SIMULIZI ZA KIPELELEZI

FEBIANI BABUYA

JF-Expert Member
Mar 5, 2022
1,038
1,927
Je unatamani kuzisoma simulizi lukuki za kipelelezi ama kijasusi kama wengi mnavyopenda kuziita?

Kama jibu ni ndiyo basi leo nakuwekea list ya simulizi zangu za kipelelezi ambazo utazipata kwa bei rafiki kabisa. Nakuweka mtirirko wake na bei zake hapa chini

1. ULIMWENGU WA WATU WABAYA....3500

2. I WANT TO DIE JUDGE...3500

3. GEREZA LA HAZWA...4000

4. INNOCENT KILLER (THE REVENGE)/ MUUAJI ASIYE NA HATIA (KISASI)....4500

5. NYARAKA NAMBA 72/ DOCUMENT NUMBER 72...4000

6. ELECTION SAGA MONEY IN BLOOD (SAKATA LA UCHAGUZI PESA KWENYE DAMU)....4000

7. JIJI LA KAMARI...4000

8. BADO NINAISHI (ASHRAFU NDILO JINA LANGU)....5000


Unaweza ukalipia ili kuzipata simulizi hizo kwa hizi namba

0621567672 (WhatsApp)..... HALO-PESA

0745982347.... M-PESA

0714581046.... TIGO-PESA

Hakiki jina, zote jina linakuja FEBIANI BABUYA.


Unaweza ukanicheki WhatsApp au ukapiga cm kwa hizo namba. Ukinicheki unatumiwa simulizi muda huo huo.View attachment 2969956View attachment 2969955View attachment 2969954View attachment 2969958View attachment 2969957View attachment 2969959View attachment 2969960View attachment 2969961
FB_IMG_1713700409446.jpg
 
Ushauri wangu:-
1. Weka walau episode 2 au 3 Kwa kila simulizi Ili wadau wapime ubora wa kazi yako, AU
2. Weka simulizi Moja free Ili wadau wapime umahiri wako wa kutunga.

NA NDIO MAANA HATA MOVIE ZINA TRAILER,LENGO NI HILO KUTOA HAMASA KWA HADHIRA

Sent from my Infinix X6516 using JamiiForums mobile app
 
Ushauri wangu:-
1. Weka walau episode 2 au 3 Kwa kila simulizi Ili wadau wapime ubora wa kazi yako, AU
2. Weka simulizi Moja free Ili wadau wapime umahiri wako wa kutunga.

NA NDIO MAANA HATA MOVIE ZINA TRAILER,LENGO NI HILO KUTOA HAMASA KWA HADHIRA

Sent from my Infinix X6516 using JamiiForums mobile app
Asante sana kwa ushauri kiongozi.

Kuhusu kupost simulizi nzima kidogo itakuwa changamoto maana since 2022 naposti humu Jf ila Hilo la episodes kadhaa nitalifanyia kazi kuanzia jioni 👏
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 1
USIKU WA KUTISHA

Usiku wa manane mvua ikiwa inanyesha mithili ya kufunguliwa kwa koki iliyopo huko angani, alionekana mwanaume mmoja akiwa ndani ya nguo nyeusi na begi jeusi kwenye mkono wake huku koti lake jeusi refu ambalo lilivuka magotini likikamilisha mwonekano wake wa kuwa moja kati ya wanaume ambao walikuwa wanatisha mno.

Akiwa na kofia yake kubwa aina ya pama kwenye kichwa chake, alikuwa anatembea haraka haraka tena kwa uangalifu mkubwa akionekana wazi kuwa mtu ambaye alikuwa makini sana na begi lake ambalo lilikuwa kwenye mkono wake ili lifike salama mahali ambapo alikuwa anatakiwa kulifikisha usiku huo.

Akiwa kwenye huo mwendo wake wa haraka baada ya kufika katikati ya barabara ndogo ambayo ilikuwa imezungukwa na majengo marefu sana ambayo yalikuwa yamejengwa kwa mawe magumu mno huku pembezoni kukiwa na vichochoro vingi ambavyo vilielekea maeneo tofauti tofauti. Alihisi kwamba hilo eneo ni kama kulikuwa na ugeni, nafsi yake ilimpa taarifa hiyo kwamba walikuwepo watu wengine ukiacha yeye.

Masikio yake yalimtekenya na kumpa taarifa hiyo kupitia mlango wake wa hisia na alikuwa akiziamini sana hisia zake kwa kuamini kwamba zisingeweza kabisa kumdanganya kamwe hivyo akawa na uhakika kwamba alikuwa kwenye hatari majira hayo ya usiku wa kiza totoro, huku taa kwa mbali zilizokuwa zimezunguka kwenye majengo ya karibu yake zikiwa zinatoa mwangaza ambao ulimsaidia kuona kila kitu ambacho kilikuwa pembeni yake.

Alisimama na kuyafumba macho yake kisha akayaweka masikio yake kwenye hali ya utulivu na usikivu mkubwa isivyo kawaida ili aweze kujua kwamba huyo mgeni au hao wageni walikuwa wamejifichia wapi na wangetokea wapi ili aweze kujihami mapema kabla hajapata madhara yoyote yale. Akiwa amesima hapo na begi lake mkononi ambapo mkono mmoja alikuwa ameuweka kiunoni sehemu ambayo ilikuwa na kisu kikali sana, alihisi kwamba kuna kitu kilikuwa kinakuja alipo kwa kasi kubwa sana kiasi kwamba sikio lake lilicheza kumpa ishara hiyo hivyo aliinama kwa kasi mithili ya mwanga wa radi ambavyo huwa unajitokeza machoni radi ikipiga kisha ungetoweka haraka.

