Punguza unywaji wa pombe, ukiweza acha kabisa

Hatuwezi kupangia watu waishi vipi kikubwa kila mmoja ashikamane na anachoona kinamfurahisha akiona kuna uwezekano wa kuachana nacho ataacha mwenyewe akiona hawezi ataendelea nacho so kama kuna shida itakuja huko mbeleni itakuwa ni yeye na nyumba yake.

Binafsi ni muumini wa kusikiliza shauri mbalimbali,ushauri wa kutogusa pombe alinipa mjomba wangu (deceased) mwaka 2002 na bado nauishi.
 
Maneno kuntu haya, yanamgusa mywaji yoyote.

Screenshot_20240423-191037_Facebook.jpg
 
Hizi maneno wakati tunaishi kwenye jamii watu wanapiga game na wanaenda miaka 90+, wakiwa wapo na afya imara naona mnatuchanganya tu.

Wanavyoileta utadhani kila mnywaji atapata hayo madhara kumbe ni 2/10 labda.

Endeleeni kufanya utafiti sasa 75mls za konyagi zinafanya nini 😀
Kwa saivi watu wengi wanakufa kwa kushtukiza na Magonjwa ya ajabu, unashangaa Leo mtu mzima kesho unaambiwa amezidiwa kafa, hivi vifo vya kushtukiza mara nyingi inatokana na mtu kutumia vilevi kwa Mda mrefu so inafka mda Viungo vya mwili vina'fail ghafura. Kwahiyo usitimie hizo narrative zako kuhitimisha kuwa Haina madhara, yawezekana Leo usiyaone ila for long time or short time utayaona tu, pombe madhara yake ni makubwa mno na Nina watu wengi ninaowajua ambao waliendekeza hivyo vilevi lakin Leo hatunao.
No one alive forever but kujali afya zetu mhimu zaidi.
 
Madhara ya pombe ni makubwa sana kuliko wengi wanavyofikri.Mimi niko kwenye tiba kwa miaka kadhaa sasa,magonjwa mengi yanayowasumbua watu ni yale ya mtindo wao wa maisha ikiwemo unywaji wa pombe kupindukia.
Wewe unayedharau na kupuuza ujumbe huu ambao umekufikia bure kabisa bila malipo ni wazi kuwa afya ya akili haiko sawa pia.Ulipaswa kumshukru Mungu kwa kukumbushwa jambo lililo jema katika maisha yako na familia yako kwa ujumla.

Mungu aendelee kutulinda
 
Tunaomba mtuletee takwimu zilizo kamilika ni kwa kiasi cha asilimia ngapi pombe inasababisha vifo? Ikifika 0.000001% naacha kunywa...tofauti na hapo peleka mavi yako hukoo
 
Madhara ya pombe ni makubwa sana kuliko wengi wanavyofikri.Mimi niko kwenye tiba kwa miaka kadhaa sasa,magonjwa mengi yanayowasumbua watu ni yale ya mtindo wao wa maisha ikiwemo unywaji wa pombe kupindukia.
Wewe unayedharau na kupuuza ujumbe huu ambao umekufikia bure kabisa bila malipo ni wazi kuwa afya ya akili haiko sawa pia.Ulipaswa kumshukru Mungu kwa kukumbushwa jambo lililo jema katika maisha yako na familia yako kwa ujumla.

Mungu aendelee kutulinda
Wewe una matatizo yako mengine unajaribu kujitetea kwa kujificha kwenye kivuli Cha pombe!
Unabisha?
 
TAMBUA UNYWAJI SAHIHI WA POMBE

Kitu cha msingi kwenye pombe siyo kujua aina ya beer au kilevi. Kitu cha msingi ni kujua percentage of pure alcohol (asilimia ya pombe halisi) na ujazo wake ( volume).

Unit moja ya pombe ni sawa na 10mls of pure alcohol or 8g of the same. Mwanaume hutakiwa kunywa unit 3 za pure alcohol na mwanamke 2 kwa siku( standard units)

Mfano , let say una kinywaji cha pombe(mzinga) umeandikwa 40 percent na ujazo labda 500mls. Hiyo asilimia 40 ni pure alcohol ya ujazo . Ukizidisha mara 500mls unapata 200mls za pure alcohol. So kwenye mls 500 only 200mls are pure alcohol
Kama unit moja ya pure alcohol Ina 10mls za pure alcohol , katika 200mls tulizopata zitakuwa na unit 20 za pure alcohol ( chukua 200mls gawanya kwa 10mls).

