Nusu ya nusu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,678
698,714
Usipende wapenzi nusu Usifurahishe marafiki nusu
Usiishi nusu ya maisha wala usife nusu kifo
Ukichagua ukimya, kaa kimya Unapozungumza, fanya hivyo hadi umalize
Usinyamaze kusema kitu Wala usiseme kwa kunyamaza
Ikiwa unakubali, basi eleza waziwazi Usijifunge
Ukikataa basi kataa kabisa kwani kukataa kwa utata ni kukubalika hafifu

Usikubali nusu suluhisho wala Usiamini ukweli nusu
Usiota ndoto nusu Usifikirie juu ya matumaini nusu
Nusu ya njia haitakufikisha popote Nusu wazo halitakuletea matokeo yoyote
Nusu ya maisha ni maisha ambayo hukuishi,
Neno hujasema Tabasamu umeahirisha Upendo ambao haujapata

Urafiki ambao hukuujua Nusu ni wakati tu wa kutoweza lakini wewe unaweza kwani wewe si nusu ya kiumbe Wewe ni mzima ambao upo ili kuishi maisha sio nusu ya maisha " target="_blank" class="link link--external" data-proxy-href="/proxy.php?link=http%3A%2F%2FJr%5Bemoji769%5D&hash=612da71b7ee1c2c33f96a4186d20d2ce" rel="nofollow ugc noopener">Jr
Screenshots_2023-08-07-04-32-14.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unatumia lugha ya kisanii lugha ngumu.

Hatujazoea mafumbo.

Mbona wakasema ni heri nusu shari kuliko shari kamili ?

Mbona maisha watu wanaondoka na umri nusu? Je ni Mungu au ni mfalme wa dunia anayefanya hayo?

Nini sasa hicho cha hapo kwenu? Je, wale wote hawana wenza? Mbona wameviziwa nusu ?
 
Kuna riwaya moja ya kingereza ninayo inaitwa half broken things, sijawahi kuielewa kiundani kutokana na mafumbo mengi mule tokea ni ichukue kweny maktaba ya shule mwaka 2013. Sasa naona context ya mshana ndio inanichanganya zaidi nikijaribu ku compare.
 
Back
Top Bottom