SoC04 Serikali iweke mpango wa uanzishwaji wa Lugha ya alama kwa shule zote nchini

Tanzania Tuitakayo competition threads

Angyelile99

Member
Oct 9, 2023
79
147
UTANGULIZI

Pamoja na uwepo wa jitihada za serikali katika kutoa elimu maalumu kwa watu wenye matatizo ya kusikia na kuzungumza, rakini bado kumekua na changamoto mbali mbali ambazo haswa zimekua zikitokana na kukosekana kwa lugha ya pamoja kati ya watu hawa na jamii inayo wazunguka hivo hupelekea kuto aminiwa, kutopewa nafasi za kimaamuzi, kuto thaminiwa na kukosa ushawishi wa kimaendeleo kutokana na kukosekana kwa hamasa ya watu wanao wazunguka na kisha kuishia kua tegemezi.

Hivo basi ili kuepukana na haya yote juu ya watu wenye changamoto ya kusikia na kuzungumza. Serikali kupitia wizara yake ya elimu kuna haja ya uanzishwaji wa elimu ya lugha ya ishara kwa shule zote hapa nchini, itakayo jenga kizazi na kutoa fursa ya kuwasogeza watu wenye changamoto hizi karibu zaidi na jamii zao kwa sababu ya uwepo wa lugha itakayo weza kuwaunganisha baina ya makundi haya mawili. Kupitia mpango wa elimu hii. Kutakua na athari chanya kazaa, haswa kwa kundi la watu wasio weza kusikia ama kuzungumza, na athari hizo ni kama ifuatavyo;

1: Kutoa fursa sawa: Kuwa na somo hili katika shule za watu walio na uwezo wa kusikia na kuzungumza kunaweza kusaidia uhakikishwaji wa fursa sawa katika nyanja ya kijamii, uchumi ama siasa kwa makundi yote mwili. Kwa mfano kutoa ajira kwa watu wenye changamoto za kusikia na kuzungumza na kua sehemu ya watumishi wa umma kwenye jamii ya watu wasio kua na changamoto hizi. Hii itakua ni kwa sababu tutakua tumejenga kizazi chenye uelewa mpana wa lugha ya alama na ishara kutokana na uanzishwaji wa elimu hii kwa shule zote hapa nchini itakayo saidia uraisishwaji wa mawasiliano

2: Kuimarisha mawasiliano na kuwaleta zaidi pamoja watu wenye changamoto hizi na wasio kua nazo: Somo la lugha ya ishara litawawezesha wanafunzi walio na uwezo wa kusikia na kuzungumza kujifunza lugha ya ishara ambayo itawawezesha kuwasiliana vizuri na wenzao wenye changamoto hizi wanao patikana katika jamii zetu. hivo itasaidia kuondoa tabaka na kuleta usawa zaidi baina ya makundi haya mawili.

3: Kukuza ufahamu, uelewa na Kujenga utamaduni wa kuheshimiana: Wanafunzi wa kawaida wasio na changamoto ya kusikia wala kuzungumza watapata ufahamu zaidi juu ya changamoto za watu wasio na uwezo wa kusikia na kuzungumza, watajifunza kuheshimu tamaduni zao na kuondoa ubaguzi wa aina yoyote. Na kuleta jamiii ya watu wenye kutambua thamani ya watu wenye changamoto hizi.

4: Kukuza uelewa wa teknolojia: Itatoa nafasi ya watu wenye changamoto ya kusikia na kuzungumza katika matumizi ya teknologia ya mawasiliano kama vile barua pepe, simu za mkononi, mawasiliano ya njia ya watsup, Instagram, twitter na mitandao mingine ya kijamii katika lugha ya ishara na watu wao wa karibu ambao wanauwezo wa kusikia na kuzungumza kwani kila mmoja atakua anaweza kutumia lugha ya ishara kwa ufanisi.

5: Kuleta ushindani wa kimaendeleo baina ya makundi haya mawili: katika suala zima la uanzishwaji wa elimu ya lugha ya ishala kwa shule zote nchini itasaidia kuibua nafasi ya kiushindani katika fursa tofauti tofauti kwa sababu kila mmoja baina ya makundi haya atakua na nafasi saawa ya kuaminiwa na kuthaminiwa katika jamiii bila ya kuzingatia tofauti walizo nazo.

6: Kuongeza ujuzi wa lugha kama ilivyo kwenye lugha nyinginezo: kama ilivyo ada katika mitaara yetu ya elimu inayo ruhusu wanafunzi kujifunza rugha mbali mbali kama vile kiingereza na kifaransa. Pia uanzishwaji wa elimu ya lugha ya ishara, itasaidia wanafunzi kujiifunza lugha nyingine ya mawasiliano ambayo itawawezesha kuwasiliana na jamii ambayo inatumia lugha hiyo.

