Ni lini Rostam Azizi aligundua na kukubali kuwa siasa za Tanzania na hasa CCM ni za 'uchwara' yaani gutter politics? Na nini hasa tafsiri yake ya 'siasa za uchwara? Kupitia hotuba yake ya kujiuzulu, Rostam Azizi ametangaza kuachana na Ubunge pamoja na nafasi yake NEC lakini atabakia kuwa mwanachama wa ccm. Kama kweli nia ni kuachana na siasa za uchwara (whatever that means) kubakia kuwa mwanachama wa chama cha siasa tena chama ambacho alikuwa kiongozi kunamtenganishaje yeye Rostam na siasa uchwara? He is still drinking the same contaminated soup which made him sick in the first place so huu utakaso anaotangaza ataupataje?