Peter Kibatala: We need a Police to Police the Police

Mkuu naunga hoja Kibatala na ya kwako. Pamoja na hayo nami napendekeza yafuatayo:

1. Muundo wa polisi ubadilishwe uwe ni wa kuhudumia wananchi. Badala ya kuwa police force ya mkoloni iwe police service ya kisasa.

2. Jeshi la polisi la sasa ligawanywe katika sehemu mbili zinazo jitegemea. Pawepo na huduma ya polisi na huduma ya upelelezi inayojitegemea kimuundo, kiuongozi, kimamlaka na kiutendaji

3. Polisi waboreshwe maslahi yao, angalau yakuweza kukimu/kumudu maisha ya sasa badala ya kutuma upolisi wao na bundiki kuendesha maisha yao. Huu ndio mzizi wa rushwa ndani ya polisi.

4. Askari polisi wote na vitengo vyao waishi kambini. Kambi zao ziboreshwe za kufaa kuishi binadamu. Ila askari upelelezi ndio waishi mtaani /changanyikeni/uraiani maana shughuli zao zinataka hivyo.

5. Katika mafunzo yao, mbali na mazoezi pawepo na somo la lazima la uelewa wa sheria, katiba, muongozo wa polisi na haki za raia kwa kila askari.

6. Kwa upande wa askari upelelezi pawepo na ukomo wa muda wa upelelezi, muda usizidi miezi 3, vinginevyo mahakamani ndio iongeze muda iwapo pana ulazima na usizidi miezi 3.

7. Katika zoezi lolote la ukamataji wa raia, raia yeyote wa jirani aruhusiwe kuchukua video ya tukio zima, video hiyo itumike kama sehemu ya ushahidi mahakamani ya mwenendo wa askari katika ukamataji na kusimamia haki ya raia.

9. Polisi wapewe vitendea kazi muhimu kama magari, pikipiki, fenicha, stationery na kadhalika kwa wakati ili kutimiza majukumu yao kwa ueledi bila ubabaishaji kama ilivyo sasa.

10. Ofisi, choo na mahabusi za polisi ziwe na hadhi nzuri kwa design, rangi na space. Hii itawamotivate askari kutenda haki. Majengo mengi ya polisi ukifika tu, unajua haki huipati! Nyingi ni mahabusu za kikoloni. Pia pawepo na vituo vya polisi kila ilipo ofisi ya serikali ya mtaa ili kurahisisha huduma.

11. Polisi iwatumikie raia wote kwa usawa. Jeshi la polisi lifuate sheria. Lisiwe jeshi la chama tawala lilojaa upendeleo. Ambalo kila askari ni mwanachama chama wa chama hiko na kusimamia ilani na sera za chama hicho. Lisiegemee upande wowote wa siasa.

Pawepo na clear separation.

12. Pawepo na muangalizi huru na maalum wa polisi ambaye kwa maoni yangu aweze kupokea malalamiko ya raia dhidi ya polisi, kuchunguza na kukarapia na kusimamisha askari yeyote kazi. Hii italeta nidhamu kwa askari dhidi ya raia.

13. Mwisho pawepo na utaratibu wa kila baada ya miaka 10, kupitia na kuoverhaul jeshi la polisi ili liweze kuendana na muda na mazingira ya dunia ya wakati huo.

Nawasilisha!
Kwani humu Jamiiforums, Jeshi la Polisi halina Special thread kama TRA, TANESCO AU DAWASA?
 
Kwani humu Jamiiforums, Jeshi la Polisi halina Special thread kama TRA, TANESCO AU DAWASA?
Hawana ubavu huo wa kuweka thread ya namna hii humu. Wanajijua walivyo, usifikiri kwamba hawaifahamu 'image' yao jinsi ilivyo.
Wao wenyewe mtu binafsi mmoja mmoja Wana account zao humu, Mambo yote yanayojadiliwa humu mitandaoni wanayaona na kuyasoma.
 
Polisi Tanzania ni aibu kubwa kabisa. Ina maana jeshi lote limejaa wajinga tu? Hakuna angalau watu wenye ku reason kwa kutumia logic? Je hakuna wenye ufahamu wa utawala wa kisheria?

Kuna mambo jeshi la polisi wanafanya yanakufanya ujiulize maswali mengi ya kukera.
Elimu,elimu,elimu,elimu,elimu,ilimu,ilimu,ilimu.

Kwenye Qur'an tukufu hata huko MWENYEZI MUNGU alitukumbusha juu ya elimu na kusisitiza ikiwezekana tukaifuate hata uchina
 
Elimu,elimu,elimu,elimu,elimu,ilimu,ilimu,ilimu.