Je ,kiasi gani unywe kwa mzinga huo ?

Ni rahisi sana ! Ikiwa unit 20 za pure alcohol zina ujazo wa mls 500 , je unit 3 kwa mwanaume ujazo utakuwaje ?
Jibu 500mls zidisha mara 3 gawanya kwa 20. (75mls )
So utakunywa mls 75 tu kwenye mzinga huo sawa na vifuniko 3 vya mls 25 vya kwenye chupa ya dawa za syrup.

Kumbuka! Pombe huzuia uchomaji wa chakula cha wanga na mafuta kwa zaidi ya saa 72 na kupelekea ongezeko la Uzito, vitambi ,ini kujaa mafuta ( alcoholic fatty liver diseases ) na insulin kinzani ( insulin resistance) , hivyo kuwa katika hatari ya kisukari na shinikizo kubwa la damu.

Ukiweza usinywe pombe kutokana na kusisimua ubongo kwenye eneo la madawa ya kulevya ( mu opioid receptor ) hivyo kusababisha utegemezi ( dependency)

Jinsi pombe inavyoathiri mwili wako

1. Ubongo wako: Pombe hata kiwango kidogo, husababisha madhara yasiyorekebishika kwenye seli za ubongo;baadhi hufa na zingine hubadilika.

2: Moyo wako: Pombe huongeza hatari ya shinikizo la damu, kiharusi, na kudhurika kwa misuli ya moyo.

3: Mapafu yako: Pombe huhafifisha shughuli za upumuaji.

4: Mfumo wako wa uzazi: Kwa wanaume pombr inaweza kuharibu seli za testesi,zikisababisha upungufu wa nguvu za kiume,kushindwa kuzaa na huenda kuongezeka kwa matiti.Kwa wanawake pombe inaweza kusababisha mvurugiko wa mzunguko wa hedhi na ovari kushindwa kufanya kazi.Pombe pia imehusianishwa na kasoro za kuzaliwa kwa watoto na matatizo ya ubongo.

5: Ini lako:Kwa sababu ini lako lazima lichuje pombe kutoka kwenye damu,pombe huathiri ini kuliko kiungo chochote katika mwili wako.
~Kalori za ziada katika pombe huhifadhiwa kama mafuta kwenye ini.
~Seli za ini zinazofanya kazi hufa kutokana na sumu kwenye pombe.
~Tishu za makovu huchukua nafasi ya seli zilizokufa,zikisababisha kuharibika kwa ini.

6: Mfumo wako wa kinga: Pombe hudhoofisha kinga ya mwili dhidi ya maradhi.

7: Ongezeko la saratani:Koromeo,Umio,Ini,Matiti kwa wanawake,Tumbo,Kongosho,Utumbo mkubwa,Rektamu,Tezi dume,Yai,Mfuko wa uzazi na mfuko wa mkojo.

Kumbuka kinga ni bora kuliko tiba!!
sawa kiongozi. ila sasa nawewe utusaidie majibu ya maswali aya machache.

tuseme leo watu woote tuache gambe kodi ya serekale itatoka wapi?

barabara shule na haya madaraja unayopita yatajengwa kwa ela kutoka wapi?

viwanda vya pombe vimeshilia ajira za makumi kwa maelfu ya watz wenzetu. sasa wakifunga ivo viwanda hawa walioajiliwa wanaenda wapi?

BTW una habari pombe ndo inaongozea kila mwaka kutuletea kodi ya kueleweka?
 
Hatuwezi kupangia watu waishi vipi kikubwa kila mmoja ashikamane na anachoona kinamfurahisha akiona kuna uwezekano wa kuachana nacho ataacha mwenyewe akiona hawezi ataendelea nacho so kama kuna shida itakuja huko mbeleni itakuwa ni yeye na nyumba yake.

Binafsi ni muumini wa kusikiliza shauri mbalimbali,ushauri wa kutogusa pombe alinipa mjomba wangu (deceased) mwaka 2002 na bado nauishi.
Kuacha pombe napo ni mtihaniiii.... Ngoja tujaribu Tena .... Niliacha kama miezi sita aseee Kasi niliyorudi nayo ni ya hatari....
 
Back
Top Bottom