Nimekubali matokeo, UKAWA Kanda ya Ziwa wako vizuri, Mnyika, Salum ni Combination ya hatari

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,537
113,677
Wanabodi,

Nimeangalia Taarifa ya habari ya ITV, saa 5:00 usiku huu, kiukweli Nimekubali Matokeo!, UKAWA Kanda ya Ziwa ni Noma!, hii combination ya JJ. Mnyika na Salum Mwalimu, ni combination ya hatari sana kwa uhai wa CCM Kanda ya Ziwa.

Kwa jinsi nilivyoushuhudia umati uliojitokeza, nairudie tena ile kauli ya kuwa Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi!

Sasa ikitokea na Kanda ya Ziwa, CCM ikachokwa mpaka basi, naomba kukiri, kwa uchaguzi wa 2015, kazi itakuwa ni rahisi sana, ni kama kumsukuma tuu mlevi!.

Kanda ya Kaskazini, waliisha kata shauri siku nyingi, kuwa CCM Basi!, ila kura za Kanda ya Kasikazini sio decisive kwa sababu kanda hiyo sio determinant ya nani anakuwa rais wa nchi hii, lakini kwa upande wa Kanda ya Ziwa, kura za kanda ya Ziwa ndio zina determine, ni nani anakuwa rais wa Tanzania!, hivyo ni decisive votes!.

Kazi kubwa ya Wana UKAWA ni changamoto ya mgombea mmoja atakayekubalika pande zote, mwenye uwezo wa kuchagulika!. Ikitokea CCM wasimsimamishe yule "jamaa yangu!", na UKAWA, ikamtwaa, ikamsimamisha mgombea mmoja strong!, 2015 hili "dubwana" linakwenda chini!.

Hongera Mnyika, Hongera Salim Mwalimu.

Wasalaam

Pasco.
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
attachment.php
 
Playing game mind as usual Pasco.

Uchaguzi Mkuu 2015 ukiisha kauli ya gwiji Jenerali Ulimwengu itatimia hata kwako pia...utaweza kuzikumbuka akili ambazo Kwa sasa umezisahau Kwa sababu ya yule mgombea anayelazimisha picha za mazoezi zitokee magazetini!

Kwa sababu ya heshima ya taaluma yetu (you and I share that at least), huwa nakuombea usizisahau moja Kwa moja.
 
Last edited by a moderator:
Kwa swala la kuchagua nani kushika usukani wa kugombea Urais ndilo jambo litakalo wasambaratisha UKAWA!
Kwanza Tujiulize UKAWA ni chama cha Siasa?
Mtu an aye faa kuwa Rais ni Lipumba lakini sidhani kama Chadema na Bavicha watakubali Lipumba kuwaongoza!

Slaa amesha chokwa kabisa na Mbowe hana sifa kabisa!
 
Siku zote CHADEMA inafanya mazuri tangu kuanzishwa kwake, wewe umejivisha upofu usiokuwa nao ndiye usiyetaka kuyaona mazuri ya CHADEMA. Huu umati uliouona kwenye taarifa ya habari ni ushahidi tosha wa kuonyesha kukubalika/kupendwa kwa CHADEMA katika kanda hiyo.

Mimi ni kawaida yangu, Chadema mnapofanya mazuri, huwa nawakubali sana, na huwapongeza, ila mnapoboronga nawabalasa na hapo kwenye kubalasa ndipo huwa shughuli!.

Pasco.
 
Mkuu Pasco

Chadema walifanyia mkutano wao uwanja wa Mbuguni sijui kama unajua ukubwa wa huo uwanja.

Hakuna chama chochote cha siasa kilichofanya mkutano uwanja wa Mbugani kikakosa watu.

Kwa kukufahamisha tu uwanja wa mbugani ukubwa wake ni nusu ya uwanja wa kidongo chekundu, nimeshangaa umefanya reference ya kanda ya ziwa kupitia uwanja mbugani chini ya camera za ITV.

