SoC02 Serikali ipige marufuku shule za bweni za msingi na maandalizi. Shule za bweni zianze elimu ya upili na kuendelea

Stories of Change - 2022 Competition

desneol

New Member
Aug 8, 2022
4
10
Hakuna maisha bora na ukuaji sahihi kwa mtoto kama kuwa karibu na mama, baba na nduguze wakati wa ukuaji.

Kumbukumbu nyingi, hali ya kujiamini, kuona mapenzi ya hali ya juu ya wazazi katika umri huu mdogo unaemjenga mtoto kuwa mwenye furaha na mapenzi kwa nduguze, wazazi, majirani na kuthamini watu wengine.


Umri huu unamjenga mtoto kujua thamani ya ubinadamu nje ya mafanikio ya kiuchumi na kifedha.

Usimkoseshe mtoto wako jambo hili kubwa la kulala chini ya dari moja na wewe kwa umri wa kutosha mpaka muda muafaka.

Mtoto mwenye furaha na uwezo mkubwa wa kutatua matitizo yake ni yule anaejua thamani ya upendo na utu sio thamani ya muda tu na kufanya vizuri zaidi ya wengine, huyu mtoto anajifunza haya kwa kuona akiwa mdogo kwa wazazi na jamii iliyomzunguka.

Mtoto atakaekuja kuwa kiongozi bora anatoka kwa wazazi bora sio shule bora.

Shule za bweni zina faida hilo sipingi, zinamjenga mtoto kuanza kujitegemea mapema na kuweza kutatua matatizo yeye mwenyewe mapema hivyo inamsaidia kupamabana na kuwa jasiri sana.

Maswali ya kujiuliza;

Je, ni sahihi kumfundisha haya mtoto wa miaka 9?
Je, huko ni kumjenga ama kumbomoa?
Je, ukuaji sahihi unatakiwa kupitia hatua hizi mapema?
Je, upi ni umri sahihi mtoto kuanza kujifunza kujifanyia mambo mwneyewe na ustahamilivu wa maisha?
Haya yote ni mambo mema kuyafahamu swali ni je umri chini ya miaka 12 ni umri sahihi kwa haya?
Je, mbona tunamfundisha mtoto hatari ya dunia kabla hajahitimu kujua ladha ya mapenzi ya dunia?

Je, hakuna jambo la thamani zaidi kuliko matokea mazuri shuleni na kuongea kwa ufasaha lugha za ng'ambo?
Je, shule za bweni ni njia wazazi walio na kazi nyingi kukimbia majukumu yao ya msingi ya malezi?
Je, jamii inahitaji nini zaidi kwa mtoto wako, kiingereza na daraja la kwanza au mtoto mwenye kuijua vizuri jamii na kuzijua thamani halisi za jamii?


Ukuaji wa mtoto hauhitaji shule nzuri tu bali unahitaji wazazi wema karibu nae muda wote.

Ni unyanyasaji na uporaji wa ngazi ya juu sana kumpeleka mtoto shule ya bweni akiwa elimu ya msingi.


Mtoto mdogo akizaliwa anaanza kunyonya ziwa la mama ake pekee kwa takribani miezi 6, bila hata ya kunywa maji, mpaka atimiapo miezi 6 anaanza kidogo kidogo chakula laini pamoja na maziwa ya mama, afikapo miaka miwili sasa kwa kiasi anakula chakula cha kawaida ila pia sio sawa na mtu mzima sababu mtoto hula mara nyingi zaidi na virutubisho vinavyohitaji katika ukuaji bora.

ukimlisha mtoto aliezaliwa leo ugari sio kuwa atahshiba vizuri bali utampa maradhi makubwa au hata kupoteza maisha, hili ni sawa kumpeleka shule ya bweni mtoto mdogo anaehitaji kuwa na wazazi wake tunatengeneza jamii yenye maradhi yanayo ua taifa letu.


Huu ulaji wa mtoto unatufundisha kuwa mtoto mdogo anahitaji hatua za ukuaji sio katika chakula tu bali pia kinachohifadhiwa katika ubongo wake.

huwezi kumpeleka mtoto mdogo shule ya bweni kwa ajili ya kujifunza utu, mapenzi, thamani ya familia?haya anajifunza nyumbani.


Hata kama walimu ni wenye mapenzi kiasi gani ila hawawezi kufikia mapenzi ya wazazi kwa mtoto yule.

Ni unynyasaji wa mtoto na uporaji wa hali ya juu kwa mtoto kumpeleka shule ya bweni akiwa bado mdogo, unampora haki ya mapenzi ya wazazi.

Mambo yafuatayo ni muhimu sana kwa mtoto kuyajua kabla hajajiunga na shule ya bweni.

Awe na uhusiano imara sana na wazazi wake.
Awe ana uwezo wa kujieleza vizuri hisia zake bila woga.
lazima aelewe utambulisho wake, imani na misingi ya imani yake, tabia na thamani ya jamii yake.