7: Kuwapa uwezo watu wenye changamoto ya kusikia ama kuzungumza kushiriki moja kwa moja katika masuala ya kijamii: Uwepo wa lugha ya ishara utawawezesha kujenga jamii ya watu watakao kua wanaelewa lugha ya ishara itakayo weza kusaidia watu wasio na uwezo wa kusikia na kuzungumza kushiriki katika shughuli tofauti tofauti za ujenzi wa jamii, kwa kiwango ambacho ni sambamba na ambavyo watu wenye uwezo wa kusikia na kuzungumza wamekua wakishiriki.

8: Ushirikishwaji wa watu wenye changamoto za kusikia na kuzungumza katika nafasi za uongozi: Uwepo wa elimu hiii ya lugha ya ishara kwa wanafunzi wasio na changamoto hizi itasaidia kujenga kizazi ambacho kitakua na uwanda mpana wa lugha. Ambapo itaweza kusaidia kutoa nafasi kwa watu wenye changamoto hizi kushiriki katika nafasi mbali mbali za uongozi kwani tayari watakua wamezungukwa na jamii ya watu wanao weza tumia lugha ya ishara na kuleta maelewano.

9: Kuondoa migongano baina ya makundi haya mawili: bado kumekua na changamoto ya kukosekana kwa mshikamano wa moja kwa moja baina ya kundi hili maalumu na jamiii ya watu wanao wazunguka katika maisha ya kila siku kama vile maswala ya ndoa, uchumba, udugu, jamaa na masuala mingine ya kila siku katika maisha kwa sababu ya kutokuwepo kwa lugha inayo weza kubeba hisia za kundi hili kwa watu wenye uwezo wa kuzungumza na kusikia hivo upelekea migongano na kukosekana kwa umoja baina ya makundi haya mawili. Na mwishoe watu wenye changamoto hizi huishia kutengwa na kunyanyapaliwa.

10: Uraisishwaji katika upatikanaji wa wataalamu wa lugha ya ishara: kupitia mpango huu wa uanzishwaji wa elimu hii kwa shule za umma zote nchini, utasaidia moja kwa moja uwepo wa kizazi cha jamii ya watu wenye taranta ya kuzungumza lugha hii. Hivo kuwapa nafasi ya kubobea kiundani zaidi katika nyanja hiii na kufanya uwepo wa wakufunzi wabobevu wa lugha ya ishara kwa wingi

11: Uwezeshaji wa maendeleo binafsi kwa watu wenye changamoto ya kusikia na kuzungumza kupitia kuajiliwa ama kujiajiri: Katika maisha ya karne ya 21. Maendeleo ya kiuchumi yamekua yakiibuka kwa watu kuishi kwa kutegemeana. Hata hivi utoaji pia wa elimu ya lugha ya ishara kwa shule zote nchini itasaidia kua na kizazi ambacho kutakua na mzunguko wa fulsa zitakazo husisha makundi yote bila kujari tofauti zao kama vile kuajili watu wenye changamoto hizi katika nafasi mbali mbali. na aidha kutoa hamasa ya kujiajiri kwasababu lugha ya ishala itatumika kama kiunganishi baina ya makundi yote haya mawili.

Kwa ujumla: Kupitia mpango huu wa uanzishwaji wa elimu hii. Moja kwa moja somo hili linaweza kuanzishwa aidha kwa kuanzia ngazi ya sekondari ama kuanzishwa kwa kuanzia ngazi ya msingi.
 
Kuimarisha mawasiliano na kuwaleta zaidi pamoja watu wenye changamoto hizi na wasio kua nazo: Somo la lugha ya ishara litawawezesha wanafunzi walio na uwezo wa kusikia na kuzungumza kujifunza lugha ya ishara ambayo itawawezesha kuwasiliana vizuri na wenzao wenye changamoto hizi wanao patikana katika jamii zetu. hivo itasaidia kuondoa tabaka na kuleta usawa zaidi baina ya makundi haya mawili.
Naam, kila mmoja anayo haki ya kusikia na kueleza maoni yake.

Sema nimewaza kitu kimoja, hivi macelebrity hawawezi kweli kutumika kuipa kiki lugha ya ishara. Mfano kwenye video zao kuwe na vipengele vinatafsiriwa na watu wa ishara. Wazo tu.
 
Naam, kila mmoja anayo haki ya kusikia na kueleza maoni yake.

Sema nimewaza kitu kimoja, hivi macelebrity hawawezi kweli kutumika kuipa kiki lugha ya ishara. Mfano kwenye video zao kuwe na vipengele vinatafsiriwa na watu wa ishara. Wazo tu.
Ni kweeli tunahitaji kua na jamii inayo weza kutumia lugha ya ishara. Ili kurahisisha uduma kwa watu wenye changamoto za kusikia na kuongea nakuleta usawa baina yetu sote
 
Back
Top Bottom