Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 2,335
- 3,084
Naona kila mmoja anamnyoshea kidole Kennedy Juma kuwa ndio aliyefanya makosa kwernye lile goli. Pengine Kennedy ana nyota mbaya ya kutopendwa na wanasimba lakini kwa goli la jana halikuwa kosa la Kennedy Juma bali ni la kipa Ayoub. Kipa alitoka golini kwake kufuata mpira pasipo mawasiliano. Alichofanya Kennedy ni kurudisha mpira kwa kipa kwa kichwa na alipiga taratibu tu ili kipa audake ila kipa akatoka eneo lake.
Jana Ayoub alifanya makosa ya aina hiyo mara tatu katika hizo mara tatu mara moja ilikuwa ni faulo, mara ya pili refa akamtetea kwa kusema kachezewa faulo wakati ilikuwa ni mgongano wa wenyewe kwa wenyewe, na mara tatu ikawa ni goli. Lakini kila shabiki wa Simba utamsikia akimshutumu Kennedy kwa lile goli wakati ni kosa la goli kipa.