Nini kilikufanya ukaacha kwenda kuabudu kwenye nyumba ya ibada?

Uzi maalumu kwa watu waliokuwa wanahudhuria nyumba za ibada na baaadaye kuacha, weka sababu yako hapa, we unayehudhuria tupe sababu ya kuhudhuria (achana na zile za dini yangu ni bora, na ya kweli kuliko zingine).

Mimi niliacha Kwenda kanisani baada ya mchungaji kutumia hela ya kanisa kununua magari yake binafsi, kila akija ibadani anakuja na gari inayofanana na suti aliyovaa, kama ni suti ya blue basi gari ya blue, kama nyeusi basi nyeusi, nyeupe, maroon, kijivu in short mchungaji alikuwa na gari ya kila rangi kulingana na nguo zake.

Wakati huo mimi natembea kwa miguu tena naambiwa toa ubarikiwe. Kubwa Zaidi, mchungaji alikuwa na nyumba ndogo, na baada ya kunogewa aliamua kuoa kabisa akawa na wake wawili jambo ambalo ni kinyume na kanuni za kikristo. Nikasema hapanaaaaaaaaa.​
  • Sababu nyingine nilisoma vitabu vingi ambavyo vimefanya nisitamani kabisaa kusikia mambo ya dini hata kidogo. Vitabu kama
    • Toledot Yeshu
    • The history of God
    • Evolution of the idea of God. Na vingine vingi.
Wewe je, kipi kilikusibu?
Msaada wa links za hivyo vitabu
 
Mimi ni

1.Mavazi mafupi ya wanawake/ Mkahaba kanisani.
2.Mchungaji mwanamke.
3.Uchawi kanisani
4.ujio wa wajasiriamali wa kidini
Hakika nimebatizwa KKKT nimepata kipaimara hapo na pia nimefunga ndoa mwaka 2002 hapo Magomeni mviringo lakini siku nilipokuja kukuta kanisa linakwenda kinyume na Biblia kuwa na kiongozi wa sala asiyekubalika na maagizo ya Biblia nilijitenga kabisa mpaka sasa masali kanisa lolote nitakapojisikia
 
Sijaacha ila nilihama kanisa kwa sababu
1. Mchungaji alikuwa akijitapa kuyapatia maisha kutokana na jitihada zake. Wakati vitu vingi vilikuwa vikitokana na michango ya waumini waliochoka kimaisha. Nilioni ni busara angekuwa anawashukuru waumini

2. Mambo binafsi ya mshirika na mchungaji yalifanywa kuwa mambo ya kanisa. Mtu kafiwa na kaka yake au wifi yake inakuwa kama ni kitu cha kanisa mnaanza kuchangishana. Mchungaji kaharibikiwa gari mnaanza michango ya kununua spea.

3. Michango ilizidi orodha ilikuwa ndefu sana

4. Washirika walianza vizinga na mikopo kwangu. Kuna kosa nilifanya wakati wa michango. Nilikuwa nachangia mara 3 au 4 ya wengine. Kujitoa kwangu ikaonekana ninazo.

5. Usipoenda kanisani unapigiwa simu. Ukikutana na mshirika ni kuulizwa tu mbona hatukuoni church. Inabidi uanze kujitetea tu kila mara

6. Mke wa mchungaji kuwa kama mchungaji mdogo
 
Uzi maalumu kwa watu waliokuwa wanahudhuria nyumba za ibada na baaadaye kuacha, weka sababu yako hapa, we unayehudhuria tupe sababu ya kuhudhuria (achana na zile za dini yangu ni bora, na ya kweli kuliko zingine).

Mimi niliacha Kwenda kanisani baada ya mchungaji kutumia hela ya kanisa kununua magari yake binafsi, kila akija ibadani anakuja na gari inayofanana na suti aliyovaa, kama ni suti ya blue basi gari ya blue, kama nyeusi basi nyeusi, nyeupe, maroon, kijivu in short mchungaji alikuwa na gari ya kila rangi kulingana na nguo zake.

Wakati huo mimi natembea kwa miguu tena naambiwa toa ubarikiwe. Kubwa Zaidi, mchungaji alikuwa na nyumba ndogo, na baada ya kunogewa aliamua kuoa kabisa akawa na wake wawili jambo ambalo ni kinyume na kanuni za kikristo. Nikasema hapanaaaaaaaaa.​
  • Sababu nyingine nilisoma vitabu vingi ambavyo vimefanya nisitamani kabisaa kusikia mambo ya dini hata kidogo. Vitabu kama
    • Toledot Yeshu
    • The history of God
    • Evolution of the idea of God. Na vingine vingi.
Wewe je, kipi kilikusibu?
Nilipoona pastor analidwa na bodyguard huku akisema sisi tutalindwa na damu ya yesu nikajua hapa hakuna liwalo

Na nilipokuja kuona Israel inalidwa kwa drone zito huku tukiaminishwa nchi zetu zinalindwa na Mungu wa Israel mm hapo nimefunga ukurasa wa mambo ya ibada labda kwenye life after death huko.
 
Back
Top Bottom