Awe anajua kitu sahihi na nini sio sahihi kutokana na mila, imani, sehemu na familia aliotoka na mwenye uwezo wa kuyatetea haya akiona hayatimizwi sababu anajua kwanini yake juu ya hayo na thamani ya kile anachoamini.

Je! haya yote tunayaweza kuyapata kwa mtoto mdogo?
Haiwezekani! Sababu hayo hujengwa nyumbani.


Huyu mtoto akirudi nyumbani huwa anachanganyikiwa nini cha kufuata, zile za shuleni au zile za nyumbani?

Shule anajua muda ni kila kitu, ila nyumbani wanasema unapaswa kujitoa muda wako kwa ajili ya wengine.

Shule anajua kufauli mtihani ndio inaleta thamani yake kwa wenzake walimu,na shule, nyumbani wanasema kufanikiwa au kutofanikiwa haipunguzi au kuongeza thamani ya uto wako.

Shule usipolipa ada unarudi nyumbani kwa maana pesa ndo kila kitu, nyumbani wanasema utu ni bora kuliko kitu.

Mitihani ya darasani inamjenga kuwa mshindani ila akiwa nyumbani atajifunza kuwa ushindani sio mbaya ila uwe na upendo ndani yake.

Mtoto mdogo aliekosa kukua akiwa na wazazi atayachukua ya shule ambayo kiukweli hawafundishwi hivyo ila mazingira ya kiushindani na matokea yanamjenga kuamini hivyo.

Je, jamii inatengeneza watu wanaojali muda zaidi kuliko kujitoa na wenye kuona fedha ni kitu muhimu zaidi hata kuliko utu?

Sisemi kuwa shule za bweni sio nzuri HAPANA., Ninachosema shule za bweni anatakiwa aende mtoto aliehitimu malezi ya wazazi na kujitambua yeye ni nani ili awe mwenye ufaulu bora na thamani yake katika jamii.

Naomba waziri wa ustawi wa jamii akae na wapanga sera za elimu wakae na kujadili hili.
Shule za bweni kwa watoto ya elimu ya upili ni bora kwa sababu mtoto atakuwa tayari anaelewa yeye ni nani na imani na mila za familia zake kwa umri huu ni sahihi kabisa kuanza kujifunza kujitegemea.



MALEZI YA WAZAZI YANAYOFUATIWA NA SHULE ZA BWENI NI MUUNGANIKO BORA ZAIDI KWA JAMII YETU YA BAADAE

Napendekeza shule za bweni za kwa elimu ya maadalizi na msingi zisiwepo kabisa.

Wazazi watambue umuhimu wa uwepo wao katika ukuaji wa mtoto una thamani zaidi kwa mtoto kuliko kumpeleka international boarding school.

Naomba waziri ustawi wa jamii na wenye kupitia miongozi ya elimu walione hili.

Sina neno na wamiliki wa shule ila jamii yangu ya baadae ndo naiwazia.

ahsante sana.
desnoel.
 
Shule za bweni kwa watoto ni vyuo vya usagaji na ushoga, bweni iwe kwa wanafunzi ambao wanalazimika kutembea umbali mrefu kwenda shule vijijini. Watoto wadogo wanabakwa sana na wenzao wa madarasa ya juu, hususani ukiwa wanaita mtoto wa mama. Matrons na patrons hawana uwezo wa ku control watoto wengi kwa wakati mmoja na kama tulivyosoma ktk magazeti hao hao ndiyo wamekuwa madalali wa kuwauza watoto wadogo wa kiume walawitiwe. Ni dhana potofu kudai mtoto akiwa boarding ndiyo atasoma kama mtoto mzembe ni mzembe tu hata aende boarding na kama ana bidii atakuwa nayo tu chini ya uangalizi wa wazazi bora
 
Kuna hiyo shule moja huko Dodoma, bweni lake lilikuwa halijamalizika kujengwa vizuri. Asa kuna mtoto wa darasa la tatu wa kiume alikuwa anaoga bafuni, akawa anateleza , kuangalia huku na huku akaona sehemu pekee ya kujishkiza ili asianguke ni bulb ilikuwa imening'inia kwa waya , vile viwaya vinavyoshikiliaga bulb. Mtoto wa watu akapigwa shoti hapohapo bafuni akapoteza maisha . Imagine.
 
Serikali ishikilie hapo hapo ili kuwapa watoto haki ya kukaa na wazazi wao ila pia kuwakinga na dhuluma wanazofanyiwa huko mabwenini.

Wengi wa walezi wa watoto hawa mabwenini ni watu wa hovyo sana.
 
When the story of change carried out, tayari serikali imepiga marufuku boarding school kwa wanafunzi wa chini ya darasa la nne
Cudos Sana kwa mhariri, what ever hakubahatika kuwa mshindi Ila wazo lake limekubalika at high level na haikuwa zali kuwa miongoni mwa content za STORY OF CHANGE
 
Back
Top Bottom