Kwenye Qur'an tukufu hata huko MWENYEZI MUNGU alitukumbusha juu ya elimu na kusisitiza ikiwezekana tukaifuate hata uchina
Mbali na Elimu, lakini pia Katiba na Sheria zilizopo nazo ni tatizo lingine. Sheria zilizopo ni kandamizi kwa Raia na zinawapa kinga Polisi wasiweze kuwajibishwa kisheria hata pale wanapofanya makosa makubwa ya jinai Kama kuua watu kiholela.
 
Mmmh police gan mwenye Masters? PhD?
Aaah wee hapanaa.
Wapo wengi sana huwa wanajiongeza wakiwa makazini, Wapo wengine smart sana hata Darasani mfano Commishner Jerali Thobias Andengeye wakati RCO Morogoro tulikuwa tunasoma naye masters alikuwa kipanga, Baadae akapanda, akawa RPC mara full commishner wa HR polisi mara nikamona general wa zima moto nasikia sasahivi mkuu wa mkoa, sijui ki utendaji jeshini yukoje lakini darasani alikuwa mkali sana
 
Hiyo si sababu na msiendelee kukariri kwamba Polisi hawana elimu. Polisi 10k+ Kwa Sasa Wana Dr, Masters, bachelor, dip au form 6. Tatizo la ukosefu wa weledi nchini halihusiani na elimu zào. Bungeni kuna maprofesa lakini bado ni Bunge la ovyo kuliko la 1975.
Nipe jina la polisi mmoja tu ambaye ana cheo cha PhD.

Yaani polisi anayeitwa Afande Dokta...
 
Itafahamika baada ya ku-surrender hizo simu!

Ni ujinga tu. Ni sawa na mgonjwa aliyekatika kidole cha mguuni halafu daktari anasema mgonjwa apimwe haja kubwa.

Vioja vya polisi vinajulikana. Manji alituhumiwa kufanya biashara ya madawa ya kulevya, halafu walimpeleka kupima mkojo.

Polisi wakitaka kukutengenezea kesi ya uwongo ndiyo huwa wanahangaika na vitu visivyo na uhusiano. Haitashangaza ukasikia kuwa watuhumiwa wamepatikana na msokoto wa bangi.
 
Ila ndio wanaokulinda ukiwa unajijambia na mkeo.vile vile siamini km polisi wanakuzidi we kwa ujinga. Hilo likibatala limelewa sifa ht yeye anaweza kula mvua za kutosha. Kesi zake nyingi anashindaga kwa kutoa rushwa kwa majaji siyo akili wala kujua sheria

Ukiwa mgonjwa wa akili, unaropoka chochote. Eti Kibatala huwa anahonga majaji!! Waombe ndugu wakusindikize hospitali.
 
these shemless and shenanigans political activist must be responsible to co-oparate with our very able police unit and for sure must be prosecuted arconding to the law of the land in regards of their confirmed offences

hii stori mingi na porojo za hawa maadvocate wa kutafuta kiki na kujulikana ni useless kabisa, na haviwezi kuzuia polisi kufanya kazi yake na mahakama kutekeleza wajibu wake ipasavyo

upotoshaji hauna faida wala maana yoyote. By the way tuache hatua stahiki za kisheria viendelee

Kelele nyingi but no content. Mtu yeyote mwenye akili timamu, mwelewa, mkweli wa nafsi na mzalendo wa kweli, ataungana na Kibatala. Kwa sababu anachoongelea Kibatala ni kupanua uwigo wa haki.

Ndani ya jeshi la polisi, kama zilivyo taasisi nyingine, kuna waovu. Kuna polisi ni majambazi, wala rushwa na watengenezaji wa kesi za kubumba, hawa hawawezi kudhibitiwa na polisi wenzao, kinahitajika chombo kingine, kama ambavyo baadhi ya mataifa wamefanya.
 
Nakumbuka mwaka 1996 pale Tunduma , ujambazi ulikua unafanywa na polis. Mitaa ilikua inafungwa saa nne usiku. Waliletwa polis Toka makao makuu kuja kukomesha matukio ya uhalifu, polis kadhaa walidakwa.
Kule Njombe kuna mwaka mmoja, polisi aliuawa kwa rungu, na mlinzi wa kampuni kwenye tukio la wizi.

