Somoche
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 6,215
- 7,220
Ndg wanabodi sisi wazazi tunatakiwa kuwalinda na kuwaelimisha watoto kadri Mungu anavyotujaalia.Hivi karibuni imeibuka tabia ya hizi shule zinazoitwa English Medium, academy au vyovyote ziitwavyo kulazimisha watoto wa darasa la 4 au la 7 wahamie boarding walale hapo hapo. Kama mjuavyo mtoto wa darasa la 4 wengi wana miaka 9 au 10 ni mtoto ambae bado anahitaji sana uangalizi wa mzazi wake. katika umri huu ni hatari sana kwa mtoto kuhamia boarding na kuishi mbali na wazazi au walezi wake unless mzazi au mlezi ama hujali au una matatizo..
Kibaya zaidi katika hizi shule wanalazimisha ratiba ngumu na katiri sana kwa watoto mtoto wa darasa la 4 analazimishwa kuanza kusoma saa 12 asubuhi hapo anapambana na marathon mpaka saa 11 baada ya hapo atapumzika kidogo saa 1 anaingia tena kusoma mpaka saa 3 usiku.Huu ni ukatiri ..huu ni uuaji wa watoto sio haki NAOMBA SERIKALI IINGILIE HILI JAMBO.
Wazazi mnaambiwa kama hutaki mhamishe au mfikishe shule saa 11 alfajiri umbebe saa 3 usiku. Vyovyote iwavyo kama umesoma unaelewa kichwa cha mwanadamu hakiwezi kuhimiri mshindo mkubwa wa kusoma mfululizo kwa umri huo mdogo mpaka ssaa 3 usiku ndio mana natoa wito Wizara ya Elimu chonde pigeni marufuku watoto wadogo kukandamizwa na shule hizi binafsi ili tu wapate No ya juu kwa ajili ya maslahi ya kutangaza biashara na jina la shule..Elimu haipaswi kuwa biashara hii inafanywa kibiashara...