamba ni kwanini nimekuja kweye maisha yako”
“Sasa suala la raisi linatokea wapi?”

“Ndiyo sehemu hasa ambayo nahitaji msaada wako Max kwani nipo hatarini sana kuuawa”
“Whaaaat?”
“Ndiyo”

“Nani anataka kukuua?”
“Unamwamini mkurugenzi wa shirika letu”
“Brandina, what are you talking about?”

“Niligoma kufanya kazi yake Max, sijajua nyuma yake kuna nani na nani ila yule ni mtu hatari sana”
“Umeyajuaje haya?”
“Kwa sababu alitaka mimi nimuue raisi”
“Whaaaaat?”

“Yeah Max, niliogopa sana na ukizingatia sina mtu hata mmoja upande wangu nimebaki na wasiwasi sana”
“Ilikuaje?”
“Alinipa maagizo tu kwamba natakiwa kumuua mheshimiwa raisi bila kuacha ushahidi”
“Na wewe ukamjibu nini?” Max aliuliza akiwa anazunguka humo ndani na kushika kichwa, alikuwa hajui kama kwenye huo mchezo hata mrembo huyo alikuwa ameingizwa, hilo kwake lilikuwa ni jambo la hatari sana.

“Nilimwambia siwezi kuifanya hiyo kazi, siwezi kumsaliti raisi wa nchi yangu wala kulisaliti taifa langu kwa namna yoyote, ila aliniambia kwamba kama nikishindwa kufanya hivyo mimi ndiye natakiwa kufa. Naomba msaada wako Max” mwanamke huyo aliongea akiwa analia na kukaa chini akiwa bado uchi kabisa. Max alimsogelea na kumkumbatia kwa hisia sana, ilimuuma sana mrembo huyo kuingizwa kwenye michezo mibaya na ni wakati ambao alijihakikishia kwamba kweli mkurugenzi huyo alikuwa msaliti kama ambavyo raisi alimtahadharisha.
“Natakiwa kuongea na raisi hili jambo”
“Hapana Max usifanye hilo kosa”
“Kwanini?”

“Kwa sababu raisi atapaniki na mchezo wote unaweza ukaharibika, mimi nimekushirikisha wewe kwa sababu nimeona ndiye mtu pekee ambaye naweza kumwamini”
“Unahitaji nini?”

“Nataka unisaidie hawa watu na huu umoja wao tuweze kuupoteza na kuupoteza inatakiwa tufanye kazi bila wao kuwa na taarifa kwamba sisi tunawatafuta”
“Siwezi kukaa kimya nitakuweka kwenye hatari kubwa sana B”

“Hatuna namna Max naomba tu kujua kama unaweza kuwa na mimi kwenye hii safari maana kama tukiwaacha hawa watu wananchi wa taifa hili watateseka sana”
“Kwani kuna mengine unayajua zaidi ya haya?”
“Ndiyo”
“Unaweza kuniambia?”

“Baada ya kufuatilia kwa umakini sana nimekuja kugundua kwamba kumbe raisi mstaafu ni miongoni mwa watu ambao wapo nyuma ya haya mambo yote ambayo yanatokea na huenda ndiye yupo nyuma ya mkurugenzi”
“Una muda gani tangu umeyajua haya?”
“Siku tano sasa. Max mbona hata haushtuki kwamba unayajua haya?” Max alihema kwa nguvu sana na kuchungulia nje hakuona mtu yeyote yule.
“Yeah”
“Whaaaat?”

“Najua kila kitu Brandina”
“Niambie kwamba unanitania sio?”
“Hapana, sina utani na wewe”
“Why unajua na haufanyi jambo lolote?”

“Brandina haya mambo ni magumu sana kuliko unavyo fikiria wewe, ni watu wazito sana ambao unashauri kuingia nao kwenye vita na tangu ulipo amua kupambana nao basi maisha yako yapo hatarini sana”
“Kipi kinaendelea Max?”
“Naweza kukuamini B?”

34 naweka nukta hapa.

Tchao
Nakubali kiongozi. Upo makini sana
 
Huyu mwandishi hana maajabu tena kwa mwendo huu maybe story yake ni ya kukopi sehem then anatuma huku au hawa ndiyo wale akina mtibeli ambao hawamalizagi story au sifa zimemlevya au hana bando la kuja huku au yuko busy sna au hana lolote ..... Na mia na yule jamaa singanojr huyu jamaa atawadanganya lakini lazima atume huyu naye sasa......
 
Huyu mwandishi hana maajabu tena kwa mwendo huu maybe story yake ni ya kukopi sehem then anatuma huku au hawa ndiyo wale akina mtibeli ambao hawamalizagi story au sifa zimemlevya au hana bando la kuja huku au yuko busy sna au hana lolote ..... Na mia na yule jamaa singanojr huyu jamaa atawadanganya lakini lazima atume huyu naye sasa......
Sawa mkuu.
 
Mkuu kumbe upo kabisa,,,, kwanza nakusalimu kwa jina la zakaria mansour..... Weka ata kipisi mkuu tutulize arosto
Hahaha 😂 😂 😂 ulivyopoa Sasa
Mchangie mwamba bwana umalizie story buku 2 sio kitu boss
 
Hii hadithi alihamishia Facebook naona na kule kasitisha 🤔
 
Good morning.

Ni muda kidogo tangu niposti simulizi humu. Nimeona wengi wakidhihaki mara unasubiri waandike ndipo ucopy (unajua kabisa hii ni hoja ya mtu ambaye kala ugali kashiba kichwani kinakuja chochote kile naye anakwenda nacho hivyo watu wa namna hii huwa nawapuuza maana sometime sio wao ni mihemko tu) wengine wakilaumu na wengine wakitoa ushauri.

Siku zote huwa napenda kuwa positive hivyo no hard feelings..... Sitaeleza sababu za moja kwa moja ambazo zilifanya nikastop kuja kuendelea kupost humu kwa sababu zina mjumuiko wa sababu za kifamilia na sababu binafsi ambazo zilinikumba na kwa vile wengi walijudge before kuuliza basi wanatakiwa kubaki na hizo judgement zao kama zilivyo ila ukiona kila kitu kinanyooka kwako shukuru Mungu
tu kuna misala mingi inawatokea watu na sio lazima mtu aje akuhadithie wewe.


Kwa sasa kiasi chake nipo sawa hivyo hii simulizi nitaimaliza hapa hapa na kesho nitaitambulisha simulizi mpya "BADO NINAISHI (ASHRAFU NDILO JINA LANGU) hivyo zitakuwa zinakuja zote mbili.


Kama unajiona unapenda kutukana au ndiyo Hobby yako basi unaweza kwenda jukwaa na mahusiano ukamalizia hasira zako kwa wale ambao wanafanya maamuzi ya kipuuzi kwenye mapenzi ila sitapenda kuona matusi hapa (kosoa uwezavyo ni sawa ila sio matusi). Ukiona huwezi kuvumilia bila kutukana basi unaweza ukaachana na uzi tu ili baadae usianze kutafuta sababu za kutukana watu (Ustaarabu)

Siku njema kwenu.
 
Good morning.

Ni muda kidogo tangu niposti simulizi humu. Nimeona wengi wakidhihaki mara unasubiri waandike ndipo ucopy (unajua kabisa hii ni hoja ya mtu ambaye kala ugali kashiba kichwani kinakuja chochote kile naye anakwenda nacho hivyo watu wa namna hii huwa nawapuuza maana sometime sio wao ni mihemko tu) wengine wakilaumu na wengine wakitoa ushauri.

Siku zote huwa napenda kuwa positive hivyo no hard feelings..... Sitaeleza sababu za moja kwa moja ambazo zilifanya nikastop kuja kuendelea kupost humu kwa sababu zina mjumuiko wa sababu za kifamilia na sababu binafsi ambazo zilinikumba na kwa vile wengi walijudge before kuuliza basi wanatakiwa kubaki na hizo judgement zao kama zilivyo ila ukiona kila kitu kinanyooka kwako shukuru Mungu
tu kuna misala mingi inawatokea watu na sio lazima mtu aje akuhadithie wewe.


Kwa sasa kiasi chake nipo sawa hivyo hii simulizi nitaimaliza hapa hapa na kesho nitaitambulisha simulizi mpya "BADO NINAISHI (ASHRAFU NDILO JINA LANGU) hivyo zitakuwa zinakuja zote mbili.


