Revolution
JF-Expert Member
- Feb 28, 2008
- 795
- 571
Habari ndugu zangu kuna tatizo kubwa katika hili suala nililowasilisha hapo juu. Shule nyingi kuanzia chekechea hadi kidato cha sita zina matatizo makubwa haswa zile zinazotoa ufaulu wa kiwango cha juu. Wanafunzi wanaamka saa nane na wanalala saa saba usiku ili wakeshe madarasani wakariri. Mwisho wa siku tukienda kwenye majadiliano ya kimikataba tunashindwa kujenga hoja. Mzazi una hela na bado unalipa na mtoto anateseka kwa kuamka saa nane usiku ili shule ipate A zote. Tunawaumiza vijana wetu.