Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 4,532
- 4,276
You really believe that? Ulielewa jinsi vitisho vya Magufuli vilivyokuwa enzi zile? Jinsi vilivyobadili mazingira ya kisiasa ndani na nje ya CCM na kuuweka mustakabali mzima wa taifa mikononi mwa mtu mmoja?Dah, mbona shajieleza vya kutosha juu ya hili jambo humu humu kwenye mada hii nikijibishana na mkuu 'Zanzibar-ASP'? Mnataka nijibu nini tena.
Halima na hao wenzake aliowaongoza kwenda Bungeni wasingeweza kuwa na uthubutu wa kufanya jambo zito kiasi kile kwa uamzi wao pekee, au ushawishi toka nje ya chama chao. Waeleweni hawa wanawake walivyokuwa ngangari kwelikweli wakati mgumu sana.
Sijasema hapa, kwamba kiongozi toka CHADEMA aliwashawishi waasi, la hasha, lakini ni lazima mjue kwamba vitisho vya Magufuli tu wakati huo visingetosha hawa mabinti wafanye kama walivyofanya. Ni lazima pawepo na 'consultation' ndani ya chama (hata kama ni kiongozi mmoja bila ya kushirikisha wengine).
Halafu hiyo “consultation ndani ya chama” ilikuwa na uzito gani kuzidi vitisho vya Magufuli na manufaa ya aina gani kiasi cha kuwa na ushawishi kwa kina Halima kutupilia mbali legacy na hatma zao za kisiasa?