Halafu umesahau kuwa kuna vyama viwili Chadema na UKAWA sijui unaongelea combination gani wakati urais unatakiwa na Prof. Lipumba na Dr.Slaa.
 
Last edited by a moderator:
Playing game mind as usual Pasco.

Uchaguzi Mkuu 2015 ukiisha kauli ya gwiji Jenerali Ulimwengu itatimia hata kwako pia...utaweza kuzikumbuka akili ambazo Kwa sasa umezisahau Kwa sababu ya yule mgombea anayelazimisha picha za mazoezi zitokee magazetini!

Kwa sababu ya heshima ya taaluma yetu (you and I share that at least), huwa nakuombea usizisahau moja Kwa moja.

kaka Tumaini heshima mbele naomba msaada wako CCM mwaka 2005 walipata kura karibu mil.9 na mwaka 2010 wakapata milioni 5 . walipoteza close to 4 million votes over 5 years. my question to you is where did they exactly loss all these votes from(geographically)?? ktk research yenu mlioifanya na je maeneo gani yanaitaji mkazo ili kuzipindua hizo million 4 zije upande wenu kwa sababu naamini 2015 dis satisfied voters kwa upande wa ccm wataongezeka especially kwa hili suala la katiba.
 
Mkuu Pasco sijaelewa unazungumzia nyomi au hoja? Maana nyomi ni jambo moja na kushinda uchaguzi ni ishu nyingine kabisa japo vinashabihiana.
 
Last edited by a moderator:
Ritz unaijua Mbugani wewe! Tazama utaelewa tu
 
Attachments

  • 1412024050289.jpg
    1412024050289.jpg
    106 KB · Views: 6,589
  • 1412024084169.jpg
    1412024084169.jpg
    80.6 KB · Views: 6,514
  • 1412024117629.jpg
    1412024117629.jpg
    89.3 KB · Views: 6,437
  • 1412024141436.jpg
    1412024141436.jpg
    85.7 KB · Views: 6,563
  • 1412024162316.jpg
    1412024162316.jpg
    70.4 KB · Views: 6,604
Kwa swala la kuchagua nani kushika usukani wa kugombea Urais ndilo jambo litakalo wasambaratisha UKAWA!
Kwanza Tujiulize UKAWA ni chama cha Siasa?
Mtu an aye faa kuwa Rais ni Lipumba lakini sidhani kama Chadema na Bavicha watakubali Lipumba kuwaongoza!

Slaa amesha chokwa kabisa na Mbowe hana sifa kabisa!

bro, sidhan kama hilo litakuwa tatizo sana kwani tukumbuke hata samweli sita alitaka kupewa nafasi ya kugombea uraisi kwa tiketi ya CDM, hivyo cjui tatizo liwe kwa vyama vingine! lkn naamini wakisimamisha mtu mmoja wanachukua dola kwan. ahsante,
 
kaka Tumaini heshima mbele naomba msaada wako CCM mwaka 2005 walipata kura karibu mil.9 na mwaka 2010 wakapata milioni 5 . walipoteza close to 4 million votes over 5 years. my question to you is where did they exactly loss all these votes from(geographically)?? ktk research yenu mlioifanya na je maeneo gani yanaitaji mkazo ili kuzipindua hizo million 4 zije upande wenu kwa sababu naamini 2015 dis satisfied voters kwa upande wa ccm wataongezeka especially kwa hili suala la katiba.
Kamanda mbona unaenda mbali sana ungeulizia tu matokeo ya uchauzi Majimbo mawili Chalinze na Kalenga matokeo yalikuaje.
 
Pole sana ila zamu hii hamchomoki mbinu zenu zote zipo mikononi mwangu nitakuwa nafumua moja baada ya nyingine nadhani mnakumbuka video yenu feki niliwafanyaje.
 
Back
Top Bottom