Nimefarijika kuwa mama mzazi Ni MTU wa fireeeee,kitaeleweka tuu.SEHEMU YA NANE:
Mume wangu aliendesha gari kwa fujo sana ile siku, ni kama alikua amechanganyikiwa, sikutaka kumuongelesha, nilikua namuogopa, mwanaume niliempenda kwa mapenzi yote leo hii namuangalia kama kitu cha kutisha. Tulifika nyumbani nikapitiliza bafuni kuoga na kujitazama vizuri kwenye kioo cha bafuni, Lahaula....sio kwa alama zile mgongoni, ni kama nilichapwa mijeledi ya kustosha , mgongo ulikua na mistari ya kama kamba nene imepita na pia kwenye ile mistari damu ilivilia....
Dominic akaingia bafuni nadhani alihisi kua Kuna tatizo kubwa zaidi ya yale aliyoyaona kwenye gari, alipoingia na kuona ule mgongo alikaa chini akaanza kulia, sikuweza msogelea hata, Dominic alilia akitamka maneno matatu tu, ' Nisamehe Sana Grace' ....aliyarudia mara nyingi isiyo na idadi. Nilitoka nikamuacha dommy hapo bafuni nikaenda chumbani kwangu nikachukua kioo cha kushika na mkono ili nijichunguze zaidi sehemu zangu za siri, nilikuta pameongezeka ukubwa, ni kama paliingizwa kitu kikubwa sana, na ndipo nilipofahamu kua yale maumivu ninayoyasikia sehemu zangu za siri yatakua yametokana na kulazimishwa kuingizwa kitu iko, yaani nilichanika kiasi.
Nikakaa kutafakari ni kosa gani nililomfanyia mama mkwe lenye kustahili adhabu hii, mbona nilimuonesha heshima sana, mbona nilimuonesha upendo mkubwa, sikupata majibu hata...Dominic alinifata pale kitandani akainama akaniangalia pia maumbile yangu jinsi yalivyosulubiwa, akanikumbatia kwa uchungu mnooo...
Tulijikuta tunalia kwa pamoja, akanambia nilikusihi usibishane na mamangu Grace, nilikusihi, sikumudu kua na subira tena, yale mafunzo yote niliyopewa kabla ya ndoa jinsi ya kuongea na mume niliyasahau ghafla, hasira ilishika mahala pake, yaani mama ake amenitendea hivi bado anamtetea? Huyu ni mwanaume wa aina gani?
Nilinyanyuka nikapack nguo zangu na za mtoto, Dominic alikua ananiangalia tu hasemi kitu, nilimfata mtoto kwa dada nikakuta ameshamuogesha, nikamwambia dada jiandae tunaondoka, nikaita bajaji tukaondoka kurudi tabata. Nikiwa njiani nikawa nawaza narudi nyumbani kuwaambia nini wazazi, niwaambie ukweli au nifiche, nikisema ukweli nitakua nimeiabisha familia ya mume wangu, nikikaa kimya pia nitakua nazidi kuumia,oh God, haya ni mazito, namwambia nani anipe japo msaada wa mawazo...
Nyumbani tulipokelewa na dada wa kazi, mama alikua kazini. Nilimwambia dada nahitaji kulala , usimwambie mama kama nipo, niliingia ndani ,nikanywa dawa za maumivu na kulala. Ilichukua mda kupata usingizi, ndoto za mara kwa mara za kutisha hazikuacha kunifata, nilipoamka mume wangu alikua amepiga simu mara nyingi sana, akanambia naomba upokee kuna jambo la msingi sana nataka nikwambie.
Sikupokea simu kwakweli, nilikua nina hasira zisizo kifani, mume gani alieshindwa kunitetea , sina mume...sina mume...alipoona sipokei akatuma ujumbe kua amemtuma bodaboda alete ile dawa aliyopewa na mama mkwe pale nje wakati tunaondoka kwa mara ya pili, akanambia hata kama namchukia kiasi gani, ile dawa lazma ninywe, hakuna dawa ya maumivu itakayonipa nafuu, alisisitiza sana ninywe dawa...akaishia kwa kumalizia kua ananipenda sana, amepambana sana kutulinda lakini yaliyotokea yapo nje ya uwezo wake....
Baada ya nusu saa, dada wa kazi akaja akanambia kua kuna bodaboda ameleta bahasha, nikaipokea nikaiweka kwenye begi tulilotoka nalo nyumbani kwangu, jioni ilifika na mama akarudi kutoka kazini, alifurahi kuniona ila akashangaa mbona mekuja jumatatu, vipi kuhusu biashara yangu...si unajua wamama tena, nilijikaza nikamwambia nimewakumbuka tu, ila mama tayari alishajua hapa pana tatizo, hakutaka kunisumbua sana na maswali, usiku ukafika na baba nae akarudi, sikufahamu ni kipi mama alimwambia baba ila hakuniuliza maswali kabisa, mda wa chakula tulikula wote kwa upendo na ibada ya usiku ikaanza kama ulivyo kawaida yetu...
Katikati ya ibada nilianguka, mama akapata hofu sana , akazidisha maombi , nilikuja kupatwa na fahamu baada ya masaa mawili, nikakuta familia nzima ipo sebuleni inaniangalia, sikua na uelewa wa nini kilitokea, lakini maumivu ya mgongo pamoja na kichwa vilinifanya nianze kulia kama mtoto mdogo....
Kwa maelezo niliyokuja kuyapata baadae baada ya kupona, miaka miwili baada ya tukio la ukweni ni kua, ile siku ya maombi ya usiku pale nyumbani hadi nikaanguka, nilipoamka nilikua nalalamika kua naumwa sana kichwa na mgongo, mama na ndugu wengine wakapambana kunituliza, kumbuka hapo hakuna mtu anaejua kuhusu dawa ya maumivu iliyoletwa na mume wangu. Msimuliaji anasema nilikua nalia kama mtoto mdogo, nikaanza kujikuna na pia nikawa nafanya fujo sana, nadhani maombi pamoja na zile dawa nilizofanyiwa usiku vilikua vinapambana...
Nililia hadi nikapoteza fahamu, baba akaona haya yamekua makubwa, wakanibeba hadi hospitali, hali yangu ikizidi kua mbaya mnooo, nilikua kama kichaaa, ili nilale ni lazma nichomwe sindano ya usingizi. Mume wangu alipewa taarifa akafika hospitali mapema tu asubuhi yake, kwa maelezo ya msimuliaji ambae ni dada angu wa kazi, maana mama aliomba aendelee kubaki ili asaidie kulea mtoto kwa sababu alikua amemzoea sana...
Nilikaa katika hali ya kukosa ufahamu kwa mda wa miaka miwili, nilikua kichaa kamili, lakini nilikua chini ya uangalizi hospitali ya muhimbili, mume wangu alipambana nami kwa kipindi chote cha matatizo yangu, hakuwahi kosa Kuja kuniona kila alipopata wasaa wa kufanya ivyo, kwa taarifa tu za ndugu wasimuliaji ni kua mama mkwe wangu hakuwahi kukanyaga hospitali hata mara moja....
Ile ratiba ya kumchukua mtoto kila inapofika birthday yake ilikoma maana mtoto alikua chini ya uangalizi wa familia yangu, kwahiyo ile ratiba ya kuadhimisha birthday kwa namna yao ya kipekee kwa mda wa miaka miwili haikuwepo. Mume wangu ni kama aliisusa familia yake, inasemekana hakukanyaga kwao tangu siku aliposikia kua nimepatwa na kichaa...
Mungu ni mwema baada ya miaka miwili ya maombi , huduma za hospitali na upendo wa wazazi, mume na ndugu wachache, nikawa sawa kabisaaa....mume wangu aliwaomba wazazi wangu anichukue , mama alisita maana akilini mwake alijua zile alama mgongoni alizoziona wakati ananihudumia hospitali zilisababishwa na kipigo toka kwa mume wangu maana hakuna ambae alikua anaujua ukweli wa nini hasa kilitokea...
Mume wangu aliwasihi sana kua haitojitokeza tena amejifunza kutokana na makosa, tulirudi nyumbani na maisha yakaendelea kama kawaida....ilipita miaka mingine mitatu ,nikabahatika kupata mtoto mwingine wa kiume, kijana wangu wa kwanza akiwa mkubwa sasa...mama alikuja kunihudumia palepale kwangu maana mume wangu aligoma nisiende popote akasema atanihudumia yeye mwenyewe...
Nilidhani vita na mama mkwe ilikua imeisha, nilijidanganya Grace mimi...hakika nilijidanganya sana....
Itaendelea....
Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
Fungua uzi boss utupe experience yako mkuu tujifunzeFamilia za kichawi zinahamasisha sana watoto zao waoe mapema wapate watoto halali wa kafala.Naliongea hili kwa uzoefu kabisa.
Mwendelezo lini?Nop....just makusanyo ya yanayojiri kitaa plus mafekeche ya ndugu mwandishi, yaaaap.....tunaishi nazo tu hizi mambo mkuuu
Kama lisaa hivi, nipo naandika wangu...hii kitu natoa kichwani kwaiyo ilibidi nianze kusoma upya nisije walisha matango pori...maana kichwa kina mengi hiki...leo tutapata mwendelezo kipenzi, episode tatu za kushiba munoooMwendelezo lini?
Mwendelezo lini?
umewezea, sema unatakiwa uandike jina kama lilivyo, penye herufi kubwa au nafasi zingatia... kama hapo cute wife imekataa tag umeandika vibaya