Paul Makonda kupokelewa kishujaa Arusha, Magari ya msafara yafurika uwanja wa ndege kumsubiri atue

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,994
10,484
Ndugu zangu Watanzania,

Arusha kumekucha,kanda ya kaskazini imesimama, wananchi wanatetemeka kwa furaha, shughuli zote zimesimama, habari ni moja tu, stori ni moja tu ni juu ya ujio wa Mwamba Mwenyewe Mheshimiwa Paul Christian Makonda Kijana jasiri kusini mwa jangwa la sahara.

Imeshuhudiwa magari ya watalii na kitalii yakiwa yamefurika kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kumsubiri Mwamba atakapotua uwanja wa ndege ,ili kuweza kumlaki na kumpokea na kuongoza msafara mzito wa Magari kuwahi kushuhudiwa ndani ya jiji la Arusha kuelekea ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa ajili ya makabidhiano ya Ofisi..

Vijana na wananchi wa Arusha wamejawa na furaha na matumaini makubwa sana juu ya ujio wa Mwamba. Ni gumzo kila mahali,ni shamra shamra kila kona,ni mshike mshike kila sehemu juu ya mapokezi ya Mwamba Makonda jasusi na komando wa vita, field Marshall aliyetangaziwa Mwisho na maadui zake lakini Mungu akautangaza mwanzo wake ulio mkuu na wa ushindi..

Leo nchi kusimama na macho na masikio ya watanzania wote kuelekezwa Arusha na kanda ya kaskazini.upinzani wanatetemeka utafikiri wagonjwa wa homa kali,moja haiendi wala mbili haisomi,upinzani hasa CHADEMA wote wanabubujikwa machozi ya huzuni ya kuona mwisho wao kisiasa ukiwa umewadia.

Endeleeni kutulia kufuatilia kitakachojili na kitakachozungumzwa na Mwamba Mwenyewe Makonda . nitaendelea kuwaleteeni kila kitu na kila habari na kila neno litakalo toka kinywani mwa Mwamba Mwenyewe Makonda Jabali la siasa.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
 
Hivi mleta hoja naomba kujua haya
1. Hili jina la ukoo ni halisia?
2. Una miaka mingapi?
3. Je una mke na mtoto?
5 haujawahi kuugua kichaa?
Maana kila unachoandika ni ujinga mtupu kiasi unadhalilisha familia yenu.
Acha kuweweseka na kuhangaika hangaika hapa.hoja hujibiwa kwa hoja na siyo viroja.
 
Wadau hamjamboni nyote?

Matangazo mbashara muda huu kutokea ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha

Paul Makonda Mkuu Mpya wa Mkoa Arusha anakabidhiwa rasmi ofisi


Kazi inaendelea
 

Attachments

  • 1712567762035.jpg
    1712567762035.jpg
    585.5 KB · Views: 3
  • 1712567758907.jpg
    1712567758907.jpg
    729.9 KB · Views: 3
  • 1712567755550.jpg
    1712567755550.jpg
    578.8 KB · Views: 3
Back
Top Bottom