Peter Kibatala: We need a Police to Police the Police

Kelele nyingi but no content. Mtu yeyote mwenye akili timamu, mwelewa, mkweli wa nafsi na mzalendo wa kweli, ataungana na Kibatala. Kwa sababu anachoongelea Kibatala ni kupanua uwigo wa haki.

Ndani ya jeshi la polisi, kama zilivyo taasisi nyingine, kuna waovu. Kuna polisi ni majambazi, wala rushwa na watengenezaji wa kesi za kubumba, hawa hawawezi kudhibitiwa na polisi wenzao, kinahitajika chombo kingine, kama ambavyo baadhi ya mataifa wamefanya.
unachekesha sana kamanda 🐒

perfection sense ni utumwa au uraibu usio faa hata kidogo 🐒

mtu timamu hababaishwi hata kidogo na mwenye mawazo au mtazamo tofauti na wake 🐒

habezi, hadhihaki wala kulazimisha anachoamini yeye na wengine wafikiri na kuamini hivyo 🐒

mihemko dalili na kiwango kibaya sana cha kukata tamaa 🐒
 
unachekesha sana kamanda

perfection sense ni utumwa au uraibu usio faa hata kidogo

mtu timamu hababaishwi hata kidogo na mwenye mawazo au mtazamo tofauti na wake

habezi, hadhihaki wala kulazimisha anachoamini yeye na wengine wafikiri na kuamini hivyo

mihemko dalili na kiwango kibaya sana cha kukata tamaa

Hapa hakuna cha kuchekesha.

Labda nikuulize swali dogo, unadhani kwa nini tuna Serikali, Bunge na mahakama? Kwa nini tuna Tume ya Haki za binadamu? Kuna haja gani ya kuwa na Tume ya haki za binadamu wakati tuna mahakama ambayo kinadharia ndiyo chombo cha kutoa haki?

Kama tungekuwa tunaamini kuwa taasisi moja inaweza kuwa perfect kusingekuwa na haja ya kuwa na taasisi nyingine. Labda tungekuwa tu Serikali. Serikali ingeweza kuwa na mahakimu kwaajili ya kuendesha kesi. Na Bunge kusingekuwa na haja ya kuwa nalo. Serikali ingeweza kuwatumia tu watumishi wake wa maeneo kuwasilisha mambo yanayohusiana na maeneo yao ya kiutawala.

Jibu ni moja tu: Ni vigumu sana kuwa na watu au taasisi moja yenye perfection ya 100%. Hata hizo nchi zenye taasisi za kuchunguza na kufuatilia vitendo vya Polisi, ni kwa sababu uzoefu umewathibitishia kuwa ndani ya jeshi la Polisi, kuna watu waovu ambao hawawezi kudhibitiwa na mamlaka za ndani ya polisi.
 
Akili ya Chadema ndiyo inayohitajika nchi hii.Miaka 60 ya akili ya KiCCM ni UCHAWA na kujipendekeza iliupate vyeo. Ungetumia akili ungeacha UCHAWA.

Ni mambo ya ajabu sana.

Ukizungumzia haki, utaambiwa wewe ni CHADEMA, kama vile CCM na vyama vingine vinasimamia dhuluma!!

Ukizungumzia uwajibikaji wa Serikali na taasisi zake, utaambiwa ni CHADEMA, kama vile CCM na vyama vingine vinasimamia utendaji holela wa Serikali na taasisi zake!!

Ukipinga ufisadi wa watendaji na viongozi wa Serikali utaambiwa wewe ni CHADEMA, kama vile CCM na vyama vingine vipo kwaajili ya kupalilia, kulinda na kustawisha ufisadi!!

Hata ikitokea mtu anayefahamika kabisa ni mwanaCCM, akazungumzia tu umuhimu wa kuwa na katiba nzuri na sheria nzuri za uchaguzi, ataambiwa kuwa huyo ni pandikizi la CHADEMA. Je, ina maana CCM ipo kwaajili ya mambo mabaya tu?
 
Akili ya Chadema ndiyo inayohitajika nchi hii.Miaka 60 ya akili ya KiCCM ni UCHAWA na kujipendekeza iliupate vyeo. Ungetumia akili ungeacha UCHAWA.
Sijawahi kuwa chawa na wala siyo mpenzi wa siasa ila kwa akili hizo za kila mtu anayewakosoa chadema ni chawa hamtofika mbali ndio maana chadema kinaonekana chama cha wahuni , nilishasema mara nyingi katika kile chama mwenye busara ni mbowe tu angalia sasa yani mtu hata hunifahamu unaanza kuropoka ujinga wako
 
Sijawahi kuwa chawa na wala siyo mpenzi wa siasa ila kwa akili hizo za kila mtu anayewakosoa chadema ni chawa hamtofika mbali ndio maana chadema kinaonekana chama cha wahuni , nilishasema mara nyingi katika kile chama mwenye busara ni mbowe tu angalia sasa yani mtu hata hunifahamu unaanza kuropoka ujinga wako
Hatutofika mbali ukimaishanini? Tusipofika mbali unakuuma ni nini wewe CCM?
 
Back
Top Bottom