Paul Makonda akutana na Vijana zaidi ya 223 maarufu kama wadudu ofisini kwake na kuwataka kuwa walinzi na mabalozi wa kutangaza mazuri ya Arusha

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,916
10,407
Ndugu zangu Watanzania,

Mwamba Makonda hapoi wala hakauki midomoni mwa watanzania.ni mtu na kiongozi wa kugonga na kuteka vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kila uchwao utafikiri field Marshall anayerejea kutoka uwanja wa vita na mapambano.

Baada ya kuwa na utaratibu wa kukutana na makundi mbalimbali na taasisi mbalimbali katika kuzieleza maono yake na Dira yake pamoja na kiu na matamanio yake ya kuiona Arusha inaku Kama kama majiji ya Washington DC Marekani au Newyork au DUBAI falme za kiarabu au Paris ufaransa au Amsterdam Uholanzi au Geneva uswissi ameweza kukutana pia na mamia ya vijana zaidi ya 223 maarufu kama WADUDU Ofisini kwake.

Ambapo pamoja na mambo mengine mbalimbali amewataka vijana hao kuwa walinzi na mabalozi wazuri wa kuutangaza mkoa wa Arusha pamoja na mazuri yote ya mkoa wa Arusha. ametaka wamuheshimishe kama ambavyo anavyowaheshimu na kuthamini vipaji vyao. Amewataka kwa pamoja waweze kushirikiana katika kuifanya Arusha kuwa mkoa wa mfano.

Hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa Arusha ni lango kuu la watalii hapa nchini .amewataka vijana hao kutumia fursa mbalimbali zinazopatikana mkoani Arusha na ambazo zitaendelea kutengenezwa kwa ajili ya kuwainua na kuwakwamua kiuchumi.

Vijana hao wameonyesha kufurahishwa sana na uchapakazi wa Mwamba Mwenyewe Makonda Field Marshal ,na kusema kwa hakika Mwamba ni kiongozi mwenye kibali cha Mwenyezi Mungu na Mbunifu sana mwenye kuwajali watu na kuwa nao karibu.. wamemshukuru sana Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan kwa kuwapelekea Mwanae kuwa mkuu wao wa mkoa.

Wamemuahidi Mwamba Makonda kumpa ushirikiano pamoja na kuwa walinzi na mabalozi wazuri wa mkoa wa Arusha katika kuutangaza mkoa huo.wamesema ya kuwa hawapo tayari kuona kijana wa aina yoyote ile akiuchafua na kuchafua taswira nzuri ya Mheshimiwa mkuu wa mkoa kwa kufanya Vitendo vya kihalifu na uhalifu. Wamesema watajikita katika kufanya kazi halali katika kujipatia kipato na kuiomba jamii kuwapa ushirikiano na Kuwaunga mkono hasa katika sanaa.

Wamemshukuru sana kwa heshima kubwa waliyopewa na Mwamba Makonda ya kukaa nao na kuwasikiliza na kuzungumza nao masuala mbalimbali.wanasema haijawahi kutokea. Wamesema Mwamba Makonda asiwe na wasiwasi ya aina yoyote ile kwa kuwa watakuwa naye bega kwa bega na kumpa ushirikiano wote atakaohitaji kutoka kwao ,ikiwa ni pamoja na kuwa wa kwanza katika kudumisha usalama na amani ya mkoa wa Arusha.

Mwamba Makonda Anaendelea kuonyesha kuwa uongozi ni kuonyesha njia,ni kuwashirikisha watu ,ni kuwa na maono na Dira ya kiuongozi na siyo kupiga Majungu,kupiga watu vita,kujikweza ,kubagua watu,kupiga umbea na unoko kwa mabosi wa juu,.Mwamba yeye amejikita katika kuchapa kazi na kuwaacha wengine waendelee kuongea tu. Asante sana Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mama Samia Suluhu Hasssan kwa kuturejeshea tena Mwamba Makonda katika uongozi. Mwamba Makonda hatakuangusha wala kukufanya ujute Mama yetu kumteua, bali utatamani kuwa ungemteuaga Mapema Zaidi.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Kila siku wadudu watamfanya huyu jamaa achizike zaidi ...Maana wadudu wenyewe machizi.
 
Kila siku wadudu watamfanya huyu jamaa achizike zaidi ...Maana wadudu wenyewe machizi.
Acha dharau kwa vijana wewe.watu aina yako hamfai hata kuwa viongozi wa familia tu.kazi ya kiongozi ni kuwaongoza watu,kuwabadili mitizamo hasi na kuwafanya wakawa na mitizamo chanya,kuwaunganisha watu,kuwainua watu na kuwakwamua pale walipokwama, kuwa karibu na watu na kujinyenyekeza kwa watu wa aina zote.kiongozi haifai kuwa mbaguzi .
 
Mwashamba akisikia jina Makonda huwa anabubujikwa na machozi na kuanza kutokwa na 'maji' baadhi ya sehemu za mwili wake!!.
 
Kwa hiyo anaunda jeshi sio?
Kwani vyombo vyetu vya ulinzi na usalama havipo?
Hata makundi ya Banyamlenge na vinginevyo vilianza kwa kivuli kama hiki!
 
Kwa hiyo anaunda jeshi sio?
Kwani vyombo vyetu vya ulinzi na usalama havipo?
Hata makundi ya Banyamlenge na vinginevyo vilianza kwa kivuli kama hiki!
Jeshi lipi lililoundwa? Unaelewa ulinzi na usalama wa Taifa letu ni jukumu la kila Raia wa Tanzania?
 
Wakuu,

Hawa wadudu wameapishwa kuwa walinzi na kupambana watu kwa mafunzo gani? Kwa sifa gani walizonazo mpaka Makonda ameamua kuwaapisha? Huku "KUPAMBANA" na kila mtu "AKAYECHAFUA" heshima na thamani ya Mkoa wa Arusha inamaana tayari wameshapewa tiketi ya kushika silaha na kujeruhi watu wakitoa tu sababu fulani amechafua heshima ya mkoa wa Arusha.

Na HESHIMA ndio ipi? Mtu akikosoa uwajibikaji wa viongozi Arusha? Au wanaotoa taarifa za Makonda kulala hoteli ya Gran Melia wakati kuna malazi yake yeye kama Mkuu wa Mkoa?

Hili halipaswi kufumbiwa macho, ukizangatia tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu 2025.

Walianza kwenda kufanya siasa kwenye makanisa na misikiti, wakaenda kuanza kufanya ukarabati wa mchongo, sasa wanaanza kuapisha vikundi na kuviita vya "Ulinzi"! Na hakuna kiongozi wowote anayetetea hili?

Wakuu mnaonaje hili?

 
Jeshi lipi lililoundwa? Unaelewa ulinzi na usalama wa Taifa letu ni jukumu la kila Raia wa Tanzania?
Kama unalijua hilo kuna sababu gani hilo kundi linalojiita wadudu?
Na lengo la hao wadudu ni nini? Na kwa nini awaagize hao wadudu ?
 
Back
Top Bottom