Polisi alikuwa kwenye lindo la bank usiku. Usiku huo akiwa na smg akaongozana na majambazi mpaka Kibena, karibia kilometa 10 toka eneo lake la kazi. Walipofika eneo la uhalifu, polisi yule alipiga risasi, mlinzi akakimbia. Majambazi yakaendelea kufungua mashine waliyokusudia. Kwa kuwa mashine ilikuwa kubwa, iliwachukua muda mrefu. Polisi akijua hakuna mlinzi, akabaki amesimama akitazama majambazi yanavyofungua mashine. Mlinzi wa kampuni alimnyemelea kwa nyuma, akamtandika yule polisi jambazi rungu moja la mpingo, akaanguka na kufa palepale, majambazi yakakimbia yakiacha kila kitu. Polisi wakamkamata yule mlinzi lakini kelele za wananchi na jitihada za kampuni, wakalazimika kumwachia, na kampuni ikamzawadia mlinzi jasiri aliyeua polisi jambazi.

Mjaka ya nyuma, nikiwa naishi Chuo kikuu UDSM kulikuwa na matukio mengi ya vibaka waliokuwa wakihusishwa na baadhi ya polisi. Likitokea tu tukio, polisi wanakuja mara moja, wanaanza kuorodhesha vitu vilivyoibiwa. Wewe unadhani wanachukua hizo taarifa kusaidia uchunguzi, kumbe wanataka kujua vitu vilivyoibiwa ili wasidanganywe kwenye mgao.
 
Nani nyumbu!!?

Halafu tangu lini idadi ya kura kuwa nyingi zikahalalisha ushindi wa mtu hasa katika nchi zetu za Dunia ya tatu!!?hata huko america idadi ya kura hazihalalishi ushindi wa urais!!

Hujui kura zinahalalisha yule aliechaguliwa tayari na wenye mamlaka ya nchi!?na sio idadi.na uwingi wa kura za mgombea!!?

Ingekua idadi ya kura inahalalisha ushindi was urais bas maalim seif,Lowasa,Tundu Lisu,Mrema wangeshaapishwa kuwa Marais was nchi hii!!hata secretary clinton angeshinda!!

Prof. Tibaijuka alisema kuwa alimwambia Lowasa wakati anahamia upinzani kuwa, hajui kuwa mfumo wetu wa Tanzania hauruhusu mtu kuwa Rais kutoka chama kingine chochote zaidi ya CCM? Lowasa akamjibu kuwa anajua, lakini amechoka kunyanyaswa.

Kwa hiyo unachokisema kina ukweli kwa sehemu kubwa.
 
Malalamiko huwa hayaishi ktk maisha ya binadamu hapa duniani. Lakini kumbuka ktk nchi za bara hili la Afrika, South Africa ndio nchi inayoongoza kwa uhalifu, sambamba na kuongoza ktk kuwawqjibisha Askari Polisi ktk kuwashitaki Mahakamani na/au kuwafukuza kazi.Afrika ya Kusini Askari Polisi wanaolalamikiwa, Wahalifu au waovu wanafukuzwa kazi na kufungwa jela kwa wingi Sana.

Hakuna mahali au taasisi ambayo inakuwa na watu wote walio safi. Kilicho tofauti ni kwamba kuna nchi ambazo kuna waovu lakini waovu wanaadhibiwa vikali kiasi cha kupunguza idadi ya watu waovu.

Lakini zipo nchi, kama Tanzania, waovu wenye madaraka au mamlaka ndani ya Serikali, kuna wakati badala ya kuadhibiwa, wanatukuzwa. Fikiria mawaziri ambao ni mafisadi, taasisi na wizara zao zinatajwa kwa ufisadi mkubwa, tena kwa vielelezo, hakuna anayeadhibiwa, na kuna wakati wanapandishwa vyeo au kuhamishwa wizara.
 
Tafsiri ya kutumia akili ni ipi? Nguvu hutumika baada ya akili

Akili ndiyo humwongoza mwanadamu atumie nguvu wapi, atumie wakati gani, atumie kwa kiwango gani. Ukiwa huna akili unatumia tu nguvu, nguvu zako zinaweza kuwa chanzo cha uharibifu.
 
Changamoto ya chombo chetu cha Polisi ni kufanyakazi kwa kupokea maelekezo toka juu!
 
Nipe jina la polisi mmoja tu ambaye ana cheo cha PhD.

Yaani polisi anayeitwa Afande Dokta...
Wapo wengi sana sana mkuu , mimi nimesoma na dr mangu ifm, na kulikuwa na phd kama 4 nimesoma nao wote walikuwa mapolisi, nenda pale oysterbay kuna ocd alitokea mbweni nae ni phd , kiufupi ni wengi mno sema kwa nature ya kazi yao huwezi kuwaona kwenye media wakijikweza
 
Back
Top Bottom