Wild Flower
Member
- Jul 20, 2023
- 87
- 103
Habari wakuu, nina marafiki wengi walio hitimu chuo mwaka jana lakini mpaka sasa wanahangaika sana na suala la ajira. Nimekuja kugundua kwamba elimu ya Tanznaia haizingatii mahitaji ya soko la ajira kwa sasa na bado tunatumia elimu ya wakolonia aisee. mimi ningeshauri hatua zifuatazo zifanyike ili tupunguze wimbi la "unemployed" mtaani:
Marekebisho ya Mtaala: Mtaala unapaswa kufanyiwa marekebisho ili kuweka msisitizo zaidi katika kutoa stadi za kitaalamu na kiufundi. Mtaala unapaswa kuwa na mchanganyiko wa masomo ya kimsingi na yale ya kitaaluma yanayolingana na mahitaji ya soko la ajira. Unakuta mtu unafundishwa History 2 mambo ya War of roses huko Europe au Fishing in Netherlands kweli?!
Ushirikiano kati ya Vyuo Vikuu na Sekta ya Umma na Binafsi: Vyuo Vikuu vinapaswa kushirikiana na sekta ya umma na binafsi ili kuelewa mahitaji ya soko la ajira na kubadilisha mtaala ili kukidhi mahitaji hayo. Hii itasaidia kuhakikisha kwamba wahitimu wanatoka na stadi zinazohitajika na soko la ajira. chuoni tunafundishwa sana theory na tukija mtaani vile tulivyofundishwa hata haviingii kabisa kwenye kazi zetu. Practical methods zitumike sana. Mtu unafundishwa kuhusu Kompyuta kwenye projector alafu ukipewa huwezi kuitumia. Kuna haja ya kuimarisha mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi ili waweze kupata uzoefu halisi wa kazi kabla ya kuhitimu. Hii itasaidia kuwaandaa kisaikolojia na kiuhalisia kwa ajira wanazotafuta.
Napendekeza kwa vyuo hata wasome miaka miwili full alafu mwaka watatu wapangiwe stations za kufanya practical ili kuepuka wimbi kubwa la wahitimu kuangukia kama volunteers au interns sehemu za kazi kwa muda mrefu kwa sababu hawana uwezo mkubwa na ujuzi unaotakiwa kwenye soko la ajira.