Sheria na Busara ni mapacha. Mchungaji Mtikila aliwahi kumwambia Rais Mwinyi ‘watamrudisha Zanzibar kwenye jeneza’, hakuitwa mhaini

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,272
47,276
Enzi za utawala wa Mwinyi miaka ya 80, mwanasiasa machachari Joseph Mtikila alikuwa akimuita Rais Mwinyi ni ‘TX’ kutoka Zanzibar na aliwahi kumwambia arudi mwenyewe Zanzibar kabla hajarudishwa kwenye jeneza, hii ilikuwa kwenye mkutano wa hadhara viwanja vya Jangwani kwa waliokuwepo wakati huo watakumbuka.

Kutokana na matamshi hayo, hakufunguliwa kesi yeyote wala kuitwa kituo cha polisi wala kuitwa mhaini.

Kwani sheria za uhaini hazikuwepo, nini kilitumika BUSARA. Ingekuwa leo enzi za Samia ndio katamka hayo maneno nafikiri angenyongwa kabisa hadi kufa.

Sheria na Busara ni mapacha.
 
Mtikila aliandika Waraka na kuusambaza kwny Mkutano Mkuu wa Umoja wa Makanisa 2009 wenye kichwa cha Habari ' Ugaidi wa Jakaya Kikwete', alitoa shutuma nzito nzito dhidi ya Rais nami Alhamdulillah nilipata nakala.

baada ya kuusambaza ma kusomwa sana Jakaya alipotezea tu.

Mbowe kwny Mkutano wa kufunga Kampeni 2015 alisema baada ya kupigwa kura jumapili wanampa Jakaya siku tatu tu za kumtangaza Lowassa kama Rais, ikifika jumatano watavamia Ikulu na kumtoa kwa Maandamano.

Baada ya hapo alirudi Nyumbani akalala na maisha yakaendelea.

Pamoja na makosa yote haya hayahalalishi wengine nao wakosee.

Nawakumbusha tena 1969 Hayati Baba wa Taifa aliwafungulia kesi ya Uhaini akina Hayati Bibi Titi Mohamed, Lifa Chipaka, Christopher Kasanga Tumbo kwa kupinga tu watu kuporwa mali zao kwny azimio la Arusha.

Pamoja na kuzunguka zunguka koote cha Msingi Wanasiasa wachunge ndimi zao kuchochea ghasia kwa kigezo chochote kile.

Akina Mzee Slaa walikosea sana na wengine wasirudie upumbavu huu.
 
Wenye mamlaka ndio wanatuangusha mtu akikutolea maneno makali maana yake ni kuwa kuna ambalo limemchukiza. Sasa wewe hutaki utolewe nishai unataka usifiwe tu haijawahi kuwezekana kokote ulimwenguni zaidi ya bongo.
Hakuna justifications ya kuruhusu watu kuchochea ghasia kwa kigezo chochote kile

Rwanda walipoteza 30% ya Raia wake wote 1994 ndani ya siku 90 tu kutokana na uchochezi kama huu wa Slaa na Wapuuzi wenzie, Taifa lenye watu 3 million lilipoteza watu million moja ndani ya miezi mitatu tu

Amani haina substitute
 
Rwanda ilipoteza sababu gani? Kwanini serikali isi bow down kutuliza tension? Wananchi ndio always wanatishiwa amani tu?
 
Rwanda ilipoteza sababu gani? Kwanini serikali isi bow down kutuliza tension? Wananchi ndio always wanatishiwa amani tu?
Hiyo sababu ndio inahalalisha kuua watu?

hakuna sababu yoyote unayoweza kuileta hapa kuhalalisha kuleta vurugu kwny Nchi

wewe ukitamani kinuke ili upambane na CCM kuna wengine wanasubiri kinuke wakianzishe dhidi ya dini nyingine, wengine wanasubiri kinuke wakianzishe dhidi ya kabila lingine, huku Wakulima wanasubiri wakinukishe dhidi ya Wafugaji, wa Tanganyika dhidi ya Znz n.k

unadhan Taifa lenye diversity kubwa kama hili likivurugike kuna Mkandarasi wa kuja kulirudisha kama awali?

Mtu yeyote akijaribu tu kuvuruga hili Taifa ni halali kabisa avurugwe kwanza Yeye walau hata Watoto wake waishi kwa amani japo watakuwa Yatima
 
Enzi za utawala wa Mwinyi miaka ya 80, mwanasiasa machachari Joseph Mtikila alikuwa akimuita Rais Mwinyi ni ‘TX’ kutoka Zanzibar na aliwahi kumwambia arudi mwenyewe Zanzibar kabla hajarudishwa kwenye jeneza, hii ilikuwa kwenye mkutano wa hadhara viwanja vya Jangwani kwa waliokuwepo wakati huo watakumbuka.

Kutokana na matamshi hayo, hakufunguliwa kesi yeyote wala kuitwa kituo cha polisi wa kuitwa mhaini.

Kwani sheria za uhaini hazikuwepo, nini kilitumika BUSARA. Ingekuwa leo enzi za Samia ndio katamka hayo maneno nafikiri angenyongwa kabisa hadi kufa.

Sheria na Busara ni mapacha.
Christopher Mtikila na sio Joseph
 
Hakuna justifications ya kuruhusu watu kuchochea ghasia kwa kigezo chochote kile

Rwanda walipoteza 30% ya Raia wake wote 1994 ndani ya siku 90 tu kutokana na uchochezi kama huu wa Slaa na Wapuuzi wenzie, Taifa lenye watu 3 million lilipoteza watu million moja ndani ya miezi mitatu tu

Amani haina substitute
Unaonaje mkataba wa bandari??
Umeupenda
 
Hakuna justifications ya kuruhusu watu kuchochea ghasia kwa kigezo chochote kile

Rwanda walipoteza 30% ya Raia wake wote 1994 ndani ya siku 90 tu kutokana na uchochezi kama huu wa Slaa na Wapuuzi wenzie, Taifa lenye watu 3 million lilipoteza watu million moja ndani ya miezi mitatu tu

Amani haina substitute
Hivyo viclip vya kuungaunga na kutengeneza ndiyo uchochezi ?!.

Ukiambiwa utoe sauti yote (clip nzima) utakuta ni kitu tofauti kabisa.
 
Back
Top Bottom