Kuinama kwake kulimsaidia kupishana na shoka la chuma ambalo lilienda kukita kwenye moja ya kuta za majengo marefu ambayo yalikuwa karibu na alipokuwa amesimama. Alihema kwa nguvu kwa tumaini la kushukuru kuweza kupona kwenye dhahama hiyo na kuamua kugeuka kwa kasi kubwa ila wakati anageuka alitumia muda mwingi sana ambao ulimuingiza matatizoni.

Alihisi kifua chake kinamuwasha maana spidi ambayo ilitumika kumkita hapo ilikuwa ni kama umeme unavyo safari kwenye njia zake, alitema damu maana alipokea mishindo mikali ya haraka haraka ya mabuti ambayo yalitoka kwa mtu ambaye alikuwa ana nguvu kubwa sana miguuni na mtu huyo alionekana dhahiri alikuwa amedhamiria kuweza kumuua moja kwa moja.

Mwanaume huyo licha ya kurushwa mbali karibu na kuta za mijengo hilo, mgongo wake ulikuwa umelenga jiwe ambalo lilikuwa lipo kwenye msingi mkubwa wa jengo moja na kama angekita hapo basi moja kwa moja alikuwa anaupoteza uti wa mgongo wake, hakuwa tayari kufa kifala sana namna hiyo hivyo aliutanguliza mkono wake baada ya kujipinda kidogo tu na mkono wake ndio ambao ukakita kwenye jiwe hilo la msingi wa hiyo nyumba. Mkono wake ulikuwa na gloves lakini nguvu ambayo ilitumika kukita kwenye huo ukuta ilifanya koti lake kujivuta kidogo na kuufanya mkono wake uonekane ambapo mkono huo ulikuwa na tattoo (tatuu) iliyokuwa inasomeka 002 mbele yake pakiwa na alama ya nyoka.

Mwanaume huyo alitua chini na kukiweka sawa kifua chake na kuifuta damu ambayo ilikuwa kwenye mdomo wake kisha akageuka kumwangalia mtu huyo ambaye alikuwa amemvamia ndani ya hilo eneo. Kwa bahati mbaya sana mtu ambaye alikuwa mbele yake hakuwa akionekana sura kwani sura yake ilikuwa imefunikwa na kitambaa cheusi huku naye akiwa amevaa mavazi kama yake mpaka kofia kichwani ilikuwa ni kama yake. Kitu pekee ambacho walikuwa wametofautiana ilikuwa ni kwamba mvamiwaji uso ulikuwa wazi na mvamiaji uso wake ulikuwa umefunikwa wote na kumfanya asitambulike kabisa kwamba alikuwa ni nani.

“Tunafahamiana kabla?” mvamiwaji aliuliza swali ambalo halikuwa na majibu, alitabasamu kidogo na kukitoa kisu chake ambacho mara ya kwanza hakufanikiwa kukitoa. Mwenzake alikuwa amesimama tu anamwangalia bila wasiwasi kwenye macho yake. Aliyakanyaga maji ya mvua chini kwa nguvu na kuyafanya yapande juu kuelekea alipokuwepo mvamiaji kisha akakirusha kisu kwa kasi kikiwa kinapita kwenye yale maji huku naye akija kwa nguvu sana kwa hatua ambazo zilikuwa zinapigwa kwa umakini sana.

Mwanaume ambaye alikuwa mbele yake hakukikwepa kile kisu bali alikiacha kikazama kwenye bega lake, wakati huyo mvamiwaji naye alikuwa amefika eneo alilokuwepo ambapo aliituma ngumi yake eneo ambalo lilikuwa na kisu ili akizamishe zaidi ndani. Mvamiaji ni kama alishtuka kutoka kwenye tafakari ambayo alikuwa nayo kwa muda ambao alikuwa hapo hivyo aliteleza kwenye maji kusogea nyuma kidogo ya alipokuwa na kufanya ngumi hiyo ipige hewa.

Mvamiwaji alizunguka teke la chini ambapo mvamiaji aliruka sarakasi ya nyuma na miguu yake ikatua kwenye ukuta na mikono ikidaka sehemu ya jiwe akawa amegeuka miguu juu na mikono uelekeo wa chini akimwangalia mwenzake ambaye aliishia kuyasambaratisha tu maji ambayo yalikuwa chini na hakufanikiwa kumpata mtu wake. Mvamiwaji alichukia sana kiasi kwamba akavua mpaka koti lake na kulirushia pembeni ila wakati anafanya hayo yote mvamiaji alikichomoa kisu kwenye bega lake na kukirudisha kwa mwenye nacho kikiwa kinaenda kwa mwendo mkali ambao ulipatikana kutokana na spidi ya mrushaji kuwa kubwa sana. Mwanaume huyo alijitahidi sana kukikwepa kisu hicho kikaishia kumbaraza kwenye shavu lake ila wakati anapambana kukikwepa kisu hicho mvamiaji alikuwa ameshuka pale juu kama kimbunga.

Alitua kwenye mbavu ya mvamiwaji ambapo ngumi mbili zilitosha kumfanya agugumie kwa maumivu makali ambayo yalijitawanya kila sehemu ya mwili wake. Alirudi nyuma akiwa anayumba yumba, mvamiaji alidunda kwa mkono mmoja na kujibetua na meteke mawili ambayo mvamiwaji aliyaona na kuyakwepa kwa kuinama ila wakati anainuka mvamiaji huyo alizungusha teke la chini na kumzoa mwanaume huyo ambaye angedondokea mgongo kwenye maji ambayo yalikuwa hapo chini yametuama ila hakufanikiwa kuiona ardhi baada ya kushindiliwa mateke mawili ya shingo ambayo yalimburuza mbali sana kwenye maji ambayo yalikuwa hapo karibu.

