Peter Kibatala: We need a Police to Police the Police

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
118,173
219,307
Ujumbe wake huu hapa .

Screenshot_2024-04-26-01-45-38-1.png
6
 
Ni kweli, kinatakiwa kiundwe chombo kingine Maalumu Cha kipolisi ili kuweza kulisimamia na/au kulichunguza Jeshi la Polisi pale linapolalamikiwa au linapotuhumiwa .Kwenye nchi karibia zote zenye tawala za Kidemokrasia hapa duniani kuna Taasisi za namna hii. Zipo Taasisi Maalumu kabisa za Kipolisi ambazo zinajitegemea (Independent Police Investigative Organizations), kazi yake ni kushughulikia malalamiko dhidi ya Polisi au Jeshi la Polisi la kawaida sambamba na kufanya Upelelezi dhidi ya Polisi. Tàasisi hizo huwa zinakuwa na Mamlaka yote ya Kipolisi, lakini Upolisi wao huwa wanaufanya dhidi ya Mapolisi au Jeshi la Polisi la kawaida. Taasisi za Kipolisi za namna hii huwa zinakuwa na Utawala wake binafsi unaojitegemea, hawana mwingiliano wowote wa kimajukumu au kiutendaji na Jeshi la Polisi la kawaida. Kwa mfano, Nchi ya Afrika ya Kusini wana Taasisi ya namna hii, inaitwa IPID ( The Independent Police Investigative Department, IPID). IPID ni Jeshi la Polisi la Kujitegemea ambalo kazi yake Kuu ni kufanya kazi za Kipolisi dhidi ya Jeshi la Polisi la kawaida, yaani kufanya Upelelezi na Kumshitaki Mahakamani Askari Polisi yoyote yule anayetuhumiwa au kulalamikiwa bila kujali cheo chake, hata kama Polisi huyo anayetuhumiwa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi la kawaida.
 
Polisi Tanzania ni aibu kubwa kabisa. Ina maana jeshi lote limejaa wajinga tu? Hakuna angalau watu wenye ku reason kwa kutumia logic? Je hakuna wenye ufahamu wa utawala wa kisheria?

Kuna mambo jeshi la polisi wanafanya yanakufanya ujiulize maswali mengi ya kukera.
Murilo akishauriwa atakwambia UNANIJUA MIMI NANI ? Amejaa mabavu matupu na ukiritimba wa ccm
 
Ni kweli, kinatakiwa kiundwe chombo kingine Cha kipolisi ili kuweza kulisimamia na/au kulichunguza Jeshi la Polisi pale linapotuhumiwa.
Tungekuwa tuna IGP anaejielwa angetosha kuwa anasimamia hili. Sema nao sijui huwa wanadhani ni maagizo kutoka juu, wanaogopa kutumbuliwa.

Hapa alikuwa anapiga simu ya upepo kuwaambie waache ujinga wafanye kazi za maana jambo linaisha.
 
Ni kweli, kinatakiwa kiundwe chombo kingine Maalumu Cha kipolisi ili kuweza kulisimamia na/au kulichunguza Jeshi la Polisi pale linapotuhumiwa .Kwenye nchi karibia zote zenye tawala za Kidemokrasia kuna Taasisi za namna hii. Zipo Taasisi Maalunu kabisa za Kipolisi ambazo zinajitegemea (Independent Police Organizations), kazi yake ni kushughulikia malalamiko dhidi ya Polisi au Jeshi la Polisi sambamba na kufanya Upelelezi dhidi ya Polisi. Tàasisi hizo huwa zinakuwa na Mamlaka yote ya Kipolisi, lakini Upolisi wao huwa wanaufanya dhidi ya Mapolisi au Jeshi la Polisi la kawaida. Taasisi za Kipolisi za namna hii huwa zinakuwa na Utawala wake binafsi unaojitegemea, hawana mwingiliano wowote wa kimajukumu au kiutendaji na Jeshi la Polisi la kawaida. Kwa mfano, Nchi ya Afrika ya Kusini wana Taasisi ya namna hii, inaitwa IPID ( The Independent Police Investigative Department, IPID). IPID ni Jeshi la Polisi la Kujitegemea ambalo kazi yake Kuu ni kufanya kazi za Kipolisi dhidi ya Jeshi la Polisi la kawaida, yaani kufanya Upelelezi na Kumshitaki Mahakamani Askari Polisi yoyote yule anayetuhumiwa au kulalamikiwa bila kujali cheo chake, hata kama ni Polisi huyo anayetuhumiwa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi la kawaida.
Naunga mkono hoja hii mkuu,KATIBA MPYA ndio kitu nchi inahitaji,umeongelea IPID hii imeshawahi sana kuandikwa humu,taasisi hii isipokuwepo police wetu wapo above the laws na wanajifanyia wanavyotaka maana wananchi wengi ni wapumbavu na waoga uliojaa uzuzu,mpumbavu mmoja pale kagera anatishia kuwapoteza watanzania wengine kisa utofauti wa kiitikadi,RPC pale anafwata mkia,IGP naye kimyaa,CJ yupo kimya,ukweli police wamemuua yule raia na police hapa ni suspects ilitakiwa nao wachunguzwe,Tanzania tumekua tunapata strong state persons na sio ICONS
 
Polisi Tanzania ni aibu kubwa kabisa. Ina maana jeshi lote limejaa wajinga tu? Hakuna angalau watu wenye ku reason kwa kutumia logic? Je hakuna wenye ufahamu wa utawala wa kisheria?

Kuna mambo jeshi la polisi wanafanya yanakufanya ujiulize maswali mengi ya kukera.
Hili ulilowaza hata Mimi naliwaza. Polisi wote wale na vyeo mabegani wameshindwa kujua mwitikio wa Jamii dhidi ya Jambo hili? Hawaoni wameanza kupambana na Jamii badala ya kupambana na wanaharakati?
 
Yuko wapi kipigo Cha mbwa Koko? Kikokotoo kilimuacha salama au kilimpitia?
Yuko polisi mmoja amefanya kazi ya upolisi miaka nenda Rudi kuitetea serikali ya CCM. Alipostaafu mafao' aliyopewa hayatoshi hata kununua IST showroom. Ameshindwa kurudi kwao maana atajielezaje kwa mates wa umri wake.
Tufanye kazi tukijua Kuna maisha baada ya kazi.
Ni hayo tu huku nikiwaza kikokotoo na NHIF.
 
Back
Top Bottom