Kama unajiona unapenda kutukana au ndiyo Hobby yako basi unaweza kwenda jukwaa na mahusiano ukamalizia hasira zako kwa wale ambao wanafanya maamuzi ya kipuuzi kwenye mapenzi ila sitapenda kuona matusi hapa (kosoa uwezavyo ni sawa ila sio matusi). Ukiona huwezi kuvumilia bila kutukana basi unaweza ukaachana na uzi tu ili baadae usianze kutafuta sababu za kutukana watu (Ustaarabu)

Siku njema kwenu.
Umeeleweka mkuu, karibu tena
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 35
“Ndiyo maana mimi nimekwambia kila ambacho nakijua kwa sababu nakuamini kama isingekuwa hivyo nisingekwambia mambo ya hatari sana kwangu kama haya ambayo yanahatarisha maisha yangu”
“Denis Kijazo anatakiwa kuuawa”
“Sijakuelewa”

“Siko pekeyangu katika hili. Kuna baadhi ya watu ambao wanahitaji afe hivyo tutamuua”
“Unamaanisha na nani?”
“Ni ngumu sana kukuambia B”
“Kwahiyo mimi nimejipendekeza sana kwako kuja kukwambia haya sio”
“Raisi”

“Whaaat? Raisi ndiye yupo nyuma ya hili?”
“Kwa sasa ndiyo”
“Kwa sasa? Ukiwa na maana gani?”
“Unamkumbuka Francis Mboye?”
“Ndiyo alikuwa kiongozi shupavu sana ambaye alikufa kwa tamaa za watu wachache, Mungu amlaze mahala pema peponi mzee wa watu”

“Yule ndiye alikuwa kiongozi wa huu mpango wa kuweza kumuua Denis Kijazo lakini aliamua kujitoa sadaka ili kuhakikisha raisi anakuwa hai maana ndiye alitakiwa kuwa kiongozi wa haya hata yeye asipokuwepo”
“Unamaanisha Denis Kijazo ndiye ambaye alimuua mkuu wa majeshi?”

“Ndiyo lakini hakufa kizembe aliacha kila kitu kikiwa kwenye njia yake na watu ambao watatusaidia katika hili”
“Unataka kuniambia kwamba kuna watu wengine tena?”

“Hiii sio kazi rahisi sana, ni kazi ambayo inahitaji watu wanaoweza kujitolea kwa kila namna na kupambana hivyo hata maandalizi yake yalikuwa ya muda mrefu sana”
“Ni akina nani?”

“Mpaka sasa siwajui bado ila nilifanikiwa kuwaona mara moja wakati nafanya mauaji kule kwenye ukumbi wa Denis Kijazo”
“Unataka kuniambia wewe ndiye ambaye uliulipua ule ukumbi?”
“Yeah”
“Raisi alikuagiza?”
“Yes”

“Na hao watu walikuacha tu au mnafahamiana?”
“Na wao walikuwa wamefika pale kufanya kama nilichokuwa nimekifanya ni kwa sababu tu niliwawahi kufika pale ila hata nisingeenda bado lile jengo lingeteketea”
“Kwa hiyo kwa sasa nini kinafuata?”
“Nasubiri amri ya raisi nadhani anaweza kunikutanisha na hao watu”

“Namshukur Mungu nimepata watu sahihi kwa sababu taifa la kizazi kijacho lilikuwa linateketea kabisa. Naomba usije ukaniangusha Max, kwa pamoja tusaidiane kuijenga Tanzania iliyo bora, sijutii kukufahamu wewe, nikihitajika kwa chochote kile naomba usisite kuniambia muda wowote ule na hao watu naomba unikutanishe nao siku ambayo utaona inafaa kufanya hivyo”
“You are welcome”
“I love you Max”

“Love you too baby girl” walijikuta wanazama tena kwenye mapenzi baada ya mazungumzo marefu ya kutishia amani ya taifa lao. Mapenzi ni upofu kama baadhi ya tamathali zielezavyo hatimaye yalitimia kwa Max, mwanaume wa kazi, mwanaume ambaye ndiye alikuwa mtu wa mhimu zaidi kwenye kuikamilisha kazi nzito ambayo ilikuwa mbele yao na ndiye yeye mwnyewe ambaye alitoboa siri kirahisi sana kwa Brandina juu ya mipango yao yote.

Akili kubwa sana ambayo aliitumia Brandina ni kumchota imani mwanaume huyo, kwa taarifa ambazo alipewa ni kwamba raisi alikuwa anajua kuhusu mkurugenzi lakini hata mtu ambaye walikuwa wanaamini kwamba anamfuatilia mkurugenzi walikuwa wana uhakika kwamba hakuwa mwingine bali Max hivyo kama alikuwa anamfuatilia maana yake ni kwamba alikuwa ana taarifa nyingi sana za kiongozi huyo na kama ilikuwa ni hivyo basi walikuwa wanatakiwa kuitumia nafasi hiyo hiyo kuweza kumkamata mwaume huyo vizuri.

Brandina alimweleza mambo ya kweli kabisa ambayo Max alikuwa ameambiwa, alipewa taarifa kuhusu watu hao kutaka kumtumia B kumuua mheshimiwa raisi na mwanamke huyo akaapa kwamba hakuwa tayari kwa hilo ndiyo maana alikuwa anahitaji msaada na mtu pekee ambaye alikuwa anaweza kumuamini, alikuwa ni Max tu pekee. Hilo lilimpa uhakika kwamba mwanamke huyo alikuwa msafi kwani kama angekuwa anatunga huo ukweli asingefanikiwa kuwa na ukweli wa mambo yote ambayo yalikuwa yanaendelea lakini Max hakujua kwamba alifanya kosa kubwa zaidi kwenye maisha yake na kosa hilo lilikuwa linaenda kuwaponza na wengine ambao hawakuwa wamejua kwamba amefanya huo ujinga.

Wakati wanayafanya hayo maongezo yao, kwenye kifungo kimoja cha shati ya Brandina kulikuwa na kifaa cha mawasiliano cha kunasa sauti, kifaa hicho kilikuwa kimefichwa ndani ya kifungo hicho huku kifungo kikiwa kimetobolewa kwa mbali sana sehemu ambayo ilikuwa inasaidia kupitisha sauti. Upande wa mbali kidogo na jengo hilo alikuwepo Dax kwenye gari akisikiliza maongezi hayo lakini pia mkurugenzi Philipo Tibaigana alikuwa ofisini kwake akiwa anaisikia vyema kabisa hiyo sauti kisha alicheka sana maongezi hayo yalipo ishia.

“Hahahah hahaha wanawake wengi ni wapuuzi sana, huwa wanashindwa kujua nguvu kubwa ya kile kitu ambacho kipo katikati ya miguu yao. Hakuna mwanaume rijali anaweza kulikwepa hili hususani unapokuwa unamtumia mwanamke mrembo kama yule” alikuwa na furaha sana wakati huo aliichukua simu yake na kupiga mahali.

“Boss deal done. Kilichobaki kwa sasa ni kuwajua watu wachache sana”
“Umefikia wapi?”

“Nilikwambia yule binti ataifanya kazi kwa muda mfupi sana, nakutumia maongezi yao saivi lakini kwa sasa watu wa kudili nao ni waziri mkuu na makamu wa raisi. Hawa hakikisha wanakuwa upande wako kisha baada ya hapo hao watu wakifika tunabaki tumebakisha hatua moja tu kuwajua watu kadhaa kisha raisi atakufa na bwanamdogo kesi inabaki kwake”

“Safi, nitumie haraka sana vijana wanafika muda wowote” simu ikakatwa huku wakiwa kwenye furaha kubwa sana maana ulishindi ulikuwa unakuja upande wao. Kitu pekee ambacho kilikuwa kinawaumiza sana ilikuwa ni kuwajua watu ambao walikuwa nyuma ya raisi lakini mpaka wakati huo ilionekana kwamba ilibakia kidogo tu waweze kuwapata watu hao kupitia Brandina ambaye walijua kwamba kwa wakati huo Max alikuwa amesha muamini hivyo angeanza kumwambia siri zake nyingi sana.