Alipata maumivu ambayo ilikuwa ni siri yake ndani ya mwili wake namna ya kuweza kuyaelezea, akiwa anatoka damu kwenye mdomo wake na puani huku kifua kikiwa kinawaka moto pamoja na shingo yake, aliinuka kwa maumivu huku akiunguruma kupiga kelela za hasira, aliinyoosha shingo yake mpaka ilipokaa sawa akageukia ule upande ambao alikuwepo mvamiaji ambaye kwa namna alivyokuwa anamshambulia alionekana kwamba alikuwa hapo kuweza kumuua.

Ila wakati anageuka tu, umeme ulikatika ghafla sana hata yeye mwenyewe alibaki kwenye mshangao maana lilikuwa ni tukio la haraka sana ambalo hata yeye hakuweza kulitegemea kwamba lingetokea majira hayo na wakati kama huo. Kukatika kwa umeme huo kwake ilikuwa ni ahueni maana angepata muda wa kupumzika japo gizani ingekuwa ni ngumu kumuona adui yake ila aliamini kwamba angekuwa makini na wakati huo angepumua kwanza kwani mtu ambaye alikuwa anapambana naye kama sio umeme kukatika basi ni wazi angemuua mapema mno.

Alitulia na kuweza kusikilizia kujua adui yake alikuwa wapi lakini hakusikia kitu zaidi ya mvua ambayo ilikuwa inaendelea kushuka kwa wingi. Akiwa anahitaji kupiga hatua moja umeme ulirudi tena lakini alishangaa baada ya kugundua kwamba mtu ambaye alikuwa amemvamia kwenye hilo eneo hakuwepo, ikimaanisha kwamba ni muda mrefu sana alikuwa ametoweka hapo. Aligeuka kwa pupa sehemu ambayo begi lake lilidondokea baada ya kupigwa lakini begi halikuwepo kwenye hilo eneo ishara ya mhusika ambaye aliingia hapo kutoweka nalo.

Aliogopa sana na kubaki akitetemeka kwenye mdomo wake, hakuwa anaamini kwamba alikuwa amelipoteza begi kizembe sana namna hiyo na begi hilo lilionekana kuwa la mhimu sana. Akiwa kwenye huo wasiwasi mkubwa aligundua kwamba mita kadhaa kwa chini kutoka alipokuwa amesimama yeye kulikuwa na karatasi nyeupe ambayo ilikuwa na maandishi yaliyokuwa yameandikwa kwa damu ikiendelea kunyeshewa na mvua pale chini.

Aliisogelea karatasi hiyo na kuiokota ila baada ya kusoma kilichokuwa kimeandikwa hapo, aliiachia ghafla sana na kuanza kurudi nyuma huku akiwa anatetemea mwili mzima mpaka meno yake kwa namna alivyokuwa ameogopa na kushtuka kwani halikuonekana kuwa tukio la kawaida kwake kuweza kuona hali kama hiyo. Karatasi hiyo ilikuwa na maandishi ambayo yalikuwa yanasomeka “KAMARI YANGU YA MWISHO NDIYO KAMARI YAKO YA KWANZA”

Aliogopa sana kwa sababu hiyo ilikuwa ni kauli ambayo alikuwa anaitumia mwanaume mmoja ambaye yeye mwenyewe alimuua kwa mkono wake miaka kadhaa ambayo ilikuwa imepita. Aliangaza ile sehemu ambayo shoka lilikita muda ule lakini hakuliona hivyo aligundua kwamba mhusika alikuwa ameondoka na shoka lake na kilikuwa ni kitendo cha haraka sana, alisogea hatua kadhaa na kukiokota kisu chake na kukipachika tena kiunoni huku akiwa anaitoa simu yake mfukoni akionekana kwamba kuna mtu wa mhimu sana ambaye alikuwa anahitaji kumpatia taarifa za tukio hilo ila kwa bahati mbaya sana simu ambayo alikuwa anahitaji kuitumia kufanyia mawasiliano ilikuwa imevunjika na hapo akakumbuka kwamba ilipasuka baada ya teke zito kuzama hiyo sehemu hivyo aliamua kutoweka haraka sana hilo eneo.


Rasmi tunaanza kuifunua episode 1, ni mwanzo tu wa yale mengi ambayo tunakwenda kuyafunua ndani ya simulizi hii mpya. Nipe muda wako, jicho lako na umakini wako ile twende sawa ndani ya simulizi hii.

Kwenye kalamu nipo mwenyewe.

Tchao.
FB_IMG_1713700415206.jpg
 
Stori: Innocent Killer (The Revenge)
Msimuliaji: Bux the story teller
Umri: 18+
Sehemu ya Kwanza:

NB: Hadithi hii ni ya kubuni na kufikirika haihusiani na maisha ya mtu yeyote, wala taasisi yoyote wala mamlaka yoyote ile, lengo lake ni kuburudisha na kutoa burudani kwa wasomaji wangu.

ANZA NAYO.........................

Saa 6:59 za usiku kukiwa na kiza kinene na mvua kali sana nje kukisindikizwa na radi zisizo isha pamoja na upepo mkali wakati huo wa usiku kwenye chumba kimoja kidogo cha vitabu ambacho ndani yake anaonekana mwanaume mmoja akiwa kwenye meza ndogo ambayo alikuwa akiitumia kusomea anapokuwa ndani ya hicho chumba mbele yake palikuwa na vitabu kumi ambapo saba alikuwa ameviweka pembeni kuonyesha alikuwa amevisoma vilibakia vitatu ambavyo navyo ilikuwa ni lazima avimalize usiku huo huo kabla hakuja pambazuka. Vitabu vyote kumi vilikuwa ni vitabu vya sheria ya nchi ya Tanzania, aliangalia saa yake mkononi muda ulikuwa umeenda sana lakini hakuwa na namna ya kufanya ilikuwa ni lazima atimize kile ambacho kilikuwa mbele yake alipiga miayo na kuiweka vizuri miwani yake usoni akainama kinyonge sana kwenye kitabu huku akiwa na mawazo lukuki kwenye kichwa chake.

