Kijana acha kunywa pombe za bei rahisi

Gulio Tanzania

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
2,193
4,647
Kutokana na hali ya uchumi kuwa mgumu vijana wengi wameangukia kwenye unywaji wa pombe za bei rahisi zinazolewesha haraka kama sungura, master, jogoo nk.

Ukiwa mtumiaji wa hizi pombe huwezi kufanikiwa kimaisha, hizi pombe zinapunguza uwezo wa kufikiria Kuna wengine wanakunywa hizi pombe za kienyeji kama komoni, ulanzi, choya, mnazi hizi ndio usiguse kabisa hata kama umeenda kusalimiwa ndugu zako huko kijijini kwenu usijaribu kugusa pombe hizi.

Sababu gani? Unavyokunywa pombe za kienyeji moja kwa moja unaunganishwa kwenye kufanya ibada za mizimu hivyo kukufunga kabisa kutoka kwenye umasikini.

Tazameni huko mitaani kwenu Hawa watu wanaotumia pombe hizi kama huwa wanabadilika, miaka na miaka wapo vile vile, wanafanya kila kazi lakini hawajawahi kutoboa!

Hata kama unapitia hali ngumu usishawishike kutumia pombe za bei rahisi.
 
Kutokana na hali ya uchumi kuwa mgumu vijana wengi wameangukia kwenye unywaji wa pombe za bei rahisi zinazo lewesha haraka kama sungura,master, jogoo nk ukiwa mtumiaji wa hizi pombe huwezi kufanikiwa kimaisha hizi pombe zinapunguza uwezo wa kufikiria Kuna wengine wanakunywa hizi pombe za kienyeji kama komoni,ulanzi,choya,mnazi hizi ndio usiguse kabisa ata kama umeenda kusalimiwa ndugu zako huko kijijini kwenu usijaribu kugusa pombe hizi

Sababu gani ? Unavyokunywa pombe za kienyeji moja kwa moja unaunganishwa kwenye kufanya ibada za mizimu hivyo kukufunga kabisa kutoka kwenye umasikini tazameni huko mitaani kwenu Hawa watu wanaotumia pombe hizi kama huwa wanabadilika miaka na miaka wapo vile vile wanafanya kila kazi lakini hawajawahi kutoboa hata kama unapitia hali ngumu usishawishike kutumia pombe za bei rahisi
Sasa vijana wa chadema watapata vipi mzuka waandamane na Sultan?,acha wapige visungura tu wanachadema
 
Ogopa sana pombe ambayo uwe na hela au huna hela utakunywa tu ...

Ni pombe ambayo hata bure unaipata tu
 
Ogopa sana pombe ambayo uwe na hela au huna hela utakunywa tu ...

Ni pombe ambayo hata bure unaipata tu
Kuna siku nilikuwa duka moja jamaa mmoja alikuja pale dukani anakawa anataka nusu kuku nikawa sielewi jamaa alipimiwa nusu sungura ikabidi nimuulize muuza duka huyu mteja anauliza kuku dukani muuzaji alibaki kunicheka tu
 
Back
Top Bottom