Raisi alikuwa ndani ya ofisi yake majira ya asubuhi akiwa mwingi wa mawzo, kwa wakati huo kitu ambacho kilikuwa kinampa sana mawazo haikuwa kwa sababu ya kazi ngumu sana ambayo ilikuwa mbele yake bali ni mtu ambaye alikuwa amekutana naye. Piusi ni mwanaume ambaye aliwahi kukutana naye miaka ya nyuma na mwanaume huyo akampenda sana na kuahidi kuwa naye kwa namna yoyote ile japo alikuwa chini ya Denis Kijazo.

Kwa miaka mingi sana alikuwa anajua kwamba mwanaume huyo alikuwa amekufa lakini haikuwa hivyo, mtu huyo alikuwa mzima kabisa tena wa afya tele jambo ambalo lilimchanganya sana. Hakuwa Piusi kama alivyokuwa amejitambulisha kwake bali jina lake alikuwa anaitwa Bilali tena alikuwa ni miongoni mwa makomando wakubwa sana kuwahi kutokea kwenye historia ya taifa la Tanzania. Alikuwa anawaza sana kwamba hilo jambo lilikuwa linawezekana vipi yeye kuweza kudanganywa kwa miaka yote kumi akiwa anaamini kwamba mtu huyo alikuwa amekufa huku akiwa anaishi? Ilikuwa imamuuma sana mwanamke huyo ambaye alikuwa na kazi nzito sana na mwanaume huyo ndiye ambaye alipaswa kumsaidia kwenye harakati zake ambazo aliachiwa na Francis Mboye.

Akiwa anaendelea kutoa machozi yake, machozi yalikuwa yanamshuka kwenye uso wake na ndio wakati ambao mlango ulifunguliwa, akaingia Max kama alivyokuwa ameagizwa na kiongozi huyo. alishangaa sana kukuta raisi anajifuta machozi kwenye uso wake hivyo akataka kutoka maana isingekuwa heshima kuongea na raisi akiwa kwenye hali kama hiyo.

“Usijali unaweza kuketi”
“Mheshimiwa sidhani kama upo kwenye hali nzuri ya kuongea japo sijajua ni kipi ambacho kilikuwa kinakusumbua”
“Mhhhh, umewahi kupenda kwenye maisha yako?”
“Hapana mheshimiwa”
“Kwanini?”

“Kwa sababu sijawahi kuwa mwanadamu mwenye furaha kabisa kwenye maisha yangu nadhani ndiyo sababu sijawahi kumpenda mtu yeyote”
“Mshukuru sana Mungu kuweza kukuepusha na hayo mambo maana yanaweza kuyaharibu hata maisha yako kama ukienda nayo vibaya”

“Asante sana mheshimiwa” alikuwa anajibu huku nafsi yake ikiwa inamsuta maana alikuwa ameshaanza kuzama tayari kwa Brandina.
“Leo kuna mtu nahitaji ukutane naye, huyo mtu ndiye ambaye atakuwa msaada mkubwa sana kwetu kuweza kuifanya kazi hii”

35 niseme basi.

Tchao
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 36
“Sawa mheshimiwa, wapi?”
“Kariakoo. Nenda saa saba na nusu usiku na kuna location ambayo nitakutumia, utaifuata hiyo mpaka itakapokupeleka basi ndipo hapo ambapo utatakiwa kukutana naye japo unapaswa kuwa makini sana maana unaweza ukawa unafuatiliwa bila wewe kujua, jukumu la kuyalinda maisha yako lipo juu yako kama unavyojua nakuhitaji sana kwenye hili”

“Siwezi kukuangusha mheshimiwa” mwanaume alikuwa anapewa ni maagizo tu kisha akatoka ndani ya ofisi hiyo lakini wakati anatoka alikutana na Dax akiwa amemkazia macho sana.
“Max what kind of game are you playing?”
“Last card”
“Unamaanisha kwamba you are the last one”

“KAMALI YANGU YA MWISHO NDIYO KAMALI YAKO YA KWANZA. So, play it if you like it” ni kauli ambayo aliitamka kwa msisitizo mkali sana ambayo ilibaki kwenye kichwa cha Dax wakati yeye akiwa anatoweka hapo maana hakuonekana kabisa kuwa mtu wa kukaa tena Ikulu, alikuwa na tripu zisizo eleweka lakini Dax aliishia kutabasamu tu maana mtu huyo walikuwa wamemuweka mfukoni bila yeye kuweza kutambua.


Upande wa pili Bilali alikuwa amejifungia ndani ya chumba chake mwenyewe, alikuwa ameketi kwenye sofa akiwa na mawazo sana, mawazo ambayo yalimrudisha mbali sana kwenye historia ya nyuma kabisa ya maisha yake. Mwanaume huyo historia yake ilianzia huko Kilombero Morogoro kwenye mashamba ya miwa, huko ndiko ambako yeye alizaliwa, huko ndiko ambako yeye alikuwa anapaita kwao lakini hiyo ilikuwa ni zamani sana. Kwa wakati ambao alikuwa anayakumbuka maisha yake ya huko nyuma alikuwa anaogopa hata kwenda kwenye eneo hilo tena maana alikuwa na kumbukumbu mbaya sana juu ya eneo hilo.

Alizaliwa akiwa na kipaji cha mpira ambacho aliamini kwamba angekiendeleza kutokana na asili ya mkoa wa Morogoro kuzalisha vipaji vingi sana vya mpira. Mpira ulimfanya awe mvivu sana shuleni kitu ambacho kiliwakera sana wazazi wake hususani baba yake ambaye alikuwa ni mwanajeshi. Kutokana na sababu kwamba baba yake alikuwa akirudi mara moja moja sana ilimpa nafasi kubwa Bilali kutoitaka shule na mama yake alikuwa anampenda sana alishindwa kuweza kumlazimisha kusoma hivyo muda mwingi sana akawa anautumia kwenye mpira ambao aliamini kwamba ungemtoa kwenye maisha yake.

Siku moja alipata bahati ya kusafiri na timu yake ya mpira kwenda nje ya mkoa lakini akiwa huko simu ilipigwa kwa kocha wake kwamba alitakiwa kurudi nyumbani haraka sana na kwa msaada wa kocha huyo alifanikiwa kupata usafiri binafsi ambao ulimfanya ndani ya msaa sita tu afike nyumbani kwao. Baada ya kufika nyumbani hakuamini kile ambacho alikuwa anakiona nyumba yao ilikuwa inawaka moto mkali sana kiasi kwamba hata yeye alichanganyikiwa akiwa anaangulia kilio kizito sana.

Jambo ambalo lilimshangaza sana ni kwamba ilikuwaje mpaka simu ikapigwa kwamba nyumbani kuna tatizo halafu muda wote huo akute moto unawaka tangu akiwa Dar es salaam mpaka anarudi huko kwao? Ni swali ambalo hakuwa na majibu yake kwa wakati huo. Alitamani sana kama angefanikiwa kuingia kwenye moto huo baada ya kuambiwa kwamba familia yake ilikuwa inateketea humo lakini alizuiwa na watu ambao walikuwa karibu kabisa na eneo hilo.

Kutokana na gari za zimamoto kuwa mbali sana na eneo ambalo walikuwa wanaishi hakuna kitu hata kimoja ambacho walikiokoa vikaishia kuteketea vyote na kumfanya asibakiwe na chochote kwenye maisha yake. Maisha kwake yalikuwa magumu sana hasa baada ya serikali kugoma kabisa kumpatia kiinua mgongo cha baba yake ambaye alilitumikia jeshi kwa uzalendo mkubwa sana, hilo kwake halikuwa swala la mhimu sana swali ambalo alikuwa anajiuliza ni kwamba kama baba yake alikuwepo kivipi alifia ndani na familia yake? Hilo lilimfanya kumfuata mzee mmoja ambaye alikuwa anaishi jirani jirani na eneo la nyumbani kwao. Mzee huyo alimpa taarifa kwamba yeye ndiye aliyepiga simu ya kumhitaji yeye arudi nyumbani baada ya kuona baba yake amerudi ghafla, mzee huyo alimhakikishia kwamba alijua kwamba mzee huyo angempiga vibaya sana ndiyo maana aliamua kutoa taarifa kwa mwalimu wake kwamba kuna tatizo nyumbani ili arudi haraka sana.