"Sina uhakika wa maisha yangu kuwa marefu baada ya kesho kwa maamuzi nitakayo yaamua najiona kuwa na maisha mafupi mno lakini mimi siwezi kuipindisha sheria ambayo nimeisomea kwa muda mrefu na naijua vizuri kuliko hata herufi za jina langu eeh MUNGU naomba unisaidie na kuniongoza katika hili" alitoka kwenye mawazo na kuivuta pumzi ndefu sana kisha akatulia na kuinamia chini kukipitia kitabu cha nane kati ya vile kumi ambavyo ilikuwa ni lazima amalize kuvisoma usiku huo.

Markvelous Japhary jaji mkuu wa nchi ya Tanzania ndilo lilikuwa jina la huyu mwanaume ambaye alikuwa ndani ya makataba yake ndogo nyumbani kwake akiwa anaendelea kujisomea vitabu vya sheria ambazo alizijua kiundani kuliko binadamu yeyote kwenye nchi yake. Kesho yake alikuwa na kesi kubwa sana ya kuitolea hukumu mbele ya mahakama ambayo ilikuwa inasubiriwa na taifa zima na ni tukio ambalo lilikuwa linaenda kurushwa na kushuhudiwa moja kwa moja mbele ya watu wote ndani ya nchi hii, alikuwa anaenda kuifanyia maamuzi kesi moja ya gaidi mmoja ambaye alikuwa na shutuma mbaya za kuweza kumuua mheshimiwa raisi wa nchi ya Tanzania kwa kumpiga risasi tano kwenye kichwa chake.

Alivuta kumbukumbu zake vizuri siku mbili zilizopita akiwa ndani ya ofisi yake maeneo ya posta simu yake ya mfukoni iliita aliiangalia alikuwa ni mheshimiwa makamu wa raisi aliipokea na kupokea taarifa nzito ambazo zilimfanya aache kila alichokuwa anakifanya aliambiwa kwamba raisi wa nchi ya Tanzania alikuwa amefariki dunia kwa kuuawa msako ulikuwa unafanyika kuweza kumpata mhusika na tayari kuna watu wamekamatwa kwa ajili ya mahojiano, hakuendelea na kazi tena siku hiyo alibeba kila ambacho kilikuwa ni cha kwake na kupanda gari yake ambayo aliiendesha kwa kasi sana bila kujali kama kuna tatizo zito linaweza kutokea kama angepata ajali na hilo gari lake, alikuwa amechanganyikiwa mwanaume ambaye alikuwa amekufa kwake hakuwa raisi wake tu alikuwa ni rafiki yake mkubwa ambaye walikua wote tangu wakiwa wadogo na kusoma pamoja alikuwa zaidi ya ndugu kwake aliumia mno aliitoa miwani yake na kufuta machozi yake akiwa yupo makini barabarani, alifika nyumbani kwake alimpita mkewe kama hamjui na kwenda chumbani ambako alikaa kwa dakika tano tu na kutoka akiwa amebadilika sura yake alijitahidi kujificha ila ilikuwa inatoa machozi muda wote.

"Who did this to my friend, oooh noooooo it's definitely impossible how can they let this happen?" Alikuwa amepanda kwenye gari yake alitoa simu mfukoni na kuipiga mahali.

"Nitakuwa hapo kwa dakika thelathini zijazo" aliongea kwa uchungu na kukata simu yake alitoka kwake kwa spidi mpaka mlinzi wa getini alibaki anamshangaa sana bosi wake alikuwa ni mtu mpole na alimjua vyema hakuwa mtu wa pombe kabisa kwenye maisha yake leo alikuwa kama mtu aliye lewa kama sio kupandwa na wazimu hata mkewe ambaye alikuwa amesimama juu ya nyumba hiyo ya ghorofa alibaki anamshangaa mumewe kwa hali ambayo alikuwa nayo jioni hiyo. Safari yake ilienda kuishia nje ya nyumba moja kubwa maeneo ya Makongo juu hapo palikuwa nyumbani kwa CDF mkuu wa majeshi wa nchi ya Tanzania mheshimiwa Jaiwelo mkupi makubilo, alikuwa anajulikana sana hapo ila alishangaa leo anavyotaka kuingia alizuiliwa mlangoni na kuulizwa kama alikuwa na miadi ya mtu huyo alimpiga jicho kali sana huyo mlinzi ambaye alimzuia bila shaka alikuwa ni mwanajeshi.

"We mjinga hivi unajua unaongea na nani ambaye unanizuia leo kuingia humu ndani?" Aliongea macho yake yakiwa mekundu wakati huo alikuwa amemkunja mwanajeshi huyo shingoni ilikuwa ni dharau sana kijana mdogo kama huyo kumsimamia jaji mkuu wa serikali na kumzuia kirahisi sana namna hiyo
"Najua lakini tumeambiwa tusimruhusu mtu yeyot....." Kabla hajaongea maneno yake yote simu yake ya mfukoni iliita, aliipokea na kuitikia mara moja tu.

"Nisamehe mkuu" kisha akasogea pembeni kumuacha jaji huyo apite kuonyesha kwamba aliipokea amri ya upande wa pili kumuacha mwanaume huyo aingie ndani bila kupata kizuizi chochote kile.

"We mjinga kwa hiki ulicho kifanya baada ya hapa nitakurudia uelewe namna ya kuishi na watu wakubwa kwenye nchi hii" mheshimiwa jaji mkuu alikuwa kama amechanganyikiwa usoni kwake kulikuwa na machozi mengi kama mtoto mdogo, alinyoosha moja kwa moja mpaka juu kabisa sehemu ya makutano ni wazi alikuwa mwenyeji sana kwenye nyumba hiyo alimkuta mtu ambaye alikuwa amemjia hapo.

"Unajua kilicho tokea?" Alisahau hata kusalimia alimuuliza mtu huyo huku akiwa amemkazia macho kwa hasira sana
"Ndiyo"

"Nina imani utakuwa umejua nani aliye husika na hili kupitia jeshi lako"?" Jaiwelo mkupi makubilo hakuongea chochote alitembea mpaka kwenye droo moja ndogo sana akatoa frashi ndogo na laptop akaja nayo mpaka pale alipokuwa amekaa mheshimiwa jaji mkuu, aliichomeka hiyo frash kwenye hiyo laptop na kuifungua ilionekana video moja tu humo ndani akairuhusu iweze kuanza kisha akaigeuzia kwa mheshimiwa jaji mkuu.

"Yuko wapi huyu shetani" aliuliza kwa hasira sana akifuta machozi yake baada ya kuweza kushuhudia namna mheshimiwa raisi alivyoweza kuuawa.

"Tayari yupo kwenye mikono yetu amekamatwa muda sio mrefu baada tu ya kutenda hili tukio"
"Amewekwa wapi muda huu namhitaji kwenye mkono wangu".

"Mark relax this is not easy as you may think, aliye uawa ni raisi wa nchi sio raia wa kawaida tu mtaani"
"No matter what I'm going to kill this idiot".

"Please don't do that kwa usalama wako na wa familia yako nisikilize kwa sasa tu tafadhali sana usifanye chochote" hakumjibu kitu mkuu wa majeshi zaidi ya kuibeba frash hiyo ambayo ilikuwa na ushahidi wote kisha akarudi zake nyumbani kwake akiwa amechanganyikiwa sana, kumbukumbu zake ziliishia hapo.

**********************
Raia wengi walilaani sana hicho kitendo cha mtu huyo kufanya hilo jambo walitaka auawe mpaka kunyongwa mbele ya mahakama wakiwa wanaona iwe kama fundisho kwa watu wengine, ushahidi kwa asilimia zaidi ya miamoja ulikuwa ukionyesha kwamba ni kweli mtu huyo alihusika moja kwa moja na hayo mauaji lakini mheshimiwa jaji mkuu alikuwa amepokea simu nyingi sana za kumtaka afanye namna yoyote ya kuipindisha hiyo kesi na kutengeneza ushahidi wa uongo ambao ungemuweka salama mtuhumiwa huyo ambaye mpaka muda huo hakuwa akijulikana ni nani. Akiwa ameanza kusoma kitabu chake hicho cha nane ghafla sana radi kali ilipiga umeme ukazima alihema kwa wasiwasi akianza kutokwa na jasho jingi usoni kwake mara simu yake ikaanza kuita kwenye hicho kiza kinene aliangalia namba ilikuwa ngeni kabisa hakuwahi kuiona kabla alisita kuipokea iliita mpaka ikakata. Sekunde kama kumi tu uliingia ujumbe ambao alisita sana kuufungua lakini hakuwa na namna.

"ANGALIA DIRISHANI KWAKO HAPO KWA NJE UTAONA MTU, KAMA KESHO UKIFANYA UJINGA WOWOTE ULE BASI FAMILIA YAKO ITAINGIA KWENYE KUNDI LA WANADAMU AMBAO WALIWAHI KUFA KIKATILI SANA ZINGATIA NILICHO KWAMBIA KESHO SAA NNE ASUBUHI MAAMUZI YAKO NDIYO YATAKAYO AMUA HATIMA YA MAISHA YA FAMILIA YAKO" ni ujumbe ambao ulimfanya aanze kutetemeka sana alitoa kitambaa mfukoni na kujifuta jasho lililokuwa linamtiririka usoni, aliiwasha tochi yake kubwa na kusogea dirishani kukiwa bado kuna kiza cha kutisha nje alifungua dirisha taratibu na kuchungulia nje alimulika tochi alishangaa baada ya kumuona ninja mmoja akiwa na mapanga yake mawili mgongoni amesimama pale chini, alionekana ni muda mrefu sana alikuwa ananyeshewa na mvua muda wote pale aliogopa mno.

Aligeuka nyuma baada ya kusikia kama kuna hatua za mtu lakini akahisi ni kichwa chake hakipo sawa aliyarudisha macho yake pale chini hakuona kitu chochote wala hapakuwa na alama ya uwepo wa mtu alianza kurudi nyuma taratibu kwa uoga aligeuka na kuchomoa bastola yake akainyooshea sehemu ambayo alihisi kuna mtu anakuja ghafla sana umeme ulirudi alishangaa mkewe amesimama mbele yake akimshangaa mumewe ameshika bastola tena ameelekezea kwake, aliishusha na kuiweka mfukoni haraka huku akiwa anatokwa na jasho jingi mno, mkewe alimfuata pale na kumkumbatia akiwa ana mpiga piga mgongoni.

"Punguza mawazo mume wangu najua siku ya kesho inakuumiza sana akili muachie MUNGU ila hakikisha unaamua kile kilicho bora mimi siku zote nipo nyuma yako kwa kila jambo" sauti moja ya kinanda mrembo sana ilimfanya atabasamu kwa mara ya kwanza tangu kuingia kwenye hicho chumba, huyu ndiye binadamu pekee ambaye alikuwa anamjua kuanzia unyayo wake mpaka nukta ya mwisho ya unywele wake kichwani, akiwa mbele ya huyu mwanamke alikuwa anapata amani sana ya moyo aliinama na kumbusu mkewe tumboni ambapo palikuwa pametuna kuonyesha ilikuwa ni mimba kubwa tu.

"Is my son wonderful?" Aliuliza akichekelea kuonyesha wazi aliifurahia mimba hiyo kuwa ya mtoto wa kiume japo moyoni hakuwa na furaha yoyote ile.

"Hahahaha ananipiga mateke tu nafikiri dada yake atafurahia sana akizaliwa maana alikuwa anatamani sana kuwa na kaka yake pale anapokuwa anaonewa" mkewe alijibu huku akijitoa mwilini na kusogea pale mumewe alipokuwa anasomea.

"Jitahidi basi mume wangu uwe unapata muda wa kupumzika na leo usichelewe sana kulala kesho ni siku mhimu sana" alitabasamu baada ya kuisikia sauti ya mwanamke aliye mpenda sana, alimfuata na kumbusu kwenye paji lake la uso.

"Nakuja baada ya nusu saa tu mke wangu" alijibu kiunyenyekevu hakuhitaji kumuudhi mama kijacho wake alitabasamu na kuanza kuelekea mlangoni lakini aligeuka kabla hajatoka.

"Jason umempigia simu kumueleza hichi kinacho endelea?" Swali la mkewe lilimshtua kidogo mwanaume ambaye alikuwa anauliziwa hapo alikuwa ni mdogo wake wa damu kabisa ambaye alikuwa nje kimasomo jina lake alifahamika kama Jason Japhary na walizaliwa wawili tu.

"Anapenda mno kulala yule nitampigia simu baada ya kumaliza kesi kesho usijali" aliongea kikakamavu ila mwili wake ulikuwa unamsaliti alikuwa akitetemeka sana mkewe alimuonea huruma sana mume wake alikuwa kwenye wakati mgumu sana hakuwa na namna aliondoka na kwenda kulala. Jaji mkuu alibaki kwenye hicho chumba lakini hakuwa na mood ya kusoma tena alibaki akiiwazia ile meseji aliyotumiwa pamoja na alicho kishuhudia nje alijikuta akiogopa mno.

Ndo kwanza tunaifungua sehemu ya kwanza kabisa ya hadithi yetu mpya ya INNOCENT KILLER (THE REVENGE), the magic finger mwenyewe nipo na kalamu yangu....Bux the story teller.

TWENDE PAMOJA MPAKA MWISHO
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
TELLER: Bux the story teller
WhatsApp: 0621567672
Email: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA PILI
SONGA NAYO................

Kulikucha asubuhi na mapema sana baada ya kunyanyuka kwenye kitanda chake aligeukia pembeni yake hakuweza kabisa kumuona mumewe kipenzi alishtuka sana mama kijacho wa jaji mkuu, aliamka haraka na kujisogeza kwenye chumba cha kujisomea ambako ndiko alijua mumewe mara nyingi sana mtu huyo alikuwa anapenda kuwa. Alimkuta kama alivyo muacha jana yake usiku hakupata hata tone la usingizi alikuwa amejiinamia mkononi ameishika kalamu yake ya wino akiwa anaiangalia kwa umakini sana mkewe alimsikitikia mno mumewe alikuwa anateseka sana.

“Umelala hata kidogo?” alimuuliza kwa upole japo alielewa kwamba mtu huyo tangu jana yake hakuweza kabisa kulala wala kuigiza kuupata usingizi.

“Najihisi kama nimelala mwaka mzima sina hata tone la kuigiza tu la usingizi mwili wangu umegoma kabisa kuleta hisia za kitu kinacho itwa usingizi tangu jana ulivyo niacha hapa”

“Unahisi utajitesa hivyo mpaka lini? Kwa sababu kuna muda kwa nafasi yako utakuwa ukikutana na kesi za ajabu za kutisha sana kama unajiona kwamba hauko sawa una nafasi ya kumteua jaji mwingine yeyote asimame kwa niaba yako leo mahakamani”

“Hakuna kesi ambayo itakuja kuwa mbaya na ya kutisha kuizidi kesi hii huyu aliye uawa ni mheshimiwa raisi wa nchi lakini ukiacha hilo aliyekufa ni rafiki yangu halafu unakuja kuniambia nimuachie mtu mwingine kesi hii unahisi kuna mtu gani ataweza kuzikataa pesa kwa majaji waliopo? Kuna muda uwe unawaza kama mtu mzima” aliongea kwa hasira sana akiwa anatokwa na machozi haikuwa kawaida kwake yeye kuongea kwa ukali sana namna hiyo mbele ya mkewe, mkewe alijua amemkosea mumewe alihitaji kumuomba msamaha lakini ni kama alichelewa mtu huyo alitoka humo ndani muda huo huo alienda kujifungia chumbani ambako baada ya dakika kumi tu alitoka akiwa amevaa zake suti na begi mkononi hakuweza hata kumuaga mkewe siku yake ilikuwa imeharibika asubuhi na mapema kabisa.

Alifika nje na kutoa maagizo kwa walinzi wake haikuwa taabu kwa sababu alikuwa mtu mkubwa hivyo hata ulinzi wake ulikuwa ni wa namna yake, aliondoka na gari yake pamoja na walinzi kadhaa na dereva wake kuelekea mahakamani. Akiwa njiani mawazo yalimpeleka mbali sana.

“Unajua kwanini sipendi siasa?”
“Haujawahi kabisa kunipa sababu”

“Siasa ina mambo ya kutisha sana ndani yake ndiyo maana naiogopa sana nilishawahi kusikia kesi kadhaa nikajikuta nawaogopa mno hawa wana siasa rafiki angu nakuona kabisa umenogewa sana huko jiangalie sana maisha yako ndugu yangu tunaishi mara moja tu”

“Mark shida yako wewe ni muoga sana unajua hii nchi inahitaji viongozi wenye maono makubwa ambao bado ni vijana na hao viongozi wenyewe ndio sisi, ebu acha kuogopa kiasi hicho rafikio angu kama kila mtu angekuwa muoga sana namna hiyo basi mpaka leo nchi hii isingekuwa imepata uhuru tungekuwa tupo bado chini ya watu”

“Huwa naipenda sana nukuu ya methali moja inasema KINGA NI BORA KULIKO TIBA ina maana kubwa sana ndani yake ukiielewa vizruri. Ni kweli nchi inahitaji viongozi wenye maono na vijana lakini hao wenzetu ambao unawaona wanafanya hivyo tayari wana watu, wana mifumo na wana njia mbalimbali za kukimbilia hasa pale yanapotokea matatizo, wanajua tunaingilia hapa na tunatokea hapa sasa wewe hapo likitokea tatizo utakimbilia wapi na anakulinda nani? kumbuka hapa nakushauri kama marafiki ambao tumetoka mbali sana pamoja mimi sihitaji kukupoteza kabisa kwenye maisha yangu” zilikuwa ni kumbukumbu za Markvelous Japhary akiwa ndani ya gari lake, alikumbuka siku moja akiwa anamshawishi rafiki yake ambaye alikuwa anaipenda na kuihusudu siasa kuliko kitu chochote kile kwenye maisha yake lakini mwenzake huyo hakuweza kabisa kukubaliana na hilo jambo aliamua kuziishi ndoto zake ambazo kweli zilimpeleka mpaka Ikulu akasimama kama raisi wa nchi na ndiye ambaye aliweza kumteua Markvelous Japhary kuwa jaji mkuu kutokana na uwezo wake mkubwa lakini pia kama rafiki ambaye wametoka naye mbali sana.

Huyu ndiye aliyeweza kuyabadilisha maisha ya jaji mkuu wa Tanzania

“Kwa yeyote aliyehusika na hili hakika sitaweza kumuacha akiwa hai haitajalisha nitajiingiza kwenye matatizo gani ila lazima nihakikishe amekufa mbele kabisa ya mahakama kama malipo kwa walicho kifanya kwa rafiki yangu, najua watakuwa wameandaa watu wengi kwa ajili ya kumtetea mtu wao ili aachiwe huru ila mwamuzi wa mwisho ni mimi hapa lakini kuna maswali najiuliza huyo muuaji aliweza vipi kupatikana kirahisi sana namna ile? Mkuu wa majeshi hajanipa undani wa mambo ebu ngoja kwanza niweze kumalizana na hili kisha nikae nae vyema aweze kunisimulia kwa undani” alishtuka kutoka kwenye kuongea mwenyewe baada ya mlinzi wake kumfungulia mlango alijiweka saw ana kushuka tayari alikuwa kwenye eneo la mahakama.

“Afe huyo, afe huyo”
“Hakikisha unamuua hawezi kutuondolea kiongozi wetu”
“Afe afe ikiwezekana aletwe kwetu tuondoke naye afe huyo afe” zilikuwa ni kelele ambazo alizisikia kwa wananchi wenye hasira kali walichukizwa mno na raisi wao ambaye walimpenda sana kuuawa walihitaji mtuhumiwa aweze kuuawa. Hilo jambo lilimpa nguvu sana jaji baada ya kuona wananchi wote walikuwa wapo upande wake, akiwa anajiandaa kuanza kuelekea lilipo lango kuu la mahakama aliivua miwani yake baada ya kuona gari la magereza linaingia likiwa na ulinzi mkali mno dakika mbili zilipita alishushwa mwanaume mmoja mwenye upara na ndevu nyingi sana ambazo ni muda mrefu hazikuwahi kunyolewa, alikuwa kwenye minyororo mizito alivyo inua uso wake moja kwa moja alikuwa anaangaliana na jaji mkuu mwanaume huyo alimkonyeza jaji mkuu huku akitema mate chini, ni moja ya dharau kubwa sana ambayo aliifanya hapo. Markvelous aliitoa miwani yake na kumuangalia vizuri huyo mwanaume kwa hasira ambazo wazi wazi macho yalizungumza kwamba kama leo ukipona wewe shetani basi mimi naacha kazi ya kuwa jaji narudi kijijini kulima vitunguu na kuchambua dagaa.

Alianza kutoka pale na kuelekea kwenye ofisi yake humo mahakamani akavae nguo za kazi wakati huo maaskari wakiwa wanatangulia na mtuhumiwa kumpeleka kizimbani, akiwa anaingia kwenye lango kuu la mahakama alipokea meseji mbili kwenye simu yake ambazo zilipishana kwa dakika moja na nusu tu moja ilikuwa imetoka kwa CDF Jaiwelo Mkupi Makubilo na nyingine ilitoka kwenye namba ambayo bila shaka alikumbumbuka kwamba ilimtafuta jana yake usiku wa manane.

‘’USIFANYE MAAMUZI YA HASIRA MARK HILI NI JAMBO ZITO SANA LA NCHI NZIMA, HII NI KWA USALAMA WAKO NA FAMILIA YAKO LAKINI PIA KWA TAIFA ZIMA LINATEGEMEA MAAMUZI YAKO SAHIHI LEO” aliisoma meseji ya CDF ila hakujihangaisha hata kuijibu aliifungua hiyo ya pili.

“UNA DAKIKA CHACHE SANA ZA KUFANYA MAAMUZI YA BUSARA KWA AJILI YA KUIKOMBOA FAMILIA YAKO KISHA BAADA YA HAPO UTAINGIZIWA SHILINGI ZA KITANZANIA BILIONI KUMI KWENYE AKAUNTI YAKO YA BENKI UTAKAPO TOA TO MAAMUZI YA BUSARA NA YA KIUME ILA ZINGATIA SANA KAMA UKIENDA KINYUME KITABU CHAKO NA FAMILIA YAKO KINAENDA KUFUTWA KWENYE HUU ULIMWENGU” hii ni meseji ambayo ilimfanya atoe kitambaa kwenye mfuko wake na kujifuta jasho ambalo lilikuwa limeanza kumtoka kwenye uso wake alihisi joto kali mno, alihema kwa nguvu na kuizima simu hiyo hakuhitaji kujisumbua nayo tena.

Tukio la kesi ya mtuhumiwa wa mauaji ya mheshimiwa raisi lilikuwa linaonyeshwa moja kwa moja mubashara kabisa kwenye kituo kikubwa cha televisheni cha nchi kilicho julikana kama Tanzamax, kilikuwa ni kituo ambacho siku zote kilitoa habari za kuaminika na zenye uhakika zaidi na kilipendwa sana na wananchi hususani wale ambao huwa wanapenda sana kupata habari moto moto ambazo huwa zinajiri ndani ya nchi yao kutoka kwa watangazaji wao mahiri ambao walipendwa sana ndani ya nchi ya Tanzania.

“Tanzania oyeeeeeee”
“Nchi yetu oyeeeee”
“Idumu nchi yetu ya amani”
“ALale mahali pema peponi kipenzi chetu raisi wetu ambaye tutampenda siku zote za maisha yetu”
“Tanzania ya amani inawezekana”
“Uishi miaka mingi mheshimiwa jaji mkuu”
“Tanzania oyeee”
“Sisi ni watanzania”
“Tunaipenda Tanzania yetu” zilikuwa ni sauti kubwa za shangwe na vigelele vingi japo vilitoka kwenye vinywa vya watu kwa majonzi sana baada ya kusikia kauli ambayo iliwafariji sana na kuyafuta machozi yao kwa kumpoteza mpendwa wao ambaye ni wazi walimpenda sana

“WITH THE CLEAR EVIDENCE FOUND I SENTENCE YOU TO PUBLIC DEATH BEFORE THE COURT MR ABIR MUSHKANI (KWA USHAHIDI WA WAZI ULIO PATIKANA NAKUHUKUMU KIFO CHA HADHARANI MBELE YA MAHAKAMA MHESHIMIWA ABIR MUSHKANI)” Hii ndiyo kauli kutoka kwa jaji mkuu ambayo iliwapa matumaini wananchi ambao walikuwa nje ya mahakama na hata wale ambao walikuwa wanaona hilo tukio moja kwa moja kwenye runinga, hukumu hiyo ilifuata baada ya takribani masaa manne kupita wakiwa wanaiendesha kesi hiyo ambapo wanasheria wengi wakubwa na wabobevu walikuwa wakimtetea sana mtuhumiwa ila wote walikuja kunyong’onyea baada ya jaji mkuu mwenyewe kuonyesha ushahidi wa video moja kwa moja wa mtu huyo akiwa anafanya hilo tukio, ni jambo ambalo lilikuwa wazi hakukuwa na namna ya kulikataa tena.

Mtuhumiwa aliyejulikana kama Abir Mushkani alinyongwa hadharani mahakamani akiwa na minyororo yake mwilini kwa sababu alionekana kuwa mtu hatari sana kama angefunguliwa hapo, hilo tukio lilionyeshwa moja kwa moja ili kama kuna wengine wenye tabia kama zake waweze kukoma mara moja, ni tukio ambalo lilimpa heshima kubwa sana Markvelous Japhary ambaye aliona kama ametua mzigo mzito kwa kulipa kisasi kwa kifo cha rafiki yake japo kwa kutenda haki. Alitoka mahakamani na kuingia kwenye chumba chake aliichukua simu yake kwenye begi lake akaiwasha, alijaribu kumpigia mkewe kwa sababu asubuhi waligombana alihitaji kumuomba msamaha kwa kumkosea na kumtamkia maneno makali sana simu iliita kidogo na kukata akahisi huenda mkewe bado alimkasirikia, alijaribu kupiga kwa mara ya pili haikupatikana akajaribu tena na tena lakini haikupatikana kabisa.

Akiwa amekata tamaa alipokea ujumbe kwenye simu yake meseji zilikuwa mbili ilionekana zilitumwa muda kidogo sema kwa sababu aliizima simu ndiyo maana ziliingia kwa kuchelewa watumaji walikuwa ni wale wale.

“UMEFANYA MAKOSA MAKUBWA SANA MARK ILE VIDEO HAIKUTAKIWA KUONYESHWA HADHARANI NAMNA ILE UNAYAJUA MADHARA YAKE?” Ilitoka kwa CDF haikumshtua sana yapili ilitoka kwenye ile ile namba ambayo tangu jana ilimpa sana onyo.

“UNA DAKIKA KUMI NA TANO TU ZA KUWAHI NYUMBANI KWAKO KAMA UTAFIKA NDANI YA HUO MUDA UNAWEZA UKABAHATIKA KUIKUTA FAMILIA YAKO SALAMA ILA ZAIDI YA HAPO UTAUJUTIA SANA ULIMWENGU HUU NA NILIKWAMBIA MAPEMA” meseji iliishia hapo hakukumbuka hata kulivua vazi lake linalo mtambulisha kama jaji mkuu alitoka nje akiwa anakimbia sana.

Mchezo ndo kwanza unaanza chukua juisi safi na popcorn tuweze kusonga pamoja.

Bux the story teller.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom