Mkalukungone mwamba
Member
- Aug 29, 2022
- 69
- 133
Jicho langu:Tabora walinyimwa goli halali kama la Aziz Ki
Klabu ya Tabora united katika mchezo wa jana walinyimwa goli la halali katika mchezo wao waligi kuu ya NBCPL waliocheza na Simba katika Dimba la Azam Complex Chamazi na Simba kuibuka kwa ushindi wa magoli mawili.
Kwa Jicho langu la kimchezo lile lilikuwa goli halali kabisa lakini inawezekana mwamuzi hakuwa na utulivu wa kutazama zaidi kujuwa je lilikuwa goli au sio goli
Lakini pia baada ya tukio hilo Simba wakaanzisha shambulizi la haraka na wakapata goli la pili na kuondoka na alama 3 muhimu kwao
Nikukumbushe tu tukio hilo liliwakuta Yanga katika mchezo wa robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika msimu huu dhidi ya Mamelod kutokea Afrika ya kusini ,goli alilofunga Azizi Ki lilikuwa kama la jana la Tabora na goli lile lilikataliwa licha kulikuwepo na VAR
Sasa kwa mtazamo wangu si lazima tuwe na VAR maana tutachelewa kufika huko ila kwa sasa shirikisho la mpira wa Miguu TFF waongee na Azam Media ambao ndiyo wenye dhama ya kurusha matangazo ya TV ya ligi yetu wapate tv nyingine ambayo atakuwepo mwamuzi katika kuangalia matukio yenye utata .
Hii inaweza kusaidia kwa udogo kupunguza utata katika michezo ya ligi kuu ya NBCPL
anaweza akawepo mwamuzi waziada katika gari la Azam tv la kurusha matangazo na endapo kutatokea utata wa naama yoyote hile basi mwamuzi aliyekuwepo katika gari ya matangazo amsaidie mwamuzi wa kati kufanya maamuzi yaliosahihi .
Lakini hadi sasa bado kumekuwa na matukio yenye utata katika michezo mingi ya ligi kuu inayoendelea na kupelekea kuumiza timu nyingine ,na ukizingatia timu zimewekeza nguvu ,pesa n.k katika mchezo husika halafu mwisho wa siku wanakutana na mambo yasio rafiki kwako katika mchezo kama viashiria vya uonevu.