Bilali alishangazwa sana na maelezo ya mzee huyo lakini mzee huyo alimwambia kwamba akiwa hapo kwake aliona kuna msafara wa magari unapaki kwa mbali huku wakishuka wanaume ambao walikuwa kwenye mavazi ya jeshi. Alimweleza kwamba baba yake alitoka kuweza kuongea na watu wale lakini baada ya muda mfupi aliona baba yake akipigwa vibaya sana na mwanaume mmoja ambaye alikuwa mbele yake na baada ya hapo alibebwa na kutupwa ndani ambapo milango yote ilifungwa na wanaume wale walitia moto mkubwa sana kwenye ile nyumba huku kila mtu ambaye alikuwa anaishi jirani akianza kuondoka na kwenda mbali.

Wanaume wale hawakukaa tena eneo lile waliondoka haraka sana na gari zao na haikuchukua muda sana ndipo Bilali akawa anarudi nyumbani na kuikuta ile hali. Kwa sababu baba yake mzazi aliutumia muda mwingi sana kufanyia kazi ndani ya jiji la Dar hata majivu yake na familia yake yalichukuliwa kwa msaada mkubwa wa vipimo vya DNA na kupelekwa Dar es salaam ambapo yalizikwa kwenye makaburi ya Sinza.

Mwanaume alichukia sana na kuapa kwamba angemtafuta mhusika wa jambo hilo kama sio wahusika lakini mzee huyo alimuonya sana kwamba hayo mambo hakuwa akiyaweza hivyo alitakiwa kuyaacha kama yalivyo tu maana yangemletea matatizo makubwa sana kwa hapo baadae lakini hakuwa tayari kufanya hivyo na ndipo mzee huyo alishauri aende jeshini lakini hakuona kama wazo hilo lilikuwa ni zuri sana kwa upande wake bali aliona kwamba alitakiwa kutafuta pesa kwa jasho sana ili aje kuwasaka watu hao atakapokuwa na uwezo mkubwa kifedha.

Hali hiyo ikaleta safari yake ya kwanza kabisa kwenda kwenye mashamba ya miwa huko kutafuta vibarua na kufanya kazi kwa bidii sana mpaka siku moja alipopata ugeni kutoka kwa mwanaume aliyefahamika kwa jina la Francis Mboye. Huyo alimchukua kutoka kwenye mashamba hayo ya miwa baada ya kumwambia aliguswa sana na kifo cha baba yake ambaye aliwahi kufahamiana naye huko nyuma. Mzee huyo alimwambia kwamba alitaka kumpeleka jeshini kisha amfanye kuwa mwanaume wa shoka sana ili baadae aje kuwalinda raia wasije kukutana na na mambo kama ambayo alifanyiwa baba yake mzazi na huo ukawa mwanzo wake wa kwenda jeshini ambako alikuja kukutanishwa na wenzake wawili ambao kwa pamoja wakaja kuunda kundi hatari sana la DRAGON BOYS.

Mwanaume alitoka kwenye mawazo hayo ya kuiwaza familia yake akiwa na maumivu makali sana. Aliisogeza kumpyuta yake ya mkononi na kuyarudia tena maelezo ambayo yalikuwa yameandikwa hapo pamoja na sauti ambazo zilikuwa zimerekodiwa hapo akairuhusu sauti moja ili aisikie tena kwa mara nyingine. Sauti hiyo ilikuwa ya Francis Mboye akiwa anakiri na kuomba sana msamaha kwamba yeye ndiye ambaye alitoa amri baba yake Bilali aweze kuuawa.

Alieleza kwamba alifanya hivyo baada ya kupata maelezo kutoka ngazi za juu ambako wakubwa walikuwa wametoa taarifa kwamba mwanajeshi huyo alitakiwa kuuawa ka sababu alikuwa ni hatari sana kwa usalama wa taifa kwa kuiba nyaraka mhimu sana ndani ya jeshi pamoja na kuiba silaha zaidi ya miamoja ambayo ilikuwa ni ishara ya kuweza kuliasi jeshi hivyo amri moja kwa moja ilitoka kwamba auawe na sio kukamatwa kama ilivyo kawaida.

Mzee huyo alisisitiza kwamba hayo yote aliyafanya kwa sababu hakuwa na namna ya kuweza kupinga amri za viongozi wake na hakujua kama watu ambao aliwatuma wangeenda kuiteketeza familia nzima kwa sababu aliyekuwa anatakiwa kufa alikuwa ni baba yake Bilali tu mzee Rikardo lakini kwa bahati mbaya sana watu hao waliua familia nzima na yeye alikuwa amekubali kubeba lawama zote kwa maana alikuwa ndiye kiongozi wa oparesheni hiyo na alitakiwa kwenda moja kwa moja kwenye eneo la tukio huenda yasingetokea yote hayo.

Baadae alipokuja kugundua kwamba watu wale walifanya makosa kufanya maamuzi ya vile alitamani kumtafuta mwanafamilia yeyote ambaye alikuwa hai ili angalau apate nafasi ya kumuomba msamaha kwa yote ambayo alikuwa ameyasababisha lakini hakuwahi kuipata hiyo nafasi mpaka siku ambayo alisikia kwamba mtoto mmoja wa familia hiyo alikuwa anaishi na kufanya kazi huko kwenye mashamba ya miwa. Ndiyo sababu ambayo ilimfanya amtafute Bilali kwa namna yoyote ile na kumwendeleza ambapo alimfanya kama mtoto wake wa kumzaa lakini alimtengeneza mwanaume huyo ili kuja kulinda amani kwa kuhofia kwamba huenda kuna siku naye atatengenezewa mtego kama wa baba yake Bilali na akakosa kumuacha mtu wa kulinda maslahi ya watu wengine.

Alisisitiza sana kwamba makosa yake hayakutakiwa kutumika kuwaadhibia watu wengine kwa maana hawakuwa na hatia yoyote ile na alikuwa anamuomba sana mwanaume huyo aweze kumsamehe sana hilo kosa ambalo alilifanya na aliamini lingemtafuna hata akiwa kaburini. Lakini baada ya hayo maagizo alimhakikishia Bilali kwamba alikuwa na familia ya watoto wa wawili na mke ambayo ilikuwa ikipatikana eneo la Masaki na mkewe alimfukuza nyumbani baada ya kuhisi kwamba mzee huyo ana wanawake wengine kutokana na kukosekana nyumbani pale ambapo familia ilikuwa inamhitaji kila mara. Hivyo alimuomba mwanaume huyo kwamba kama akija kumsamehe basi siku hata moja aende kuijulia familia yake hali na mali ambazo aliziacha kwa Bilali aliamini kwamba anastahili kwa sababu yeye ndiye ambaye aliiteketeza familia ya kijana huyo.

Mwanaume baada ya kumaliza kusikiliza sauti hiyo aliishia kutoa machozi tu maana bado alikuwa na hasira sana kwenye moyo wake. Aliangalia saa ilikuwa inasoma saa sita na nusu usiku, ulikuwa ni wakati wa kwenda kukutana na mtu wake, aliingia ndani ya suti na kutoweka hilo eneo ambalo alikuwepo yeye na wenzake.

Justin Mtadei ambaye mwanzo alikuwa ni DCI lakini mheshimiwa alimteua kuwa waziri mkuu, asubuhi na mapema sana alikuw aamewahi ndani ya ofisi yake ili kuweza kuianza kazi yake maana ndiyo ilikuwa siku yake ya kwanza kabisa kuingia ofisini tangu aapishwe hivyo alitakiwa kufanya kazi kwa bidi sana na kuhakikisha kila kitu anakiweka sawa. Akiwa ndani ya ofisi hiyo, alipokea ugeni mzito sana asubuhi hiyo hiyo ambao hata yeye mwenyewe ulimshtua sana maana hakutegemea juu ya jambo kama hilo kuweza kufanyika.

Denis Kijazo alikuwa amefika mwenyewe ofisini kwa mtu huyo na kuomba kukutana naye, alikuwa ni mtu mkubwa sana ndani ya taifa ambaye hakuwa na uwezo wa kuweza kumkatalia jambo kama hilo ingeonekana kuwa dharau kubwa sana kwa upande wake.

36 inafika tamati.

Tchao.
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 37
“Mheshimiwa imekuwa ni ghafla sana, sikutegemea kwamba mtu kama mimi naweza kutembelewa na wewe”
“Ushakuwa waziri mkuu wa nchi sasa kwanini haujiamini?”
“Niseme ni fahari sana kwangu kutembelewa na wewe”
“Upo upande gani bwana Mtadei?”

“Unamaanisha nini?”
“Usijifanye wewe ni mgeni sana wa hiki kinacho fanyika”
“Bado sijakuelewa, unaweza kwenda kwenye pointi yako moja kwa moja?”
“Nimekuuliza umechagua upande gani wa kuichanga karata yako?”
“Mimi nalitumikia taifa na raisi wangu, sasa habari za kuchagua upande wa kwenda zinatokea wapi?”

“Hautamani siku moja kuingia Ikulu labda?”
“Whaaaat?”
“Wewe ni msomi mzuri sana acha kujifanya huelewi ninacho kisema”
“Sijawahi kuwaza kuwa raisi wa nchi hii”
“Then kwa sasa unaweza kuwa”

“Kivipi?”
“Unajua cha kufanya”
“Ooooh fu**k no”
“Niliwahi kukufuata kwa mara ya kwanza kwa kutuma watu wangu ukakataa kufanya kazi na mimi wakati mimi ndiye nilikuweka kwenye ile nafasi ya kuwa DCI, unajua kwanini sikukutoa?”

“Hapana labda ulivutiwa na utendaji wangu wa kazi”
“Nani anayejali utendaji wako wa kazi? Nobody gives a sh**t Justin”
“Unataka kumuua raisi wa nchi yako?”
“Yes”

“Siwezi kuruhusu wewe ukakamilisha hili na nitahakikisha hili jambo linafika mahali husika”
“Hivi unahisi kuja hapa nimekurupuka au nimekuja kukubembeleza?”
“Unaanza kunitisha sio?”

“Nina mpango wa kukufanya kuwa raisi wa nchi hii baada ya huyu changudoa kufa kwa sababu wewe ni mtu smart sana ila kama hautataka hilo basi nitaua familia yako yote kisha utakuwa wa mwisho”
“Nitakuua Denis, usije ukajaribu kuigusa familia yangu, naapa nitakuua kwa mikono yangu mwenyewe”

“Huu wakati ambao upo unanitisha hapa, piga simu nyumbani kwako” waziri mkuu alishtuka sana, ilikuwa ndiyo siku ya kwanza kabisa kazini lakini ilionekana kuanza vibaya sana kwa upande wake. Aliishika simu yake na kupiga simu nyumbani kwake. Simu ilipokelewa na mkewe akiwa analia, alidai kwamba mtoto wake wa mwisho wa kike ambaye waziri mkuu huyo alikuwa nampenda sana alikuwa anatoka damu puani na kutoa povu. Alimwangalia Denis Kijazo kwa hasira sana na kumpa taarifa mkewe kwamba angemrudia kwa dakika moja tu huku mwili wake ukiwa umejaa jasho.

“Wewe mshenzi, umemfanya nini mwanangu?” aliongea kwa hasira akiwa anamrukia na kumkwida Denis Kijazo shingoni akiwa na uchungu sana.
“Jinsi unavyozidi kupoteza muda wako ndivyo unazidi kuwa na nafasi ndogo zaidi ya kumuokoa mwanao”

“Tafadhali sana, nakuomba usimuue mwanangu” alibembeleza huku akiwa anapiga magoti.
“Sumu ambayo amepewa inaua kwa dakika thelathini na kwa sasa zimepita dakika kumi hivyo tuna dakika ishirini za kuongea kikubwa na kama dakika hizo zikiisha ikiwa bado umekaza kichwa chako basi utakuwa umemuua mwanao kwa mikono yako mwenyewe. Ameanza kutokwa na damu puani, kisha masikioni na mwisho wa siku ataanza kukakamaa na kukauka kabisa kama kakaushwa na umeme napo ni kwa sababu amewekewa kiasi kidogo sana cha sumu ila kama ingewekwa kubwa basi angekuwa amekufa mpaka sasa”

“Nani kafanya hili jambo Denis?”
“Nina watu kila sehemu ndugu yangu, pesa ni kitu kizuri sana lakini pesa ni kitu kibaya sana. Pesa inanunua imani ya mtu, pesa inawanunua watu na kuwabadilisha hivyo wanadamu wanaangalia mlipaji mkubwa ndiye wanamuabudu. Kwa hilo unahisi wafanyakazi wako na walinzi wako unaweza kuwafanya wajitoe hata kufa kwa ajili yako?”

“Unataka nini Denis?”
“Nahitaji uwe upande wangu. Nasikia kwamba leo jioni wewe unakutana na mheshimiwa raisi pamoja na makamu wa raisi ambaye naye ameianza kazi leo hii. Kwahiyo kitu ambacho nakitaka ni wewe kunipa taarifa zote ambazo zitaongelewa leo na mipango itakayokuwepo lakini kila siku utakuwa unanipa mrejesho wa kila kitu kinacho endelea ila tu zingatia usije ukanidanganya maana muda wote unafuatiliwa hata hapa ofisini kwako usipaamini sana kama nilivyokwambia kwamba mlipaji mkubwa ndiye ambaye anasikilizwa zaidi kuliko mtu yeyote yule”

“Baada ya hapo?”
“Kama ukitekeleza haya yote huyu malaya akifa basi Ikulu inabaki kwenye mikono yako”
“Na makamu wa raisi?”

“Bado sijaongea nae ila yeye nampigia simu saivi kama akigoma basi sitakuwa na muda wa kumbembeleza kwa sababu nilikuwa namhitaji mmoja tu kati yenu ila kama naye akigoma basi atakufa muda sio mrefu, nahitaji sierikali iwe na watu ambao wananisikiliza mimi hivyo kwa ambaye atahitaji kuwa kinyume na mimi basi lazima awahi kwanza kupumzika awaachie uwanja wanao jua namna sahihi ya kuzichanga karata zao bila wasiwasi”

“Mponyeshe mwanangu, nitafanya kama unavyotaka wewe”
“Sio ninavyotaka sema tunavyotaka kwa sababu kuanzia sasa mimi na wewe ni washirika lakini pia tutakuwa marafiki. Mbali na hilo ukiifanya kazi yako vizuri kila mwenzi utakuwa unaingiziwa mabilioni ya pesa kwenye akaunti yako ambayo nahitaji uniandikie hapo sasa hivi” mzee huyo aliongea akiwa anaitoa simu yake mfukoni na kutoa maagizo mtoto wa kiongozi huyo aweze kupewa dawa kwani mazungumzo yalienda vizuri. Wakati huo waziri mkuu alikuwa anamalizia kuandika akaunti namba yake kwa ajili ya pesa na baada ya hapo alipiga simu haraka sana nyumbani na kupewa majibu kwamba mwanae alipewa dawa na kurudi kwenye hali yake hata kazi alishindwa kufanya vizuri akaamua kurudi nyumbani kwa mwanae ambaye alimpenda sana.

Baada ya kumalizana na waziri mkuu mheshimiwa aliweza kutoweka ndani ya eneo hilo ili kuendelea na mipango mingine. Siku hiyo kazi alikuwa amepanga kuifanya yeye mwenyewe bila kutuma mtu hivyo safari yake ilikuwa ni kuelekea kwa makamu wa raisi ambaye naye hiyo ndiyo ilikuwa siku yake ya kwanza kabisa kuweza kuingia ofisini. Mheshimiwa Kasian Ndepo ambaye kwa mara ya kwanza alikuwa IGP.

“Mheshimiwa karibu sana”
“Nashukuru, nikupe hongera kwa kuweza kuanza majukumu mapya ambayo kwa sasa yanakufanya wewe kuwa mtu wa pili mwenye nguvu zaidi nchini”

“Nashukuru sana lakini pongezi za dhati kabisa nikupe wewe maana kama usingenipa ile nafasi ya kuwa IGP mpaka sasa nisingeonekana na kuweza kulitumikia taifa langu kwa moyo wote”

“Ni kawaida sana na ni jambo zuri mno pale ambapo unakuwa unakumbuka kule uliko toka”
“Nakujua vizuri sana mheshimiwa hauwezi kupoteza muda wako kuja hapa bila ishu ya mhimu, kuna kitu gani naweza kukusaidia?”

“Ni vyema sana kama umeanza kunijua sasa, ni kweli kama unavyo ongea wewe kwamba huwa sipotezi muda sehemu ambayo haina manufaa kwangu. Nipo hapa kwa kuhitaji kufanya kazi na wewe”

“Sijakuelewa”
“Usiwe na haraka utanielewa tu”

“Nakusikiliza mheshimiwa”
“Unaweza kuniambia kwamba mpaka sasa upo upande gani wa shilingi?”

“Unaweza ukaniweka kwenye lugha ya kawaida ili nikuelewe?”
“Nmaanisha kati ya raisi na mimi upo upande upi?”

“Mheshimiwa raisi wewe mwenyewe umemuweka madarakani halafu leo unaniuliza niko wapi wakati unajua kabisa kwamba nimekula kiapo cha kuitumikia serikali ambayo kiongozi wangu ni raisi mwenyewe? Hivyo moja kwa moja lazima nimchague yeye”

“Unamaanisha kwamba mimi unanikataa?”
“Wewe unataka nini?”

“Nataka ufanye kazi chini yangu”
“Hilo haliwezekani mheshimiwa”

37 nakomea hapa.

Tchao
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 38
“Sijaja kukuomba, hilo ndilo jambo la msingi ambalo unatakiwa kulizingatia”
“Hata mimi najua kwamba wewe huwa sio mtu wa kuweza kumuomba mtu kwa lolote”
“Na bado unaleta ubishi”

“Mzee nadhani ulishatoka kwenye mifumo ya serikali hivyo utakuwa unaheshimiwa kama mstaafu, kuna kitu gani hasa ambacho umekisahau huku mpaka unataka kutengeneza utimu na raisi?”
“Kwahiyo kupewa hiyo nafasi ya kuwa makamu umeanza kujiona kwamba taifa hili unalijua sana?”

“Sijasema kwamba nalijua ila huo ndio uhalisia, najua tangu mwanzo juu ya udhalimu wako na ushenzi ambao ulikuwa unaufanya na sikuwahi kupendezwa nao kabisa ikafika mahali nikawa natamani nipate mtu ambaye anaweza kupigana na wewe ili niungane naye niumalize huu ujinga wako na namshukuru Mungu raisi amejitoa kwa hilo hivyo nitamuunga mkono kwa asilimia miamoja. Kitu cha kukushauri ni kwamba achana na kila kitu na kisha kamuombe msamaha mheshimiwa raisi nina imani hili jambo litaisha mapema sana ila kama ukiwa mkaidi madhara yake yanaweza kuwa makubwa zaidi hata ya unavyo fikiria wewe” mheshimiwa alitabasamu na kusimama akiwa anazunguka ndani ya ofisi hiyo.

“Niliwahi kuwa na vijana wengi sana kama wewe ambao kwao ushupavu ulionekana kuwa sifa ya kutaka kusifiwa na wananchi, waliwahi kuwepo ambao walijiita wazalendo na kuamua kujitoa sadaka kuhitaji kuweka mashindano na mimi kama unavyo jigamba wewe hapa lakini unajua kwamba wako wapi hivi tunavyo ongea mimi na wewe? Hawawezi kuwepo, wengine walikufa na familia zao, wengine familia zao zilikufa kisha wao nikawaacha wakaishi, sasa kwa wewe hapo unahisi ni kipi kinaweza kukufaa kijana ambaye nimekuweka kwenye madaraka ya kuonekana mwenyewe?” aliongea kama utani ila alikuwa aamaanisha sana mheshimiwa huku akiwa anazikagua picha mpya za makamu ambazo zilikuwa zimewekwa siku hiyo ndani ya ofisi yake.

“Hakuna kitu ambacho unaweza ukanitisha nacho mr Denis, naomba pia utoke kwenye ofisi yangu kwa sasa nina kazi za kufanya sitaki huu upumbavu wako kuusikia tena”

“Hahaha hahaha hahah bwana mdogo wewe ndo unanikoromea mimi na kutaka kunitoa kwa nguvu kwenye ofisi yako? Hata raisi wako hana huo uwezo wa kufanya hivyo. Kwa sababu umegoma kwa njia ya amani basi sitakuwa na lawama hapo baadae, uwe na kazi njema” aliiangalia saa yake kisha akamsogelea makamu wa raisi na kusikitika huku akiwa anampiga piga mgongoni na kutoka ndani ya hiyo ofisi. Makamu alibaki amesimama tu asimmalize mtu huyo kwani alikuwa anaongea vitu ambavyo havikuwa vikieleweka kabisa kwa upande wake.


Usiku walikuwa wamekutana watu watatu kwenye chumba cha mikutano kuweza kuzungumza mambo mazito sana kuhusu taifa lao. Mheshimiwa raisi alikuwa amewaita makamu wake pamoja na mratibu mkuu wa shughuli zote za kiserikali ambaye alikuwa ni Justin Mtadei. Chumba kilikuwa kimya sana wote wawili wakiwa wanasubiri raisi aanze kuongea, aliwangalia kwa zamu zamu kwa muda kidogo kisha akaanza kuongea;

“Sababu kubwa ambayo imefanya mpaka leo mpo hapa ni kwa sababu nawaamini, siwezi kusema kwamba nawaamini kwa asilimia zote miamoja ila naweza kukiri kwamba nafsi yangu imeamua kuwaamini sana na ndiyo sababu kubwa ambayo imenifanya mimi kuwapa hizo nafasi kubwa ambazo nilikuwa naweza kumpatia mtu yeyote yule. Lengo la mimi kuwaweka hapo sio kwa sababu ya kunilinda mimi wala kuyalinda maslahi yangu binafsi, hapana bali kuyalinda maslahi ya watanzania ambao ndio wamiliki halali wa taifa hili.”

“Huenda nisieleweke kirahisi sana kwamba nataka tujilinde na nani ila kuna watu ambao walilifanya taifa hili kuwa lao, watu ambao walihisi kwamba hii nchi wanaweza kuigeuza kuwa chochote wanacho kitaka wao na wanadhani bado wataendelea kufanya hivyo lakini kwangu nimeona kwamba haya yanatosha kwa sasa. Tunataka taifa ambalo linakuwa na uhuru kwenye kila kitu kufanya mambo yake na sio watu fulani kukaa na kujiamulia juu ya nini ambacho kinatakiwa kufanyika”

“Mtu ambaye tunaenda kupambana naye ni Denis Kijazo ambaye ni mtanguluizi wangu, ni mtu ambaye mazingira mengi sana ameyaandaa kwa ajili yake na familia yake na ni mtu ambaye anahitaji taifa hili liwe la kwake na familia yake na marafiki zake ambao kwa muda mrefu sana kwa pamoja wamelitumia taifa hili kujichumia mali zao wenyewe bila kujali hali ya wananchi ipoje. Hivyo nyie ni watu ambao nimewaweka kwenye hizo nafasi ili kwa pamoja tuweze kupigana na kuwatoa watu hawa kwenye ramani ambazo walikuwa wamezichora. Nimeanza na kulipua jengo ambalo ndiyo yalikuwa makazi yao makuu ambayo walikuwa wanafanyia kila kitu” mheshimiwa alitulia baada ya kumaliza kuongea ambacho alikikusudia huku wanaume wawili wakiwa wanamsikiliza kwa umakini sana na hakuna hata mmoja ambaye alionyesha mshtuko juu ya alicho kiongea mpaka yeye mwenyewe alibaki ameduwaa.

“Mnajua kuhusu hili?” alilazimika kuwauliza watu hao. Makamu wa raisi alikohoa kidogo kujiweka sawa ili kumpa raisi kile ambacho alihisi kitakuwa sawa kwa wakati huo.
“Mimi nimetembelewa na Denis Kijazo mheshimiwa”
“Lini?”
“Leo”

“Alikuwa anataka nini kwako?”
“Alikuwa anahitaji nikusaliti wewe kisha niungane naye”
“Kuna ulazima wa mimi kujua upo upande gani?”

“Tangu siku ile nimekula kiapo basi damu yangu itamwagika nikiwa nalipigania taifa langu, nmemjibu waziwazi kwamba mimi siwezi kumpinga raisi wangu hivyo sina kitu ambacho ninaweza kumsaidia yeye. Licha ya kunipa vitisho vingi lakini mimi nilimruhusu yeye kufanya kile ambacho angeona kwamba kinampendeza”

“Amekupa kitisho gani?”
“Kuhusu familia mheshimiwa”
“Oooh shiiiit! Umewasiliana na familia yako?”

“Ndiyo wakati nakuja huku nilitoa nyumbani wapo salama na nimeimarisha sana ulinzi” makamu wa raisi aliongea kwa kujiamini sana lakini raisi alionekana akitikisa kichwa, alikuwa anamjua vizuri mtu huyo na namna alivyokuwa anawamiliki watu hivyo jambo la makamu kusema familia yake ilikuwa salama kwa sababu tu aliweka walinzi hakuwa sawa hata kidogo na huenda kama angelijua hilo basi angechukua tahadhari kubwa zaidi. Raisi hakutaka kumshtua, akamgeukia waziri mkuu
“Vipi kuhusu wewe?” waziri mkuu alitulia kwanza maana akili yake ni kama ilikuwa iko mbali sana.
“Anataka nikuue wewe”

“Umekubali juu ya kazi yake?”
“Ndiyo” makamu wa raisi alishangaa sana
“Whaaaaat?”

“Yeah, siku zote ukitaka kumkamata ndege usitumie nguvu, tafuta nafaka ambazo anazipenda yeye kisha utazitumia hizo kirahisi sana kuweza kuikamilisha kazi yako”
“Ukiwa unamaanisha kwamba?”

“Atahisi kwamba mimi nipo upande wake ila mimi ndiye naweza kutumika kumteketeza. Nilimkubalia nikiwa na mipango miwili kwanza kuhakikisha anacheza mbali na familia yangu ili kichwa kisiwe na mawazo ninapokuwa nafanya kazi lakini pia nilihitaji aniamini maana yake ni kwamba atakuwa ananialika mpaka kwenye baadhi ya kazi zake na hapo nitajua mambo yake mengi sana na nadhani tutakuwa na mwanzo mzuri sana wa kummaliza, hakuna mtu anaye mpenda yule mzee kwenye nchi hii labda vipofu ambao hawawezi kuona anayo yafanya”

“Safi sana, umetumia akili kubwa sana. Nadhani sikufanya makosa kuwaweka hapo japo ulikuwa ni ushauri wa meja jenerali Francis Mboye kabla hajafa”
“Anahusikaje kwenye hili?”

“Yule ndiye ambaye aliutengeneza huu mpango”
“Kwahiyo kuna watu wengine ambao tupo nao?”

“Ndiyo”
“Tunaweza kuwajua?”

“Tushakuwa washirika hivyo mtawajua. Wa kwanza ni Max, huyu ni mlinzi wangu wa kiume na wa pili ni Bilali na kundi lake ambalo wanaitwa DRAGON BOYS, hawa wote walikuwa ni vijana wa Francis Mboye na ni makomando. Wapo watatu ila wanatosha kuifanya kazi yoyote ile ambayo inahitaji akili na mabavu kwa pamoja lakini pia huyu Bilali atakuja kutupa jina au majina ya watu wengine ambao watatupa msaada katika hili ambayo mzee alimwachia yeye pekee”
“Kwahiyo meshimiwa tunaweza kusema tumejiandaa kwa hili?”
“Ndiyo”
“Ni kipi ambacho kinafuata?”

“Ni kwamba kwa sasa nasubiri Max akutane na Bilali kisha baada ya hapo tutakutana wote kwa pamoja na baada ya hapo ndipo tutaanza kuitekeleza hii kazi rasmi. Kuna majina ya watu wawili ambayo yamejitokeza katikati ambao ni gavana wa benki kuu na Madilu Mpagazi ambaye ni mfanya biashara mkubwa sana ndani ya taifa hili lakini pia Laurent Mande ambaye alikuwa ni gavana aliyepita anadaiwa kwamba yupo hai na anaishi. Hivyo tutakuwa tunafanya kazi zote kwa wakati mmoja kwa kugawana majukumu na kazi za kwanza itakuwa ni kuanza na hawa wa pembeni kwa kuwaua wote na baada ya kuhakikisha kwamba hakuna kitu tena ambacho kinaweza kutokea ndipo tutamface yeye moja kwa moja na kumuua na watu wake wote ambao watakuwa wamebaki”

38 inafika mwisho.

Wasalaam.
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 39
“Max na Bilali wanakutana lini na mpango unatakiwa kuanza lini mheshimiwa” waziri mkuu aliuliza akionekana kabisa kuwa na hamu kubwa sana ya kuweza kulijua jambo hilo.
“Nitawapa taarifa kuhusu hilo lakini na nyie kwa sasa kila mtu anatakiwa kuanza kuifanya kazi ikiwa ni kukusanya taarifa zote za mtu huyu na watu wake maana naamini kwamba mna vijana wenye uwezo mkubwa sana na kama mtapungukiwa vijana basi mtanipa taarifa niweze kuwaongezea”

“Sawa mheshimiwa, lakini huyu mtu ni mkubwa sana huoni kama kifo chake kinaweza kuleta utata na kutuchafua kama taifa?”
“Hilo nalijua vyema na mniachie mimi, siku ya mwisho nitamhitaji akiwa hai kabisa mzima wa afya ili afe kifo ambacho hakuna mtu hata mmoja ambaye ataweza kuhisi chochote zaidi ya kuamini kwamba amekufa kihalali”

“Nchi ilikuwa inasubiri kwa hamu kubwa sana kuweza kumpata raisi wa aina yako na kwa hili najua Tanzania itakuwa kwenye mikono salama sana”

“Hatutakiwi kuanza kujipongeza mapema sana namna hii kwa sababu hii ni vita ambayo yeyote anaweza kufa kati yetu, kumbuka huyu mtu anaijua serikali hii kuliko sisi wote hapa kwa sababu ameiendesha kwa miaka kumi akiwa kama kiongozi mkuu hivyo usije ukaona ukimya wake ukajua amekata tamaa, huko aliko naye pia anajiandaa na kutuundia mipango mizito sana. Kwahiyo jambo la mhimu sana ni kuutanguliza uzalendo mbele kwanza kabla ya jambo lolote lile, Mungu atulinde tuweze kuikamilisha kazi hii”

“Mungu ibariki Tanzania” waliitikia kwa pamoja kisha raisi akawaruhusu wanaume hao waweze kuondoka Ikuku. Baada ya kufika nje ya ofisi hiyo waziri mkuu akigeuka na kutamka;
“Tumia imani ya mtu ili kumfanya akuamini, kufanikisha hilo unatakiwa kuhakikisha yeye anakuamini kwanza kisha unaitawala akili yake. Rahisi sana” waziri mkuu aliongea kwa msisitizo sana huku akiwa anatabasamu na kutoweka hilo eneo.


Saa saba na dakika ishirini na tano usiku, Max alikuwa anatembea taratibu ndani ya mitaa ya Kariakoo. Alikuwa anategemea kutumiwa location ya mheshimiwa raisi lakini mpaka zinabakia dakika tano tu za kuweza kukutana na mtu ambaye aliambiwa akakutane naye hakuwa ametumiwa hiyo location na wakati huo alikuwa ameishika barabara ya Mnazi mmoja kuelekea kwenye makutano ya barabara ya Mnazi mmoja, gerezani, Karume na Msimbazi.

Alikuwa ameishika simu yake akiwa anaingalia kwa umakini wakati anakaribia kufika kwenye hayo makutano, alisimama baada ya kuhisi kwamba simu yake haikuwa sawa, simu ilikuwa nzito sana tofauti na alivyokuwa ameizoea siku zote. Hali hiyo ilifanya taa nyekundu kuwaka kwenye kichwa chake baada ya kujua kwamba hapakuwa na usalama sana ndani ya hilo eneo. Aliiangalia vizuri sana aligundua kwamba dakika kumi zilizokuwa zimepita simu hiyo ilikuwa imehakiwa bila yeye kujua, alitabasamu na kusikitika maana alikuwa mzembe sana siku hiyo kitu ambacho kilikuwa kosa kubwa sana anapokuwa mazingira hatari sana kama hayo.

Aliirudisha simu yake mfukoni na kusimama pembezoni mwa duka moja akiwa ameegamia nguzo na kufumba macho, masikio yake yalikuwa makini sana kusikiliza kile ambacho kilikuwa kinakuja eneo hilo. Mwili ulisisimka sana na kumfanya asimame na kuhema kwa nguvu baada ya kuhisi kama kuna upepo ulikuwa unakuja kwa kasi sana ndani ya sehemu ambayo alikuwepo, alijivuta pembeni kidogo ulisikika mlio mkali wa kitu kikigonga kwenye nguzo ya umeme. Aliangalia kwa umakini na kugundua kwamba kilikuwa ni kitu kama saa lakini pembezoni kilikuwa na vitu vyenye ncha kali sana kiasi kwamba kama vingezama kwenye mwili wake ingekuwa hatari sana.

Akiwa anashangaa kutaka kujua kwamba ni nani ambaye alikuwa amefika ndani ya hilo eneo umeme ulikatika ghafla sana, alishangaa sana eneo hilo kutowepo kwa mlinzi hata mmoja hiyo ilikuwa ni ishara kwamba wenyewe walifika mapema hata kabla yake na kuweza kusafisha eneo hilo hivyo hata yeye wakati anafika walimuona vizuri sana.

Akiwa anaendelea kujiuliza alipokea maumivu makali kwenye bega lake bila kuelewa kwamba mtu ambaye alikuwa anamshambulia alikuwa anatokea wapi, kabla hajatua chini alipigwa na buti lingine kali sana ambalo lilimzoa mpaka katikati ya barabara ambapo alitua kwa mkono mmoja na kuzunguka kwa nguvu sana kisha akakaa sawa akiwa kwenye mavazi meusi. Mwanaume alisimama vizuri na kujinyoosha pale ambapo alikuwa ameguswa na mwanaume huyo huku akizizungusha koti lake kubwa na kutoa shoka ambalo aliliweka pembeni kwani alipewa maagizo kwamba anatakiwa kuongea na mhusika hivyo hakuona sababu ya msingi ya yeye kuweza kutumia shoka maana ingekuwa ni kufanya mauaji.

Umeme ulirudi tena ghafla sana hiyo sehemu tu ambayo walikuwepo ndipo alipo muona mwanaume mmoja akiwa na simu yake anaibonyeza na bila shaka huyo ndiye ambaye alikuwa anacheza michezo yote hiyo ya kuhaki simu na kukata kata umeme. Walikuwa ni wanaume wawili ambao walikuwa wanamtazama kwa hasira sana.

“Aliye watuma yuko wapi?” aliuliza swali rahisi sana lakini nani angemjibu hilo swali lake? Hawakutakiwa kuwa na maneno ya kwenye kanga sana bali walipaswa kujibizana kiume. Aligundua kitu ambacho kilikuwa kinahitajika hapo hivyo aliurudisha mguu wake mmoja nyuma na kuuweka vizuri kuwapokea wanaume ambao walikuwa wanakuja kwa pamoja wakiwa wanazunguka kwa kasi kubwa sana ambayo ilimfanya arudi nyuma.

Mwanaume mmoja alikuwa anakuja kwa kasi akiwa anazunguka chini huku mmoja akiwa juu, alijigeuza kutaka kupita katikati yao lakini hakufanikiwa baada ya kupigwa na ngumi tatu za nguvu lakini hata yeye hakutua kinyonge baada ya kugeuka kwa kasi na kumtandika mwanaume mmoja na mabuti mawili wa kifua ambayo yalimtupa mbali sana. Aliyekuwa na saa ya chuma kwenye mkono wake aliirudisha kwa nguvu na kuanza kumfuata Max lakini saa hiyo ilidakwa na kurudishwa kwake hali ambayo ilimfanya aache kushambulia kwanza na kuamua kujilinda na kuikwepa saa yake mwenyewe ambayo ilimbaraza kwenye shavu lake ila kwa bahati mbaya sana wakati anageuka baada ya kuikwepa saa yake alichotwa na mtama bila kutarajia wakati anashuka chini alipigwa na buti baya sana la uso ambalo lilimburuza kwa hatua kadhaa akabaki chini anagugumia kwa maumivu.

Aliyekuwa kando yake alizunguka na double kick ya hatari ambapo teke moja Max lilimkosa na lingine likatua kwenye mbavu yake na lilionekana kumuingia vyema kwa namna alivyo itikia ila naye alirudisha ngumi nyingi sana za kifua ambazo zilimfanya mwanaume huyo kuhema na kupiga goti huku akiwa anatapika damu maana ngumi ambazo zlitandikwa zilionekana kuwa nzito sana kuliko hata hali yake ilivyokuwa inaweza kuhimili. Max alikuwa anamsogelea taratibu mwanaume huyo hali ambayo ilionyesha hatari ya yeye kuimaliza kazi haraka sana.

“Mwache bwana mdogo huyo, mimi ndo nina shida na wewe. Sogea ujaribu habati yako kwa dakika tatu na kama ukishindwa kuzihimili basi nakuua”
“Wewe hapo ndo unanipa mimi muda wa kujilinda, hahaha hahaha hahahah” max alicheka sana akiwa anamsogelea Bilali kwa mahesabu makali sana, huyo ndiye mwanaume ambaye alikuwa amefika hapo na huo ulikuwa ni muda wao mzuri zaidi wa kuweza kupimana mabavu.

Hatua zao wote ziliwakutanisha katikati ya barabara ambapo wote walizunguka na mateke makali ambayo yalitua kwenye shingo zao na kila mmoja akaonekana kuyasikilizia maumivu haswa maana walikuwa wamekutana wanaume wawili ambao walikuwa na uwezo mkubwa sana wa kimapigano. Bilali alidunda chini huku akiwa kama anaruka sarakasi ya mbele ila ilikuwa danganya toto tu maana hakwenda bali alisimama ila kwa bahati mbaya sana Max akawa ameingia kwenye huo mtego ambapo aliishia kupiga hewa alikutanishwa na buti la taya na kumfanya arudi nyuma lakini hakurudi kijinga bali aliudaka mkono wa Bilali ambapo alimvutia upande wake na kulipitisha goti kali sana kwenye kifua cha mwanaume huyo na kila mtu akadondokea upande wake huku akiwa anajishika kwa nguvu.

Wote walichomoa visu vikali sana kwenye viuno vyao huku vijana wa Bilali wakiwa wamekaa pembeni kila mtu akiwa anasikilizia maumivu makali wakiangalia wazee wa kazi wanavyo itendea haki sanaa ya mapigano huku wao wakionekana kama waliingilia sherehe ambayo hakikuwa yao. Namna watu hao walivyokuwa wanavizungusha visu vyao ilikuwa ni ngumu sana kuweza kuamini kwamba kuna mmoja angepona hapo.

Ilichukua dakika kumi na tano wakiwa bado wanapigana vibaya sana bila kupumzika, kila mtu alikuwa na maumivu kwenye sehemu ya mwili wake mpaka pale ambapo Max alifanikiwa kukifikisha kisu kwenye shingo ya Bilali lakini naye mwanaume huyo kwa mkono wake wa kushoto alikuwa amekiweka kisu chake kwenye sehemu ya siri ya Max. waliangaliana kwa dakika nzima kisha kila mtu akaitoa silaha yake wakasogea pambezoni mwa barabara ili wazungumze sasa baada ya kupokeana na kuweza kutambuana kwa uzuri kabisa.

“Kuna sababu gani ambayo imekufanya wewe uhitaji kuniona hapa?”
“Hutaki hata tutambuane japo kwa majina ndugu yangu?”

“Max”
“Bilali”
“Nakusikiliza”

“Unaonekana ni mtu ambaye hupendi kupoteza kabisa muda wako”
“Namchukia sana mtu ambaye anautumia vibaya muda wangu na msaliti. Hao ndio adui zangu wakubwa wawili kwenye maisha yangu”

“Unaonekana kuwa makini lakini mbona unakuwa mzembe sana kiasi hicho, huoni kama unaweza kufa kirahisi sana namna hii?”
“Mhhhh inawezekana ila huyo wa kuja kuniua alitakiwa awe amejipanga sana kwa sababu atawatoa sadaka watu wengi sana”

“Wakija watu wawili wenye uwezo kama wangu si wanakuua vizuri sana?” Bilali alitamka huku akiwa anatoa kinywaji kwenye koti lake na kukinywa kidogo kisha akamrushia na Max.

“Mhhhh sio rahisi sana namna hii, kama unataka kuniua linakuwa suala la kuishi na kufa hivyo siwezi kupigana kirahisi sana namna hii. Kama ningekuwa na lile shoka kwenye mkono wangu wale vijana wako wawili wote walikuwa wanakufa kwa dakika mbili tu kwa namna walivyo wazito lakini pia hata wewe sidhani kama ungekuwa umekaa kwa amani sana mpaka sasa ila nikiri kwamba wewe ni miongoni mwa watu hatari sana ambao mimi nimewahi kukutana nao”

39 inafika mwisho.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom